IlipoishiaJapo mambo yale yalikuwa mageni kwangu na yenye kuniumiza ila  yalinifundisha vitu vingi sana ambavyo hata kama ningesoma  hadi ngazi ya digrii nisingeliweza kujifunza. Usingizi  haukuja kabisaa nilikaa macho hadi niliposikia adhana  wakiazini msikiti wa jirani ndipo nilipofahamu kuwa palikuwa  pamepambazuka. 

Tulikuwa na zamu ya kwenda kule Dar City Mimi na Shonaa,  nilijiandaa. Muda ulienda nikiwa ninamsubiria Shonaa, Jua  lilipoanza kutua Shonaa alirudi akiwa mwenye furaha,  alinionesha kiasi cha pesa alichokiingiza. 

Kilikuwa ni zaidi ya laki moja, niliitamani pesa hiyo maana  kama ningeliipata basi ingenitosha kwa Nauli ya kuelekea  Tabora, aliketi lakini aliniona nikiwa sina fruaha kabisa. Endelea 

SEHEMU YA NNE 

“Mbona upo hivyo Jojo kuna tatizo?” Alihoji Shonaa, niliona  hata sura yke ilipoteza uchangamfu pia, ndipo nilipogundua  kuwa alikuwa akiumia pindi ninapokuwa sina furaha, ilinibidi  nimsimulie kilichotokea jana Usiku kuanzia tukio la kudeki  choo na lile la kutaka kubakwa. Shonaa alichukia sana,  alimfuata Sarafina Chumbani kwa hasira, sikutaka kwenda huko  ila nilisikia namna walivyokuwa wakigombana 

“Kama hauwezi wewe tafuta mahali pa kwenda kulala, yaani kodi  nalipa Mimi alafu umtese Mtoto wa Watu amekukosea nini? Gesti  zipo nyingi kwanini ulete Mwanaume hapa Sarafina?” Ilikuwa ni  sauti ya Shonaa iliyojaa hasria sana, nilijikuta nikitokwa na  machozi kwa namna ambavyo Shonaa niliyejuana naye kwa siku  

mbili tu anipambanie namna ile, nilijikuta nikisema pole pole  huku chozi likinibubujika 

“Bamedi siyo Malaya” Nilisema kisha nilikataa kwa kichwa  changu, tafsiri iliyokuwa imejengeka kwa wengi ni kuwa  Baamedi hawana utu, ni Watu walioshindwa Maisha, kupitia kwa  Shonaa nilipata somo kuwa moyo wa Mtu ni kichaka kikubwa  sana. 

“Unanifukuza Mimi kisa yule Dogo?” Alisema Sarafina kwa sauti  ya juu pia 

“Unamjuwa yule? Angelikuwa ni mdogo wako wa kuzaliwa naye  ungelimfanyia haya uliyoyafanya? Angebakwa je? Sarafina wewe  ni muathirika na unalijuwa hilo, ingekuwa hatari kiasi gani  kwa Jojo?” Alisema Shonaa kwa sauti iliyoambatana na Kilio 

“Unaamuwa kunidharirisha Shonaa si ndiyo, kuathirika ni jambo  la ajabu?” Alisema Sarafina, nilishindwa kuvumilia  nilijikutana nikikaa kwenye kochi taratibu huku nikiwa  ninalia, nililia kwa mengi kwanza namna ambavyo Shonaa  alionesha kujali juu yangu, pili niliwaza kama yule Mwanaume  angenibaka ingekuwaje? Licha ya kuwa na umri wa miaka 28  lakini bado nilikuwa sijakutana na Mwanaume yeyote yule. 

Nilisikia sauti ya Kofi kisha nilisikia sauti ya Sarafina “Unanipiga Mimi Shonaa?” 

“Ndio, kwasababu huna utu Sarafina, hujali chochote kile,  mbona mimi nawapenda nyie lakini hamnipendi kabisa?” Alisema  Shonaa kwa sauti yenye maumivu sana hadi roho iliniuma 

“Naondoka Sarafina, ila sitokaa kimya. Nitafanya kwa ajili  yako na Huyo Jojo wako” Alisema Sarafina kisha nilimuona  akipita mbele yangu akiwa na begi lake, alisimama akanitazama  kwa jicho kali sana kisha aliondoka zake.

