Monk Adrian mzaliwa wa California nchini Marekani, huyu amejikita zaidi kwenye mambo yahusuyo utangazaji ikiwemo Televisheni ingawa si mwandishi kamili. Monk aliandika kijitabu chake mwaka 2008 akituuliza ‘CAN YOU TRUST THE MEDIA?” Sina hakika kama walimjibu.
Achana na Monk ambaye labda yeye haamini katika tasnia ya habari. Ghafla nimelikumbuka swali ambalo wazungu huwa wanajiuliza katika soka “DO YOU BELIEVE BIG PLAYERS TO BE TOGETHER?” Kwa Kiswahili cha kawaida kabisa ni kwamba una waamini wachezaji wakubwa kuwa pamoja?. Ni swali.
Hata mimi pia nimejiuliza baada ya kuona picha za kufurahisha kwa mashabiki wa Yanga na za kutisha kwa mashabiki wa timu pinzani. Kiufupi niwataje tu mashabiki wa Simba.
Picha hizo zikiwaonesha wachezaji ambao wamekonga na wanakonga na kukongoa nyoyo za mashabiki wa mpira nchini. Ni hizo uzionazo juu hapo.
Lipo wazi Aziz Ki ni mchezaji bora sana ni hivyo hivyo tu kwa Pacome. Chama mara nyingi anatajwa ni mchezaji bora zaidi kuliko hata wachezaji wanaoonekana bora. ‘The brain’ Akiwa na mpira mguuni majibu unayapata mwenyewe. Na wote hao ni wafalme katika soka la Kibongo.
Chama alikuwa anaiamua Simba ifanye kitu gani na alipewa kila uhuru kwenye eneo la mwisho la Simba. Aziz Ki pia ana ufalme wake Jangwani na hasa ukichagiza msimu huu ameibuka mfungaji bora wa ligi. Alichokifanya Pacome kila mtu ni shahidi, na yeye pia ni mfalme. Hapo sijamtaja Max Nzengeli.
Katika dunia ya soka Pacome, Aziz na Chama wote ni kama wanafanana ingawa wanaweza pia kucheza namba tofauti, wawili wakatokea pembeni na mmoja katikati. Swali ni je kila mtu ataonyesha ubora wake akiwa katika eneo ambalo labda hakulizoea? Kwa mfano Aziz Ki akimpisha Chama katikati je yeye atakuwa bora kama ambavyo tunamjua?
Tuliwahi kuona wakati ule Aziz Ki na Feisal walipokuwa wote Jangwani. Kuna muda ilibidi Nabi amweke Aziz nje ili Fei awe karibu zaidi na lango, na hapo tuliuona ubora wote wa Feisal. Lakini nyakati ambazo Ki na Fei walianza pamoja Fei alishuka chini kabisa na ubora ulipungua.
Gamondi atakuwa tayari kuupata ubora wa Chama na kumpoteza Aziz Ki au Pacome? Ubora ambao Chama anaimbwa nao kwa sasa ulionekana akitokea katikati licha ya mara chache alitokea pembeni na hapo tumeona mashabiki wa Simba wakilalamika kwanini Chama atokee pembeni?
Achana na ubora wa mtu wote hao watatu hakuna mchezaji anayepaswa kuanzia nje. Wote wakianza nani atakuwa mtu wa mwisho kwenye kuamua majukumu muhimu?. Nani atapiga mipira iliyokufa?. Nani atapiga penati? Wote ni wazuri katika maeneo hayo? Sasa hawatagombania kupiga ili kila mtu ajenge ufalme wake?
Tuliwahi kuona mara kadhaa ndani ya klabu ya PSG wakati ule Cavani na Neymar wakicheza pamoja, walikuwa wakinyang’anyana mipira kila mtu akijiona bora kuliko mwenzie.
Achana pia na kila mtu kutaka kujiona bora je wakicheza pamoja timu italeta uwiano ule unaotakikana? Tuliiona hapa PSG ya Messi, Neymar na Mbappe, ilikuwa timu ya kawaida sana iliyojaza mastaa. Au PSG ya Cavani, Zlatan Ibrahimovic, Pastore na mastaa wengine haikuwa timu bali ni wachezaji bora tu waliogoma kuonesha ubora wao.
