IlipoishiaTulienda moja kwa moja anapoishi Shonaa akaniambia kesho yake  atanipeleka kwa huyo Bosi, nilikuwa nimechoka hivyo sikuwa na  maswali mengi zaidi ya kuhitaji Kupumzika tu, kweli  nilipumzika hadi asubuhi kulivyo pambazuka. Shonaa aliamka  mapema sana, alikuwa amepangisha chumba kimoja na sebule,  nilienda hadi sebleni nilimsalimia 

“Mambo Dada?” Aliacha alichokuwa anakifanya kisha alitabasamu  akanijibu 

“Poa tu umeamka salama?” Aliniuliza 

“Ndiyo nipo sawa! Umedamka hivyo?” Nilimuuliza 

“Si unajuwa tena Maisha ya Mjini ndugu yangu, ukiendekeza  Usingizi utakufa masikini” Alisema kisha tulicheka, niliona  nimepata Mtu wa kuzungumza naye na kumuuliza maswali yangu 

“Jana ulisema utanipeleka kwa Bosi asubuhi hii” “Usijali, subiria nimalize kupasi nguo zangu” Alijibu Shonaa  

Endelea 

SEHEMU YA PILI

“Unaitwa Nani?” Nilimuuliza 

“Naitwa Shonaa, wewe ni Jojo Eeh?” 

“Ndiyo Naitwa Jojo” nilijibu huku nikiwa ninatabasamu. 

Punde mlango wake uligongwa waliingia wasichana wengine  wawili ambao walikuwa wamelewa, walisema maneno ya hovyo  hovyo kisha walipitiliza hadi chumbani, mmoja alinisukuma  nikaangukia kwenye kochi, kiukweli nilishtuka sana. 

“Usijali Jojo utazoea, ndiyo Maisha yetu” Alisema Shonaa  nilimsogelea 

“Ndiyo Maisha yenu? Ina maana mnaishi Watatu hapa?”  Nilimuuliza Shonaa, alinisogelea akaniambia, Bado watatu  hawajarudi 

“Eeeh?” Nilishangaa Watu sita wanaweza vipi kuishi hapo 

“Wewe ni wa saba Jojo, utazoea tu najuwa inakupa wakati Mgumu  sana. Atakaye wahi kurudi analala Kwenye kitanda, ukichelewa  kwenye kochi, ukichelewa zaidi unalala chini” Alisema Shonaa  kisha aliendelea na kazi yake, kusema ule ukweli nilijilaumu  kwanini nilikuja Dar, niliona ugumu ulio mbele yangu.  Nilitoka ndani nikampigia Msonjo ili ikiwezekana nirudi  Tabora mara moja, niliona ni bora kulala njaa kuliko Maisha  yale 

“Jojo tutapata wapi nauli ya wewe kurudi haraka hivyo?  Vumilia kidogo mbona mapema hivi unakata tamaa jamani?”  Ilikuwa ni sauti ya Msonjo 

“Sikia Msonjo, yaani siwezi kuvumilia japo kwa sekunde moja,  wewe haupo ila Maisha yanatisha hivi Watu wa Mjini ndio  wanaishi hivi? Chumba kimoja Watu saba?” 

“Jojo! Ngoja niongee na Bosi tuone inakuwaje!” Alisema Msonjo 

“Jitahidi nakuomba Msonjo nipo katika nyakati ngumu sana”  Nilisema kisha salio liliisha kwenye simu yangu, nilipogeuka  nyuma nilimuona Shonaa akitikisa kichwa chake, alikuwa  akisikitika. 

Shonaa alirudi ndani bila kusema chochote ila alikuwa  amesikia mazungumzo yangu, nilipofika ndani aliniambia 

“Jiandae tuondoke” basi nilielekea chumbani, yaani nilikuta  mazingira ya hovyo sana, jinsi walivyolala wamewekeana Miguu, 

mwingine alikuwa ametapika karibu na begi langu, kichefuchefu  kilinizonga. Nilijikaza tu hivyo hivyo nilibadilisha nguo,  kisha nilitoka. 

“Ndio unavaa hivyo?” Aliniuliza Shonaa 

“Ndiyo kwni kuna tatizo?” Nilimuuliza 

“Mmh! Haya twende” Alisema Shonaa kama vile kuna jambo  alitaka kusema. Tulipanda daladala hadi Sinza kwa Remi,  kulikuwa na kumbi kubwa mpya ya Starehe iliyoitwa Dar City  ndiyo ilikuwa ikimilikiwa na huyo Bosi aliyeitwa Muntaza. 

Tulienda hapo kwenye huo ukumbi, palikuwa pameshachangamka  asubuhi asubuhi, Watu walikuwa wakipiga mitungi kama hawana  akili nzuri, tena ilionesha walikuwa wamekesha hapo hapo,  ilikuwa ni siku ya Jumamosi. 

“Shonaa upo na mrembo” Alisema mmoja wa walevi kisha  alimshika shonaa titi, alafu Shonaa hakuonesha kuchukia ndio  kwanza alikuwa akicheka, nguvu ziliniisha 

“Kama kawaida si unanijuwa Mimi” Alisema Shonaa kisha  tuliingia kwenye chemba moja 

“Shonaa haya Maisha sitoyaweza” Nilisema 

“Jojo bado hujayaona Maisha tayari unasema hutoweza, sasa  unaweza kurudi kwenu Tabora na huna pesa hata ya kula? Acha  ujinga, fanya kazi hata mwezi mmoja kisha ndio  uondoke…..unakata tamaa mapema, inabidi upambane  kuhakikisha unapata pesa, hapa Mjini kila kitu ni pesa”  Alisema Shonaa akiwa amenikazia jicho, kisha aliongoza mbele  nami nilimfuata. Nilikuwa sijala ila Maisha niliyoyaona  yalinifanya nishibe, hebu fikiria Mtu anashikwa Titi mbele za  Watu alafu anacheka wakati Tabora Mtu umshike bega tu bila  ridhaa yake anakupiga kofi, nilitikisa kichwa changu 

