Ilipoishia
“Ingia kwenye gari” ilikuwa kama ndoto vile, nilifungua mlango wa gari ili niingie kwenye gari. Kabla hata sijaingia nilihisi uzito kwenye mgongo wangu alafu nilipata nguvu ya kuuliza
“Nani wewe!” Niliuliza kwa sauti ya juu mno kisha niliona kama vile Dunia ilikuwa imesimama, ghafla nilisikia sauti ya kugongwa kwa mlango. Mara nilijikuta nikirushwa pembeni, nilitumia nguvu ya mwisho kuangalia niliona pikipiki ikianguka kando yangu ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa nimepata ajali ya Pikipiki. Sikuelewa kilichoendelea, mzimu wa laana na matatizo uliendelea kuniandana. Endelea
SEHEMU YA SABA
Nilizinduka nikiwa Amana Hospital, daktari alikuwa kando yangu akiangalia jinsi nilivyokuwa nikiamka kutoka katika Usingizi mzito wa ile ajali, nilikuwa na maumivu makali ya Mgongo
“Tulia utakuwa sawa” Alisema Daktari huyo ambaye alianza kukagua macho yangu kisha aliniuliza
“Unaitwa Nani?”
“Naitwa Jojo” nilijibu kwa maumivu makali sana.
“Unaishi wapi?” Aliniuliza, nilitikisa kichwa ishara ya kuwa nilikuwa sina makazi
“Ndugu zako wapo wapi?”
“Sina ndugu hapa, wapo Tabora…..aliyenileta hapa yupo wapi?” Nilimuulizia yule Msanii
“Umeletwa hapa na wasamalia wema tu hata hivyo wameondoka zao”
“Msanii hajafika hapa?”
“Hakuna aliyekuja kukuona” Alijibu yule Daktari kisha aliniambia
“Unapaswa kwenda soba kwanza ili kukuondoa kwenye matumizi ya madawa, vipimo vimeonesha damu yako inakiwango kikubwa cha madawa ya kulevya” Alisema yule Daktari kisha alisema
“Gharama zote zitalipwa na Hospitali”
“Asante sana” nilisema, nilifurahi kwa upande mmoja sababu sikupenda kuwa Mtumwa wa madawa ya kulevya tena.
Nilipopata unafuu nilipelekewa Soba, nilifundishwa vitu vingi mno, nilikutana na wengine ambao walikuwa wameathirika zaidi na Madawa ya kulevya, niliishi huko kwa zaidi ya miezi sita hadi nilipopona kabisa na kuacha matumizi ya dawa za kulevya. Baada ya hapo, nilikabidhiwa kwa Mama mmoja ambaye alikuwa akiitwa Mama Zahara, alikuwa ni Mama fulani mnene hivi
“Utaenda kuishi kwake sababu huna mahali pa kwenda kuishi, huko mtaani utarudi tena kwenye ulevi” Alisema Mtu wa Soba. Nilifurahia sana kwenda kuishi kwa huyo Mama, niliona naenda kufungua ukurasa mpya wa Maisha yangu, ukurasa ambao utatengeneza upya Maisha yangu.
“Utaishi kwangu kwa Muda kisha utaamuwa kama utaendelea au utarudi kwenu Tabora” Alisema Mama Zahara, basi tuliingia kwenye gari yake kisha tulienda nyumbani kwake, alikuwa na nyumba nzuri sana kubwa ambayo alikuwa akiishi na Wasichana waliotoka Soba.
Niliishi hapo kama Mwanafamilia, Maisha yalikuwa mazuri sana, tulipewa kila kitu, hadithi za walio wengi pale walikuwa hawana makazi kama Mimi, wengine waliondoka na wengine tulibakia.
Miezi miwili ilikatika nikiwa hapo kwa Mama Zahara, Siku moja Mama Zahara alisafiri, alituaga kuwa anaenda Mombasa Kenya. Alituhasa sana kuendelea kuishi kwa upendo wa hali ya juu sana na pia kuishi kwa kujali afya na malengo yetu, alipoondoka kila mmoja aliachiwa pesa yake kwa ajili ya kujikimu kidogo maana alikuwa anaenda kukaa huko kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kulikuwa na Mdada aliyeiywa Salome, tulijenga ukaribu sana, alikuwa na hela nyingi kuliko Msichana yeyote pale, nilipata shahuku ya kumuuliza
“Hivi Salome hizo pesa unatoa wapi?” Kwanza alicheka kisha alinijibu
“Nazitafuta Jojo, unafikiria pesa inaokotwa?”
