Ilipoishia “Haraka nikiwa nimevalia pensi na tisheti nilielekea huko, kweli niliona Kijiwe cha Watu watatu hivi ambao baada ya kuniona Mimi walikaa tayari, nilitoa ishara ya vidole ambayo Juma Baro aliniambia, ilikuwa ni ishara ya kuwaambia kuwa kuna amani, ishara hiyo ilikuwa ikitumiwa na Wauza unga pekee, walipoona Ishara hiyo walikaa kisha nilisogea hadi hapo, nilinunua kete mbili za madawa kwa shilingi elfu 20 kisha nilirudi kwa Mama Nesha nikiwa na shahuku ya kutuliza kiu yangu.
“Jojo?” Alisema Mama Nesha baada ya kusikia mlango ukifunguliwa
“‘Ni Mimi Mama, nimerudi” Nilisema mkononi nikiwa na Juisi ili kusiwe na maswali. Endelea
SEHEMU YA SITA
“Haya namalizia kupika kikiwa tayari nitakuja kukuita” alisema Mama Nesha kwa sauti ya mbali akiwa Jikoni nami nilimjibu
“Sawa Mama” Basi nilipitiliza hadi Chumbani kwangu huku ile kiu ikizidi kuongezeka hadi nilisahau kufunga mlango, nguvu zilianza kuniisha nikawa nafungua kete huku nikiwa natetemeka, nilikuwa nimekaa chini, nilifanikiwa kufungua kisha nilianza kuvuta madawa kwa pupa sana, kwakuwa nilikuwa nimeshazoea wala hayakunipa shida sana.
Nilivuta kwa nusu saa hadi niliona akili ikisizi kama vile nilikuwa nataka kuingia usingizini, kumbe Mama Nesha alikuja Chumbani kuniambia kuwa chakula kipo tayari, aliniona nikiwa ninavuta madawa sababu mlango ulikuwa wazi
“Jojo” alisema Mama Nesha kwa mshituko Mkubwa
“Unatumia madawa ya kulevya Jojo?” Aliuliza kwa mshituko akiwa amenisogelea, alinikata hamu zote nikamtazama kama mwizi aliyefumwa akiiba, sikutaka Mtu yeyote ajuwe kuwa nilikuwa natumia madawa ya kulevya
“Kumbe ndiyo maana ulipoteza fahamu kwa siku mbili ni sababu unatumia madawa ya kulevya, hii taarifa nampa Baba Nesha kisha naenda polisi sitaki uje utuletee matatizo” Alisema Kisha alianza kuondoka kwa haraka pale chumbani, kiukweli madawa yaliniondoa utu wangu kabisa, nilibadilika kutokana na Maisha niliyoishi mwote nilimopita, nilifikiria kumuuwa Mama Nesha
Haraka nilimkimbilia Mama Nesha hata kabla hajafika chumbani kwake, nilimkaba shingo yake kwa nguvu sana sababu madawa yalikuwa yakinipa nguvu, nilihakikisha namuuwa Mama Nesha bila huruma huku madawa yakishinikiza kufanya hivyo.
“Jooo Joo, unanii…uwaa” Alisema Mama Nesha lakini sikujali hata mateso aliyokuwa akiyapata, sikutaka kuingia matatizoni kabisa. Niliendelea kukaba shingo yake hadi hatua ya mwisho ambapo alilegea kabisa na kufariki. Nilipomuuwa Mama Nesha ndipo akili yangu ya kawaida iliporejea, niliwaza kukimbia msala huo.