Punde Shonaa alitoka chumbani akiwa anavuja chozi,  nilimkumbatia Shonaa, naye alinikumbatia, nilijiona nipo  kwenye mikono salama ya Mtu ambaye alikuwa tayari kuharibu  Maisha yake kwa ajili yangu 

“Pole sana Jojo, Mtu asiye na utu hafai kuitwa Mtu, Sarafina  nimemvumilia sana kwa tabia zake ila hali yake kiafya ndiyo  iliyonifanya nisimuache. Nilimpokea kama wewe nilivyokupokea  miezi kadhaa iliyopita, nilimchukulia kama Mdogo wangu ila  akauingia Mji kwa pupa sana akapata Ugonjwa” Alisema Shonaa,  nilijitoa mwilini mwake kisha nilimwambia 

“Sitaki kurudi tena Tabora” Kauli yangu ilimshangaza sana  Shonaa akaniambia kwa upole sana 

“Rudi nyumbani Jojo, rudi ukaishi Maisha yenye kumpendeza  Mungu wako, haya siyo Maisha ya kuishi. Nenda kakae karibu na  kaburi la Mama yako, tokea jana Nilipokuona ukiongea na simu  nilikuonea huruma sana. Nilienda kutafuta pesa kwa ajili  yako, hii hapa” Shonaa alinipa kile kiasi cha pesa ambacho  alikuja nacho. 

Moyo wangu ulikufa ganzi hadi nilijiuliza Shonaa alikuwa ni  Binadamu wa aina gani? Alikuwa ni Binadamu au Malaika? 

“Shonaa sitaki kukuacha peke yako” Nilisema nikiwa ninatokwa  na Machozi 

“Sitaki yakukute kama yaliyomkuta Sarafina, rudi nyumbani  ukaishi Maisha yaliyo Mema, umejifunza kitu kwenye Haya  Maisha na nina imani utakuwa balozi mzuri sana ufikapo  nyumbani” Alisema Shonaa, nilifuta chozi langu kisha  nilimfuta Chozi na yeye. 

“Asante Sana Shonaa Mungu azidi kukubariki katika Maisha  yako, sitakusahau hata siku moja na Daima nitakuweka katika  Maombi yangu! Umechukua nafasi ya Mama yangu japo umri wetu  unaendana” Nilisema, Shonaa alitabasamu akaniambia 

“Anayeweza kufanana na Mama yako Jojo ni Mama yako mwenyewe,  hakuna wa kufanana naye! Mimi ni rafiki yako tu” Basi  tulicheka pale kisha akaniambia 

“Utabakia hapa, Mimi naenda kazini, nitamdanganya Bosi kuwa  umetoroka na kurudi kwenu sawa? Kesho utaenda nyumbani Jojo”  Alisema Shonaa, aliondoka na kuniacha na tabasamu kubwa sana  kwenye uso wangu

Nilisali na kumwambia Mungu asante kwa wema alionitendea,  kusema ukweli Shonaa aliniomesha kitu cha tofauti sana na  jinsi ambavyo nilikuwa nafikiria. 

“Mungu akulipe Shonaa” Nilisema nikiwa naziangalie zile pesa,  zilitosha kabisa kufika Tabora na chenji ikabakia. 

Nilitoa pesa kidogo kutoka katika ile hela aliyonipa  nikanunua chakula cha Asubuhi na Mchana, jioni Shonaa  aliporudi alinieleza kuwa amewaambia wasichana aliokuwa  anaishi nao waondoke kwake, pia alinieleza kuwa alimwambia  Bosi kuwa nimetoroka 

“Basi Bosi alimpigia Simu huyo aliyekusafirisha kuja huku  sijui anaitwa Sonjo..” 