“Sijamaanisha kuwa inaokotwa ila nimeuliza ili nijuwe”
“Jibu zuri ni matendo, kesho ni Jumamosi, usiku tutoke” Alisema Salome, alikuwa ni Mdada fulani mnene kiasi mweusi, macho yake yalikuwa makubwa
“Usiku tena?”
“Ndiyo, hofu yako ndiyo umasikini wako, ni lazima Jojo ujifunze kutengeneza pesa kwa ajili ya Maisha yako, unafikiria siku ukiondoka hapa kwa Mama Zahara utapewa pesa ya kuanzia Maisha? Utapewa nauli tu, sasa utaishi vipi huko kwenu?” Alisema Salome, maneno yake yalikuwa na mashiko kwenye ufahamu wangu, alichokisema niliona kina ukweli
“Sawa tutaenda” Nilimkubalia bila kujuwa alikuwa anataka kunipeleka wapi, wakati huo ule uzuri wangu ulikuwa umerejea tena kwa kasi sana sababu nilikuwa naishi vizuri sana pale kwa Mama Zahara.
Siku iliyofuata Usiku tulitoka tukiwa tumevalia vinguo vifupi, japo nilimuuliza tulikuwa tunaenda wapi ila aliniambia nitaona, nilimuamini sababu alikuwa ndiye rafiki yangu pale kwa Mama Zahara.
Tulichukua Taxi hadi Magomeni, ilikuwa mishale ya usiku wa saa tano, tulipofika aliniambia tusubirie. Tulisimama barabarani tu, baridi lilikuwa kali sana pale kiasi nilikuwa najikunyata.
“Tutasimama hadi saa ngapi Salome? Mimi nimechoka” nilisema, kiukweli tulisimama kwa zaidi ya nusu saa, alikuwa akisimamisha magari binafsi ya Watu lakini yalikuwa hayasimami
“Salome nimechoka mwenzio” Nilisema huku hasira ikianza kunishika
“Unataka kuharibu sasa si ndiyo?”
“Salome hii ni Biashara ya Ngono unaifanya si ndiyo? Sasa si bora ungeniambia kule nyumbani unafikiri ningekuja huku Mimi? Yaani sijui mimi nakuwaje Aisee huwa naingizwa kwenye mambo yasiyofaa kirahisi sana” Nilisema kwa kujilaumu, Salome alirudi kuendelea kusimamisha gari
Nilikaa pembeni, Idadi ya Wanawake hapo ilianza kuongezeka, walivalia kama sisi tulivyovaa na wengine walikuwa wakivuta sigara, niliyachukia Maisha yale kabisa, nilimfuata tena Salome
“Kama huwezi kuondoka na Mimi basi nitaondoka mwenyewe Salome” Nilisema
“Nipe dakika tano tu nakuomba Jojo kisha tutaondoka” Alisema Salome
“Sawa ni dakika tano tu baada ya hapo sitakuwa na muda wa kuendelea kukusubiria” Nilisema kisha nilirudi kuketi kando kidogo ya waliposimama wao
Baadaye niliona gari ikisimama, Salome alianza kuzungumza na Mtu wa kwenye gari japo sikusikia walichokiwa anakizungumza ila nilihisi itakuwa amepata Mteja
Alikuja akaniambia
“Si ulikuwa unataka kwenda nyumbani? Basi wewe nenda mimi nitarudi asubuhi” Alisema Salome
“Sasa ulichoniletea huku ni nini Salome? Aaah” nilisema kwa kuchukia sana
“Nenda Jojo tutaongea nyumbani ila usimwambie Mtu yeyote” Alisema Salome kisha alikimbilia kwenye gari akapanda kisha gari iliondoka. Nilichukia mno istoshe kiatu kilikuwa kinanibana sana mguu wa kushoto, niliamuwa kukivua ili nisizidi kuumia.