Haraka nilirudi chumbani kwangu, nilichukua begi na vitu vyangu vyote kisha niliondoka, nilikimbilia stendi nilipanda gari ya kurudi Dar. Nilikuwa nimechanganikiwa kabisa, uzuri ni kuwa Baba Nesha alikuwa amesafiri
“Dada futa pua yako kuna uchafu” Alisema Mkaka aliyekaa siti moja na Mimi, aliuwona ule unga eneo la pua yangu ila hakujuwa kama ulikuwa ni Unga wa madawa ya Kulevya
“Asante sana” Nilijibu kisha nilijifuta haraka sana, ilikuwa ni mishale ya saa 9 Mchana, nilifika Dar saa 1 Usiku. Sikujuwa niingilie wapi usiku ule, pesa iliyobakia ilikuwa chache sana. Usiku ule niliona ni bora nitafute Gesti nilale
Nilipata gesti maeneo ya Temeke Mwisho kule kwa nyuma, nililala hapo Usiku huo hata sikukumbuka kula. Asubuhi niliona taarifa ya habari ikielezea juu ya Mauwaji niliyoyafanya ila uzuri ni kuwa hakuna aliyekuwa na picha yangu ila tu jina la Jojo ndilo lililo tajwa, nilimuona pia Baba Nesha akisema kwa uchungu na maumivu makali sana, alielezea jinsi alivyoniokota Shambani kwake na kunifanyia wema, yalikutwa madawa ya kulevya kwenye kile chumba ambacho nilikuwa nikiishi. Roho iliniuma sana ila sikuwa na jinsi sababu tayari nilishaamuwa kukimbiza Maisha yangu vinginevyo ningekamatwa na polisi.
“Nimekuwaje Mimi Jojo?” Nilisema kwa maumivu makali sana ndani ya moyo wangu, sikutegemea kabisa kama ningefikia hatua ya kuwa Muuwaji. Nilifikiria sana niliona ni bora nitafute pesa nirudi nyumbani kwetu ila sikuwa na kazi. Nilibakiwa na shilingi Elfu 10 tu ambayo ilikuwa ndiyo pesa pekee niliyonayo, niliiangalia huku nikitafakari
Ghafla mlango uligongwa, nilishtuka sana, nilihisi ni polisi maana kesi ya kuuwa ni kubwa mno, niliuliza
“Nani?”
“Nahitaji kufanya Usafi” nilisikia sauti, nilijuwa tu atakuwa ni Mtu wa Usafi wa ile Gest, niliangalia saa ya ukutani niliona ni saa 3 asubuhi, muda wa Mimi kuondoka pale Gest uliwadia, nilienda kumfungulia kisha aliniuliza
“Unalipia tena au unaondoka?”
“Naondoka, ila nitarudi, naomba nikuachie Begi langu tafadhali”
“Mh! Labda ukamuombe yule Mkaka wa mapokezi maana mimi sihusiki kabisa na hayo, muombe atakukubalia tu ilimradi kuwe na usalama”
“Usalama upo Dada yangu” Basi, kwakuwa nilikuwa nimeshajiandaa, nilikuwa nimevalia suruali nyeusi na raba nyeusi, juu shati jeupe nilielekea Mapokezi kumuomba Mkaka wa Mapokezi anihifadhie begi langu
“Habari Kaka yangu”
“Salama” alinijibu akionesha sio Mtu wa Stori nyingi
“Samahani Kaka yangu naomba unihifadhie Begi langu kuna mihangaiko nikaifanye nikirudi nitalichukua” Nilisema kwa kujiamini kama vile mfanyabiashara aliyetokea mkoani kuja Dar kununua bidhaa, yule Mkaka kwa umakini sana kisha aliniuliza
“Kuna usalama?” Nilijichekesha kidogo kisha nilimjibu “Ndiyo Kaka yangu”
“Fungua tuone kuna nini!” Alisema akiwa ananikodolea macho kama Askari wa Barabarani
Nilijiamini sababu sikuwa na chochote cha kushangaza, nilifungua begi nikatoa nguo zote
“Ni nguo zangu tu Kaka yangu”
“Sawa liache ila hakikisha unalirejea leo leo” Alinisistiza kwa ishara ya Kidole, nilimuaminisha kuwa nitalifuata japo sikuwa na uhakika maana hata sehemu ya kwenda kuliweka lile begi sikuwa nayo, nilirejesha nguo kwenye begi haraka sana kisha nilimpatia lile begi
“Asante Kaka yangu jioni nitarudi Baada ya Mizunguko”
Basi niliondoka pale, hadi kituo cha magari ya kuelekea Mjini. Niliona Magari ya Kariakoo, Tabata, Ubungo, niliona ni bora nielekee Ubungo maana jina hilo halikuwa ngeni kwangu kuliko Kariakoo na Tabata.
Nilikuwa mwingi wa kuwaza, nilitoa ile Elfu 10 kisha kondakta aliniambia hana Chenji atanipatia mbele, basi nikatulia zangu. Nakumbuka ndani ya gari waliweka redio ya Clouds kipindi cha Leo tena ikawa inasikika ile habari ya Mimi kumuuwa Mama Nesha.