“Enhee ni Msonjo” 

“Basi huyo huyo, wakawa wanakupigia sana alafu simu yako  ikawa haipatikani, moja kwa moja wameamini kuwa umetoroka  Jojo” Alisema Shonaa 

“Asante sana Shonaa sitaacha kukushukuru kwa huu wema wako”  Nilisema 

“Usijali Jojo tupo pamoja ni lazima Binadamu tusaidiane  sababu hakuna anayeijua kesho yake, alafu nimekuletea zawadi”  Alisema Shonaa, alinipatia simu kubwa ya Kutachi, sikuamini  macho yangu, nilimkumbatia kwa furaha sana 

“Shonaa sijui hata thamani ya huu wema nitaulipa kwa kitu  gani, aah ni wema uliotukuka sana” Nilisema 

“Usijali Jojo, ipo siku tunaweza onana tena Mungu  akakusimamie huko uendako” 

“Nawe pia Ubaki salama Shonaa” Basi ilikuwa ni siku iliyojaa  furaha sana kwangu, baadaye walikuja wale wasichana wengine  wakachukua mabegi yao wakaondoka. 

Nilitamani sana nisiondoke kwa namna ambavyo Shonaa  alivyonitendea wema ila sikuwa na jinsi! Nililala Usingizi wa  Mang’amg’am kisha naangalia saa yangu 

Saa 10 Alfajiri nilimuamsha Shonaa, tulijiandaa ili  anisindikize Ubungo, maana wakati huo Stendi ilikuwa Ubungo,  aliita Bajaji, tulianza safari ya kuelekea Ubungo, tukiwa  barabarani nilimwambia Shonaa 

“Moyo wangu unasita sana kuondoka”

“Usiwaze hivyo Jojo, ilikuwa ni hamu yako kurudi nyumbani,  unapaswa kufanya hivyo” 

“Sawa” Nilimjibu, ilituchukua dakika 45 kutoka tulipokuwa  tunaishi hadi Ubungo, Alfajiri hiyo iliambatana na baridi  kali na giza kiasi 

Shonaa alimlipa pesa yule dereva baada ya kuwa tumeshafika  Stendi, aliniacha nikiwa nimekaa sehemu akaenda kukata tiketi  kisha akarudi, tuliongozana hadi ndani kwa ajili ya kupanda  Basi, nilikuwa namtazama sana Shonaa maana sikuamini kama  nilikuwa namuacha na kurudi kwetu Tabora. 

Alinisaidia kuingiza begi kwenye Buti kisha aliniaga huku  chozi likimtiririka 

“Kwaheri Jojo, sijui kwanini nalia, sijui kwanini naumia  kuachana na wewe hapa” Alinikumbatia kwa uchungu, hadi chozi  lilianza kunitoka 

“Nitarudi siku moja nikiwa tayari Shonaa, naumia pia kuachana  na wewe hapa” Nilisema kisha tulisikia Honi ya Basi ikipiga 

“Nenda Jojo” Basi niliachana na Shonaa kwa maumivu na  masononeko makubwa, nilipanda kwenye Basi, nilimuona Shonaa  akitokomea zake getini. Nilitamani sana nisiachane na Shonaa  lakini haikuwa na jinsi, muda wa Basi kuondoka ulikuwa  ukikaribia. 

Niliishika rozali yangu na kuibusu, nilianza kuwaza jinsi  ambavyo nitafika Tabora, niliona kama nimefunguliwa kutoka  Utumwani maana aina ya Maisha ambayo niliyakuta siyo  niliyoyategemea japo mwisho wake ulikuwa mzuri na wenye  kumbukumbu isiyo sahaulika. 

Pembeni yangu alikuwepo mdada mmoja ambaye alikuwa na Mtoto  Mchanga, nilianza kuhisi kubanwa na haja ndogo ilinibidi  nimuulize yule Mdada kama anaijuwa ilipo choo, bahati nzuri  alikuwa anayafahamu mazingira ya Pale Ubungo, alinielekeza  mahali ambapo ningejisaidia haja ndogo ambayo niliona  ingenipa kero kwenye safari yangu, Nilisahau pochi yangu  yenye pesa na simu ndani ya Basi, nilikuja kukumbuka nikiwa  nimeshashuka, nilipotaka kurudi kuchukua niliona nitachelewa  maana gari ilikuwa ikianza kushtua taatibu kama ishara kuwa  inataka kuondoka, kwasabahu yule Mdada aliniambia ni hapo  tuuu hivyo nilijipa tumaini la kuwahi kurudi. 

Nilikimbia kuelekea huko, nilikuta Watu wengine wakiwa  wanasubiria zamu ya kuingia Chooni, basi nilisubiria hadi Watu watano walipomalizika kisha niliingia Mimi. Nikiwa  najisaidia nilianza kusikia honi za gari kwa fujo sana alafu  kama gari zilikuwa zikiondoka, hata kujisuuza sikuwahi,  nilivaa nguo haraka sana. 