Nilisimama pembezoni mwa waliposimama wale wanawake wanaojiuza, nilikuwa nasubiria gari ya kurudi nyumbani. Ghafla nilisikia purukushani, nilipogeuka niliona wale wanawake wakikimbia huku na kule huku wakipiga mayowe. Nilihamaki, nilihitaji kujuwa wamepatwa na nini, punde niliona Watu waliovalia sare za polisi.
Nami nilianza kukimbia, polisi wawili wakawa wananikimbiza, walinikamata mita chache tu kabla hata sijafika mbali.
“Naomba mniache tafadhali” nilisema wakiwa wananipeleka kwenye gari ya polisi
“Wanawake wa Siku hizi bwana, Mwanamke mzuri kama wewe ujiingize kwenye biashara ya ukahaba, twende tukakufundishe kazi huku” Alisema Askari mmoja
“Mimi siyo kahaba nilikuwa nasubiria gari nirudi nyumbani, sijawahi kuuza mwili katika Maisha yangu” Nilijaribu kujitetea kidogo ili niachwe.
“Twende utajuwa huko huko kama ulikuwa ukiifanya hiyo biashara au ulikuwa hauifanyi” Alinijibu yule askari
“Kweli mimi sijafanya kama mnataka nimpigie ndugu yangu ambaye nilikuja naye huku” Nilisema tena
“Ndugu yako atakuja kituoni kutoa maelezo huu siyo muda wa maelezo” Alinijibu Polisi mwingine, tayari tulikuwa tumeshafika kwenye gari. Waliniingiza kwenye gari ya Polisi, Wale makahaba nao walikuwa wamekamatwa pia.
Tulipelekwa kituo cha Polisi, tulitupwa Mahabusu. Siku iliyofuata niliitwa na Polisi nikaambiwa niwapigie ndugu zangu ila kibaya sikuwa na simu wala namba ya Mtu kichwani, angalau ningempigia Salome au hata Mama Zahra lakini hata hivyo Mama Zahra alikuwa nje ya Nchi ningempata vipi?
“Afande siijui namba ya Ndugu yangu hata mmoja ila naomba nipo chini ya Miguu yako twende nyumbani kwetu,
watakuthibitishia kuwa Mimi sijiuzi kabisa” Nilisema, yule Polisi alicheka akasema
“Hayo ndiyo maneno yenu, nakusikitikia sana Ndugu yangu sababu Rais ametoa maagizo makali sana kuhusu Biashara mnayofanya, siku tatu zijazo mtafikishwa mahakamani na mtahukumiwa kufungwa Miaka mitatu au Faini isiyopungua Milioni 6” Alisema yule Polisi
“Kaka yangu wewe una ndugu au hata Dada kama Mimi, naomba usimame kama Kaka kwangu niangalie Mdogo wako ninavyoteseka” Nilisema
“Nikisema nisimame kama Kaka nitasimama kwa wangapi? Tutakomesha hii Biashara kweli? Nenda ukafunzwe na Walimwengu huko uendako” Alisema kisha nilirudishwa Mahabusu. Ni Mimi peke yangu ndiye niliyekuwa nikilia ndani ya Mahabusu sababu sikuzoea maisha yale kabisa.
Nilionekana kero kwa wale mahabusu wengine wakawa wananisema sana nijikaze sababu Biashara ile ndiyo kila kitu, nilijaribu kuwaambia kuwa Mimi siyo kahaba ila hawakutaka kunielewa kabisa wakasema kama siyo kahaba nilifikaje pale? Na nilijuana vipi na Salome wakati Salome ni kahaba wa muda mrefu?
Sikuwa na utetezi kabisa, niliishia kulia tu. Ukurasa wangu mzuri wa Maisha ambao ulifunguka na kunipa furaha sana ulianza kuchanika, nilijikuta nikirudi kwenye Maisha yaliyojaa giza tena, niliishi hapo kwa hizo siku mbili na hakuna aliyekuja kunitafuta.
