Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally leo akizungumza na Mashabiki kuelekeza mchezo wao dhidi ya Asec Mimomas hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Akizungumza na Matawi kama hamasa kwa mashabiki kukata tiketi na kuhudhuria mchezo huo kwa wingi siku ya Jumamosi, Uwanja wa Benjamini Mkapata

Wanasimba amshaamsha kuelekea Jumamosi tutainza leo pale Vingunguti kuanzia saa 4 asubuhi. Njoo tufurahi na tukate tiketi

Jumamosi mapema Wanasimba tunakutana uwanjani kushangilia timu yetu. Kamata tiketi yako sasa. Tarehe 25 ni tarehe ya kila Mwanasimba kwenda uwanjani.”

Timu iko vizuri kwenda kushinda mchezo wa Jumamosi. Hakuna timu yoyote ambayo inaweza kutusumbua kwenye Uwanja wa Mkapa. Tumedhamiria kushinda na hatuwezi kufanya hivyo bila shabiki bora kuwepo uwanjani.

Sisi tuna uchungu na timu yetu na ili kuonyesha kweli tunauchungu lazima tuisaidie timu kushinda Jumamosi. Wabaya wetu wanawekeza nguvu kubwa kutukejeli ili tupoteze mwelekeo na mchezi wa Jumamosi lakini Simba tumeshakuwa wakomavu, tutahakikisha tunapata ushindi mbele ya Asec Mimosas.”

Wachezaji wameshatuahidi kwenda kuipambania timu yetu. Kilichobaki ni sisi mashabiki kwenda uwanjani, tumeshaujaza mara nyingi uwanja na Jumamosi tunataka hivyo.”- Ahmed Ally.

Lengo kubwa la hamasa hii kuhakikisha mashabiki wote wa Simba SC wanajitokeza kwa wingi kukata tiketi za mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya mabingwa Afrika pamoja na kujitokeza uwanjani

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version