Kwa wale wakongwe wenzangu tuliishuhudia pia Uingereza ya Michael Owen, Wayne Rooney, Paul Scholes, Steven Gerlard, Frank Lampard, Rio Ferdinand na John Terry ambayo ilijaza mastaa karibu wote lakini haikufuzu hata hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro au kombe la dunia, achilia mbali kucheza fainali na kutwaa taji lenyewe.
Tusubiri na kuona kama Chama, Pacome na Aziz Ki watakuwa kitu kimoja kuifanya Yanga matata au watakuwa ni mastaa waliojazana kila mtu kutaka kujiona bora kuliko mwenzie.
Kama watakuwa kitu kimoja basi nina hakika Yanga itakuwa timu tishio barani Afrika na naiona kabisa wakicheza fainali ya klabu bingwa mwakani. Ikiwa sivyo Yanga itakuwa ni timu inayotisha kwenye makaratasi kwa majina na si uwanjani.
SOMA ZAIDI: Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?
11 Comments
Kuna nmn napata ukakasi na Admin we ni SSC…mbn Madrid ya Figo ilikuwa ni mastaaa wakina Roberto Carlos zizzou jmn
Ilifika wapi champions?
Kwa kwel sijawahi kuona timu iwe na mastaa alafu ikafanikiwa nafikil tunaishi na picha kichwan lakn hatujui kipi kitatokea
Mbona tim zenye mafanikio zina wachezaj wakubwa wenye majina na still wakiingia kwa pitch wako na performance kubwa kwa hyo hapo kwa yanga huyo chama akileta mambo ya ajabu atawekwa kwa reserve coz pacome na aziz ni kawaida kucheza pamoja
Acheni kukalili kwa PSG Ebu angalieni hata Real Madrid walkua na BBC (Bale, Benzema na Cristiano) lakini c kila mtu aliuona moto wale, pia saiv kuna vinicius, rodrigo, jude na mbape amejiunga pia. Hapo ni falsafa ya kocha na utayari wa wachezaji kuclick kwenye namba mpya kwa wakati, tumieni mifano ya kutosha tuwaelewe asee sio mfano wa PSG tuu🙄🙄🙄
Upo sahihi kiasi chake lakini utofauti ni kwamba Chama anakuja kuongeza viungo tu kwenye mboga ambayo imeshapokea, Yanga sio mpya ni timu ile ile ya msimu uliopita awa wanaokuja ni kuongeza nguvu tu, ingekuwa wote ni wapya hapo shida ingekuwepo.Pia uwa natamani wachambuzi wa bongo mchambue mpira alafu mkimaliza maoni yenu mseme tuheshimu taaluma ya makocha wenye izo timu,kuna muda unamsikiliza mchambuzi mpaka unasema mbona kama anaona kocha wa timu husika ajui lolote,Umesahau kutaja Madrid ya Ozil,De Maria,Ronaldo, Benzema,Kroos,Modric.
Moja wapo ya kuwatumia ni hii na hii sms itunze,kuna siku Naby atapanga hivi, Diarra, Job, Bacca, Yao na Shadrack, mbele yao Aucho na Muda au Nzengeli, mbele yao Pacome, Chama na Ki Aziz,alafu Dube anamaliza.Kikosi kingine ongeza wewe iyo timu yangu wasioweza kukaba ni chama na Aziz tu,Pia mpira wa siku izi mtu unacheza kwa maelekezo, majukumu na nafasi uliyopangiwa na kocha,ivyo punguzeni presha tuwaache makocha wafanye kazi.
Kama unaki2 vileee 🤔🤔🤔🤔
Ok ao wataonekana awajaagizwa NBC wameagiza kombe la mabingwa Sasa nyie endeleeni kuongea sisi tunaendelea kuiesimisha inch hahahah😜
Pingback: Barua Kwenu PAMBA JIJI FC Kuelekea Ligi Kuu 2024/2025
Naona mmeisahau Barca ya mess Neymar na suares and iniesta au bas wale hawakuwa mastaaa 🤣