Siku ya tatu tulipelekwa Mahakamani, Polisi walisimama kama Mashahidi, nililia sana Mahakamani ili niachiwe lakini haikusaidia. Hakuna hata mmoja kati yetu aliyekuwa na kiasi cha Shilingi Milioni 6 ili asifungwe, sote tulihukumiwa kifungo cha miaka mitatu.
Tulipelekwa gerezani, siku tunavalishwa sare za Gerezani na kukatwa nywele zetu ndipo nilipoamini kuwa nilikuwa nimetumbukia kwenye shimo lenye giza, nilifikiria Miaka mitatu ilivyokuwa Mingi nitaweza kuishi gerezani kweli? Kama kulia nililia sana hadi mwili ulishika moto lakini hakuna kilichosaidia, kilio changu na machozi yangu yaligeuka kuwa chozi la samaki lisombwalo na maji, hakuna aliyenisikia wala kuthamini chozi langu, kila Mtu alikuwa na matatizo yake ndani ya Gereza hivyo isingelikuwa rahisi kusikilizwa.
Nilikubaliana na hali halisi, niliyaanza Maisha mapya ndani ya gereza. Maisha yaliyojaa ubabe, uonevu, utata, manyanyaso na kazi ngumu sana. Tulifanya kazi ngumu na kupewa chakula kidogo tena hicho kidogo anakuja Mtu anakuchukulia kwa ubabe wake na hakuna cha kumfanya.
Nilimpata rafiki ndani ya gereza, aliyeitwa Isabela naye alikuwa Mtu wa Tabora hivyo tulikuwa na memgi ya kuzungumza. Yeye alihukumiwa kwa kosa la kumkata Mkono kimada wa Mume wake, japo tulikuwa katika nyakati ngumu sana ila tuliishia kucheka tuu maana hakukuwa na njia nyingine zaidi kutumikia adhabu, Mume wake hakuwahi kuja kumuangalia Gerezani kwa miezi zaidi ya mitatu. Isabela alihukumiwa kifungo cha miaka miwili tu
“Ukishamaliza kifungo una mpango gani?” Nilimuuliza Isabela tukiwa shambani tunalima
“Kurudi Tabora tu maana nimegundua Mume wangu hanipendi kabisa licha ya kumzalia Mtoto mmoja, angekuja kuniona angalau ningekuwa na tumaini. Ila najutia sana hasira zangu, ona nateseka mwenyewe kwa ajili ya mtu ambaye hajali chochote kuhusu Mimi” Alisema, niliona jinsi alivyokuwa na maumivu moyoni, ghafla nilijiona sina matatizo kabisa.
“Pole sana Isabela, yataisha tu. Ukifika Tabora nenda nilipokuelekeza waambie nipo Gerezani” Nilisema.
Basi Maisha ndani ya Gereza yaliendelea, siku moja baada ya kazi ilikuwa ni majira ya saa 7 Mchana, ulikuwa ni muda wa kupata Chakula. Tulikuwa tukipanga mistari miwili kwa ajili ya kupata Chakula, msitari wa kwanza nilikuwepo Mimi, sasa katika tazama tazama nilistaajabu nilimuona Sarafina, yule Mdada ambaye alifukuzwa na Shonaa kisa Mimi, nilitamani kumuita ila nilikumbuka kuwa alikuwa na hasira na Mimi, nilimgeukia Isabela nikamuuliza
“Yule yupo hapa kwa muda gani?” Nilimuonesha kidole Sarafina
“Nimemkuta hapa, anaonekana kahukumiwa muda mrefu ila inasemekana aliiba pesa kwa tajiri mmoja”
“Vipi unamjuwa?”
“Ndio namjuwa” Basi baada ya kuwa tumeshachukua chakula tulienda kula, Isabela aliniuliza
“Unamjua vipi yule”
Nini Kitaendeea? Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?
Usikose SEHEMU YA NANE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx
6 Comments
Aiseee huyo dada nae kama chizi
Kila siku ni ukurasa mpya maishani
Asante
Looh jamani Jojooo anakuwa zuzu
sehemu ya nane please
Ndivyo mungu anatupitisha magumu ili kujifunza na kuwa bora zaidi