Nilishtuka sana nikahisi kama nimegundulika kuwa ndiye niliyeuwa maana niliona kama watu wananiangalia kumbe hata haikuwa hivyo bali ni wenge langu tu
“Konda nashuka” Nilisema huku nikiwa kwenye hekaheka za kupishana na watu kwa nguvu ili nishuke
“We Dada si ushuke taratibu” Alisema Mdada mmoja, wala sikujali nilisukuma Watu hadi nilipofika mlangoni, hata sikukumbuka chenji yangu nilishuka kisha niliingia mtaani, niliona kabisa nilikuwa nimechanganikiwa kabisa. Kila niliyekutana naye niliona ni Polisi na anakuja kunikamata, nikawa kama Chizi jumlisha na madawa ya kulevya amabyo nilikuwa nikiyatumia. Ilikuwa ni maeneo ya Buguruni Sheli, niliongoza njia ya kuelekea Vingunguti kupitia kwa Mnyamani.
Nilitembea kwa umbali mrefu sana bila hata kuhisi kuchoka hadi nilipofika Machinjio ya Vingunguti, nilishuka na ile barabara ya kuelekea Barakuda, nilipofika Kwenye Daraja nilituliza wenge langu. Nilikuwa wa hovyo sana kuliko hata ninavyoweza kuelezea hapa
Nilitembea taratibu, njaa ilianza kunichapa huku ile hamu ya kuhitaji madawa ya kulevya ikizidi kuniingia. Kila aliyenitazama aligundua haraka kuwa nilipoteza uwezo wa kujiamini, rangi na asili yangu ya uarabu ilifunikwa na mawazo nikawa kama Muarabu aliyefirisika. Ilifika mahali hata viatu niliviona vizito, nilivivua na kuvishika mkononi, nilitafuta sehemu nikakaa
Mwili ulijaa arosto ya Madawa ya kulevya mno, nilijilaza chini ya Mti nikiwa nimejikunyata. Niliwaza nikutane na Shonaa anisaidie lakini sikujuwa alikuwa akiishi wapi, sikuwa na simu wala nilikuwa simfahamu Mtu yeyote ndani ya Jiji la Dar-es-salaam.
Nilikuja kushtuka giza lilikuwa limeingia, mwili ulikuwa hauna nguvu kabisa. Kumbe pale nilipokuwa nimelala palikuwa ni maskani ya wavuta bangi, moshi wa Bangi ulipopita kwenye pua zangu nilijikuta nikisisimka sana, nilimuomba jamaa aliyekuwa anavuta akanipa
Niliivuta haraka haraka kama vile Mtu mwenye njaa kali anapopata chakula katika mazingira asiyoyategemea.
Wahuni wote walinishangaa sana kisha ukimya ukawa umetawala, hata sikuchukua dakika moja nilikuwa nimeumaliza ule msokoto, basi liliibuka shangwe kutoka kwao wakinisifu kuwa Mimi ni jembe. Nilicheka pia maana nguvu ilikuwa imeshaniingia mwilini, wahuni walikuwa ndiyo wanangu.
Basi tulikaa pale wakiwa wanapiga stori zao, kulikuwa na ubaridi fulani hivi ambao kila nilipovuta Bangi nilihisi joto la kutisha lenye raha ndani yake. Kadhaa waliondoka akabakia Jamaa mmoja tu ambaye alianza kuniuliza maswali ya hapa na pale
“Unaitwa Nani mrembo?” Aliuliza akiwa anacheka cheka, alikuwa teja
“Jojo”
“Oh Jojo jijooo…Hahaha! Naitwa Domingo, mimi ndiye niliyepiga kampeni zote za CCM mwaka 1890 Nchini Japani” Alisema, zilikuwa ni stori za kuchekesha sana ambazo kwa muda huo niliona zilikuwa kweli kwasababu nilikuwa muathirika wa madawa hivyo akili yangu ilijaa uteja mno
“Ha!ha!ha! Wewe ni noma” nilisema nikiwa ninafurahi
“Sema nini Jojoo…twenzetu mageto tukale raha au unasemaje?” Aliuliza Domingo
“Poaa” Nilijibu hata sikufikiria Chochote, Tuliondoka tukiwa tunapiga Stori za ajabu ajabu zilizotokana na bangi
Gheto lenyewe lilikuwa ni kiota kilichojengwa kwa mifuko kando ya Mto msimbazi.