Tuliingia kwenye chumba kimoja ambacho alikuwemo huyo  Muntaza, kilikuwa ni chumba kinachonuka sigara na pombe,  alikuwa na wasichana wawili makamo yangu. Aliwaondoa baada ya  sisi kuwa tumeshaingia na kuketi kwenye sofa jirani na  alipoketi yeye, nilijikuta naanza kukohoa kutokana na ule  moshi. Muntaza alikuwa ni pande la Mtu, alikuwa na cheni  nyingi na pete, alafu alikuwa na kitambi, umri wake ulionesha  alikuwa zaidi ya miaka 50 

Basi Shonaa alimsogelea na kumpiga busu huyo Muntaza,  nilitazama pembeni nikiwa ninakohoa.

“Wow!” Alisema Muntaza 

“Bosi huyu ni Jojo uliyeniagiza kumpokea” Alisema Shonaa,  nilijichekesha kidogo ila kiukweli moyo ulikuwa ukinienda  mbio sana. 

“Hukumuelekeza mavazi ya kuyavaa?” Alihoji Muntaza “Ndio Mwanzo Bosi nitaongea naye vizuri” 

“Ok! Muelekeze majukumu yake” Alisema Muntaza kisha aliondoka  hata bila ya kunisemesha chochote. 

Alpoondoka Muntaza nilizidi kukohoa, nilikuwa nimevaa gauni  na mtandio kichwani. 

“Jojo ukitaka kuishi hapa vziri kubali hali halisi ila  ukileta misimamo isiyo na maana utajikuta Mji unakushinda  huu. Hapa ndiyo ofisini kwako, kwangu na kwa wale wadada  wengine tuliowaacha kule nyumbani, mavazi ya hapa ni kama  yangu” Alivyosema hivyo nilimtazama alivyovaa, yaani alivaa  kikomdomu tu na vest, chini raba 

“Ukizubaa unapotea, kuwa mjanja” 

“Lakini kusema ule ukweli Shonaa haya Maisha sina uhakika wa  kuyaweza kabisa, najilaumu sana kuja huku Dar ila  aliyenitafutia kazi nimemuomba anisaidie kuongea na Bosi ili  anipe nauli nirudi kwetu” Nilisema. 

“Usijidanganye kuhusu kupewa nauli, hata Mimi nilikuja kama  wewe miaka miwili iliyopita, nilikuwa muoga nilikuwa nikilia  nirudi nyumbani lakini ilishindikana” 

“Lakini Shonaa mimi nimefiwa na Mama yangu mwezi uliopita,  nahisi nitakuwa namkosea sana kufanya kazi ya hivi, alinilea  katika mazingira bora sana” nilisema 

“Sawa alikulea katika mazingira bora ila hakuacha msingi  wowote, laiti kama angelikuachia msingi basi usingekuja huku  kutafuta Maisha, hata Mimi Mama yangu nimemzika miezi  michache iliyopita huko Kilimanjaro, nimerudi sababu hii ni  kazi inayoendesha Maisha yangu” 

Maneno ya Shonaa yalinikata sana kauli, niliona napaswa  kukubaliana na hali halisi japo bado tumaini langu lilikuwa  kwa Msonjo aliyenileta Dar. Kulikuwa na nguo zikizokuwa mle  kwenye chumba alinipatia nizivae, nilijitahidi kukataa lakini  aliniambia hakukuwa na sababu ya kutoka Tabora kuja Dar ni bora ningebaki Tabora. Basi nilizichukua nikabadilisha,  sikujiangalia mara mbili, yaani chupi ilikuwa ikionekana,  nguo zilibana na kushika mwili wangu, kila kiungo  kilijichonga. Kibaya zaidi aliniambia nisivae sidiria 

“Shonaa hivi siwezi kusema ukweli nitaweza vipi kutembea  jamani mbona unanipa wakati mgumu hivi” nilisema, Shonaa  alicheka sana. Kabla hata hajaongea chochote aliingia Muntaza 

“Yupo tayari?” Aliuliza 

“Ndiyo Bosi” 

“Haya akaanze kazi” Alisema kisha alijitupa kwenye Sofa akiwa  anakohoa. Ningefanyaje unafikiri? Nilitoka na Shonaa bila  ubishi wowote ila nilikuwa navuta vuta nguo zangu ili  zisinichonge hapa mbele kwa Bibi. 

Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza katika Maisha  yangu kufanya kazi ya Ubaamedi, nilikutana na vikwazo vingi  ikiwemo kushikwa shikwa lakini nilijitahidi kukwepa kadili  nilivyoweza. Saa 12 walikuja wengine, Mimi na Shonaa tulirudi  nyumbani kupumzika. Nilipewa elfu 10 kama pesa ya siku ya  kazi, niliiweka pembeni ili ikitimia pesa ya Nauli niondoke  zangu. 

“Umeionaje siku yako ya kwanza kazini?” Aliniuliza Shonaa 

“Nzuri tu” Nilisema kisha nilitoa tabasamu feki, sikutaka  tena kujionesha kuwa kazi hiyo nilikuwa siitaki, kwakuwa  niliona naweza pewa kila siku elfu 10 hivyo ningeweza kurudi  Tabora haraka sana. 

“Najuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwa  kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge,  sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi” 

Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwa  akinikagua, nilionesha lile tabasamu feki 

“Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibana  kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononi 

“Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamu  lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamu  lililotoka moyoni 

“Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengine  walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

 Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx

  

1 Comment

Leave A Reply


Exit mobile version