Nilipotoka nilimsikia Mtunza Choo akisema 

“Wahi gari zinaondoka” Ujuwe nilichanganikiwa sana, kibaya  zaidi sikukumbuka jina la gari ila nilikumbuka liliposimama  tu lakini hata hivyo nilipofika nilikuta gari zikiwa  zinagombea kuondoka na zingine zikiwa zimeshaanza kuondoka,  kiufupi kulikuwa na purukushani hata ile gari haikuwepo pale,  nilihisi kufa. 

Nilihamgaika sana na kama unavyojuwa Ubungo kunavyokuwa na  purukushani, nilikuwa mgeni hata sijui niingilie wapi nitokee  wapi, nililitafuta lile gari, nililiona gari lililofanana na  lile nililikimbilia haraka nikalisimamisha, nikaulizwa naenda  wapi? 

“Naenda Tabaro nilienda kujisaidia” nilijibu nikiwa nimeweka  mguu mmoja kwenye gari 

“Hii siyo ya Tabora, hii ni ya Morogoro. Za Tabora  zimeshaanza kuondoka jitahidi ukawahi getini” Alisema Yule  Mbaba mweusi, mnene mwenye kutambi. 

Basi nilishuka nikaulizia lilipo geti la kutokea Mabasi,  nilielekezwa. Kibaya zaidi ni kuwa sikuwa na kumbukumbu jina  la Basi linaitwaje maana tiketi alienda kukata Shonaa alafu  hata sikuisoma kutokana na furaha niliyokuwa nayo. Nilishika  kichwa nikahisi kinawaka moto, dhahiri niliona safari ya  kurudi Tabora ikiwa inafia hapo, nilianza kulia, Mlinzi  aliniuliza 

“Unalia nini?” 

“Nimeachwa na Basi langu” Nilisema nikiwa ninalia tena kwa  kwikwi 

“Nenda kwenye kampuni ya Basi uwaeleze, mabegi yapo humo?” 

“Kila kitu kipo mle hadi simu na pesa, nisaidie Kaka yangu”  Nilisema 

“Sina cha kukusaidia ndugu yangu, mnaanzaga hivyo hivyo alafu  mtuingize Mkenge, tafuta Maboya wengine” Alisema Mlinzi kisha  aliachana na mimi kabisa, nilijaribu kumuomba anisaidie  lakini ilishindikana tena alinitishia angenipiga.

Basi niliendelea kuhangaika kutafuta lile basi bila mafanikio  yoyote yale, hadi jua linachomoza kulikuwa na Mabasi machache  sana ambayo yalikuwa hayana safari kwa wakati huo. Nilitafuta  mahali pa kukaa maana niliomba sana msaada bila mafanikio yoyote, niliketi juu ya jiwe moja lililopo pembezoni mwa  barabara iliyokuwa ikielekea getini, palikuwa na Miti kadhaa  iliyojipanga, Basi niliketi hapo. 

Sikujuwa hata mtandio wangu niliudondoshea wapi, nilikuwa  kama Chizi maana wakati nalia nilitimua sana nywele zangu.  Nilikaa hapo kama Bubu, niliwaza sana hadi kichwa kiliacha  kufikiria tena, Sikujuwa niende wapi maana Sikuwa na namba ya  Mtu yeyote yule Kichwani, sikuwa na kumbukumbu ilipo Ile  kumbi ya Sterehe maana nilienda mara moja tu, kingine sikuwa  na kumbukumbu pale nilipokuwa naishi na Shonaa palikuwa  panaitwaje maana napo nilikaa kwa siku mbili tu, nilikuwa  Mgeni Dar, Nilimkumbuka sana Shonaa hadi Chozi likawa  linanidondoka tu. 

Nini Kitaendelea

Usikose SEHEMU YA TANO ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

 Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx

10 Comments

  1. Jojo umezid ushamba unaachaje pesa kweny gar😠😠
    Apo usimsingizie mungu huo ni uzembe😡😡
    Any way admin upo vzr ahsante Kwa hadith

Leave A Reply


Exit mobile version