Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) imekuwa jukwaa la kuonesha vipaji vya wachezaji wa soka kutoka bara la Afrika. Katika toleo la hivi karibuni la AFCON, Senegal imeonyesha uwezo wake wa kipekee, na kuvutia macho ya wapenzi wa soka duniani kote.
Ukitazama katika mitandao ya kijamii baada ya mchezo wa Senegal dhidi ya Cameroon ambao Simba wa Teranga wamewafunga Simba wasiofungika mabao 3:1 huku golini akiwa golikipa wa klabu ya Man Utd kutoka katika ligi kuu ya Uingereza anayejadiliwa sana ni golikipa Andre Onana.Kuna wakati unajiuliza kwanini sasa wakati aina ya magoli ambayo amefungwa ni uzembe wa mabeki wake
André Onana amekuwa nguzo muhimu katika ushindi na mafanikio ya Timu ya Taifa Cameroon katika baadhi ya mechi ingawa mchezo dhidi ya Senegal ni mchezo wake wa kwanza katika michuano ya AFCON mwaka huu. Akiwa kama golikipa, ameonesha ustadi wake wa hali ya juu katika kuokoa michomo hatari, kutoa mabao na kuwa kiongozi langoni lakini pia kupangwa kwake kuanza leo ni pamoja na uzoefu wake katika ligi za Ulaya, hasa akiwa na Man Utd, umemfanya awe mchezaji wa kuaminika na mwenye uzoefu.
Hata hivyo, kuna wakati ambapo Onana amekutana na changamoto na kushutumiwa kwa baadhi ya makosa yake langoni. Hii ni sehemu ya mchezo wa soka, na hata wachezaji bora wanaweza kukutana na nyakati ngumu. Ni muhimu kuelewa kwamba sio Onana pekee anayepaswa kulaumiwa wakati mambo yanapokwenda vibaya.
Ukiitazama nchi ya Senegal ambao ni mabingwa watetezi ina timu imara yenye vipaji vingi katika kila idara. Washambuliaji kama Sadio Mané, na mabeki imara kama Koulibaly wameifanya Senegal kuwa mojawapo ya timu bora katika bara la Afrika. Hivyo basi, ni muhimu kuelewa kuwa matokeo mabaya hayawezi kumlazimu lawama Onana pekee.