Ukiambiwa utaje orodha ya mabondia wanaopatikana nchini Tanzania huwezi acha kutaja jina la Hassan Mwakinyo ambeye ni miongoni mwa wale mabondia ambao wanaipeperusha bendera ya Tanzania katika anga la kimataifa katika mchezo wa ngumi.

Wakati mwingine unaweza kuta kauli ambazo kama sio mpenzi au mtu unayefuatilia mchezo wa ndondi ukadhani anakosea lakini katika namna nyingine ndio maisha halisi ya ngumi yaliyo na ndio njia nzuri zaidi ya kuendelea kuufanyia matangazo mchezo huu.

Mwakinyo ananikumbusha kuhusu kauli yake aliyoitoa akisema kuwa kukiandaliwa pambano lake lenye kiingilio cha Tsh Milioni 1 za kitanzania na kukiwa na pambano la Mayweather kwa kiingilio cha buku basi yeye atajaza ukumbi kuliko Mayweather utajiuliza kivipi? Lakini yeye mwenyewe anasema sababu kubwa ni kuwa anapendwa sana na mashabiki.

Wapo ambao wanatamani sana Mwakinyo akutane na Twaha Kiduku wapigane ili wajue nani mkubwa kwa Tanzania japokua danadana zimekua nyingi ila tukumbuke tu wawili hawa kupigana bado sana kwani kushindwa kwa mmoja maana ake ni kumshusha hadhi yake aliyonayo katika jamii ni sawa na mategemeo ya kolabo kati ya Diamond na Alikiba.

Ngumi, kama mchezo wa mapigano, umekuwa na historia ya kusheheni maneno ya majivuno kutoka kwa mabondia. Maneno haya yanakua yanaonesha namna ya kujiamini na kujionyesha yamekuwa sehemu ya utamaduni wa mchezo huu.Tukumbuke tu maisha anayoishi Mwakinyo haswa kwa kauli zake mara nyingine hutumiwa kwa lengo la kuvutia mashabiki na kuwapa burudani. Uzalendo na kujiamini kwenye mazungumzo ya mabondia huongeza msisimko kwa mashabiki, na hivyo kuleta shauku kubwa kwenye michezo. Hii inaweza kusaidia kuvutia wafuasi wapya kwa mchezo wa ngumi nchini Tanzania.

Wakati mwingine tusingemfahamu bondia Karim Mandonga bila ya kauli zake zilizompa jina na maisha kwa ujumla kwani kupitia maneno ya majivuno ambayo ameyatoa ndo maisha hayohayo ya Mwakinyo ambayo huongeza umaarufu wa mabondia na mchezo wa ngumi kwa ujumla. Wanapojieleza vizuri, wanaweza kuvutia mikataba ya udhamini na kuvutia vyombo vya habari. Umaarufu huu unaweza kusaidia kuwavutia wadhamini na kuongeza thamani ya mchezo wa ngumi nchini, hivyo kusaidia katika maendeleo ya uwanja huu wa michezo.

Tufahamu kuwa kupitia majivuno ya mabondia yana jukumu kubwa katika kuikuza ngumi nchini Tanzania. Huku wakichangia kuvuta mashabiki, kuongeza hamasa, kuimarisha umaarufu wa mabondia, na kujenga ushindani, maneno haya yana athari kubwa kwenye michezo. Lakini ni muhimu kwa mabondia kujua jinsi ya kutumia maneno yao vizuri na kwa busara ili kuchangia chanya katika maendeleo ya mchezo wa ngumi nchini na kuwapa fursa zaidi za kujitokeza kimataifa.

SOMA ZAIDI: Messi Ni Monalisa Wa Mpira Wa Miguu Duniani

Leave A Reply


Exit mobile version