“Hili ndiyo ghorofa langu Jojo, nimekuelewa sana ujuwe” Alisema Domingo, Bangi zilinifanya nione ni kweli ghorofa, basi tulilala na kufanya mapenzi hapo bila hata kujuwa afya ya Domingo, Maisha yangu Mimi Jojo yalizidi kuharibika
Asubuhi, Bangi ilikuwa imeondoka. Nilijishangaa mahali nilipokuwa nimelala, huyo Domingo nilimtazama mara mbili, alikuwa amejawa na chawa kwenye mwili wake, alikuwa na ukurutu wa kutosha alafu nywele zake zilibadili rangi na kuwa za dhahabu kutokana na uchafu
“Nini hiki Jojo?” Nilijiuliza, nilitema Mate, japo nilikuwa teja lakini sikufikia hatua ya kuwa Mchafu. Haraka nilitafuta viatu nikaondoka zangu pale nikamuacha Domingo akiwa amelala. Watu walioniona nikiwa ninatoka Pale walinishangaa kutokana na uzuri nilionao
Basi nilirudi kule Buguruni kwa kufuata ile barabara niliyokuja nayo Barakuda. Nilipoteza muelekeo wa Maisha kabisa, Jojo hali yangu ilikuwa mbaya sikula Tokea nilipokula kule Rufiji, niliona Vijana waliokuwa wakiomba omba kwenye magari yaliyo kwenye foleni, nilijiangalia nikaona ni bora nami nikaombe msaada mana kuna Wakati nilikuwa najitambua kabisa na kujuwa kuwa sipaswi kuyaishi maisha ya Uteja
Niliomba kwenye gari moja badala ya Jingine, wengine walinikebehi, wengine hawakutaka kunisikiliza kabisa, gari ya mwisho nilimkuta Msanii mkubwa sana wa kike hapa Tanzania ambaye siwezi kumtaja jina lake, alikuwa ndani ya gari nzuri sana akiwa naye anasubiria gari zianze kuondoka, niligonga kioo chake, alipofungua ndipo nilipomuona kwa uzuri, alinifanya nitabasamu sababu sikuwahi kumuona ana kwa ana
“Nikusaidie nini?” Aliuliza huyo Msanii maana nilikuwa namkodolea macho tu hata kusema nilikuwa siwezi
“Naomba msaada Dada yangu sina pa kuishi, sina kazi, nahitaji kurudi kwetu Tabora” Nilisema, aliniangalia kwa muda mrefu bila kusema chochote kisha alimgeukia Mwanaume aliyekuwa naye kwenye gari nahisi alimuuliza kwa ishara kama anisaidie au aniache, yule Mwanaume alinitazama juu chini kisha akamwambia
“Mchukue”
“Ingia kwenye gari” ilikuwa kama ndoto vile, nilifungua mlango wa gari ili niingie kwenye gari. Kabla hata sijaingia nilihisi uzito kwenye mgongo wangu alafu nilipata nguvu ya kuuliza
“Nani wewe!” Niliuliza kwa sauti ya juu mno kisha niliona kama vile Dunia ilikuwa imesimama, ghafla nilisikia sauti ya kugongwa kwa mlango. Mara nilijikuta nikirushwa pembeni, nilitumia nguvu ya mwisho kuangalia niliona pikipiki ikianguka kando yangu ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa nimepata ajali ya Pikipiki. Sikuelewa kilichoendelea, mzimu wa laana na matatizo uliendelea kuniandana. Nini Kitaendeea? Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?
Usikose SEHEMU YA SABA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx
11 Comments
Awesome thanks
😍😍😍
Daah imenoga atar kiongoz
Daaaah
Unge onganisha ya saba tu maana umetuacha na alosto
Lahaulaa
Daah imenoga atar kiongoz
Nimeipenda pia nimefunzwa kitu
Jojo jijooo😂😂😂 ila mateja bana
Sijui kwanini nakua n arosto ya hii kama Jojo na dawa zake
sehemu ya saba please
Mzigo hatari unazidi kuelekea pazuri keep it up…..