IlipoishiaPopo walianza kuruka ruka walipokua wanazidi kwenda mbele ndani ya Pango hilo lenye ukubwa wa kutosha, walifika mahali Zandawe alisimama kisha yule sokwe akasugua kucha zake kwenye jiwe, ukatoka moto akaweka kwenye kifaa kilichopo kwenye jiwe, Naam! Hapo palikua na tambi iliyoshika moto haraka na kufanya pango liwe na mwanga, Benjamin alishtuka alipowaona Popo wakubwa mfano wa Bata Mzinga wakiwa wametulizana

“Usiogope” alisema Zandawe, haikua rahisi kwa Benjamin lakini alihitaji ujasiri wa ziada ili kusonga mbele zaidi, Benjamin alizituliza pumzi zake na mapigo yake ya moyo yaliyokua yakienda ‘Songombingo’

Waliendelea mbele kwa zaidi ya hatua ishirini huku yule Sokwe akiwa ameshikilia ule utambi unaowapa Mwanga.  Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA TISA

Kitu kilichomshangaza Benjamin ni ukubwa wa eneo walilosimama kwa sasa, palikua na mwanga wa kutosha uliotokana na taa tofauti na ile tambi iliyotoa mwanga mdogo.

Palikua na miili iliyoning’inizwa ikiwa na kombati za jeshi, Benjamin alizidi kuogopa kwa matukio aliyoyaona hapo ndani ya Pango na Msitu mzima, Zandawe alimgeukia Benjamin na kumuuliza

“Inatosha kwako kuniamini?” Benjamin alikaza macho yake na kumeza funda zito la mate, akatikisa kichwa chake kumwitikia Malkia Zandawe

“Ndi…oo” alimjibu Zandawe, ilihitaji Ujasiri wa ziada kwa Benjamin kujikaza na hali ile, Zandawe akamwambia Benjamin

“Huu msitu ni mali yangu, hakuna anayeweza kuingia hapa bila ruksa yangu, wote waliojaribu yaliwakuta haya unayoyaona Benjamin, hawa ni jeshi wa Tanzania, wengine ni Wanajeshi kutoka nje, wengine ni wachunguzi waliokuja kuuchunguza Msitu huu lakini wote waliangukia pua, unafikiri nimewezaje kufanikisha yote? Kwasababu nina jeshi la ndege linalonisaidia katika vita.” Alisema kwa uchungu sana huku chozi likimtoka, hata Benjamin

alishangaa kwanini Malikia Zandawe alikua akilia

“Hawa watu waliuwa Wazazi wangu kwenye Msitu huu, walinifanya kua Yatima” alisema Zandawe kisha alitoa ishara ya kidole akiwa ameunyooshea mwili mmoja ulio juu ya Mnyororo wenye sare za Kijeshi

“Nachukia hili vazi, ndiyo sababu nilikusaidia Benjamin, ndiyo sababu nilikuhifadhi.

Ungekua askari ningekua nimeshakuuwa palepale Bwawani, sikutaka kufanya hivyo” alisema Zandawe, alikua akibubujikwa na mchozi, Sokwe Yubo naye alikua akitokwa na mchozi, akasogea na kunfuta chozi Zandawe

Ndani ya pango hilo palikua na silaha za kutosha ambazo alizinasa kutoka kwa Wanajeshi waliojaribu kuingia Msitu wa Magoroto, alikua na silaha za kila aina.

Kisiwani Mbudya, Usiku huo huo.

Kisiwa cha Mbudya kilipokea bugudha ya sauti kali ya chopa, sauti ya Chopa ambayo Bi. Sandra alikuwemo ili kuitika wito wa Waziri Mkuu wa Tanzania Bwana Haji Babi, katika kisiwa hicho palikua na nyumba moja ya mapumziko, ndimo alimokuwemo Waziri Haji Babi, Bi. Sandra aliuwona ulinzi wa kutosha uliokizunguka Kisiwa hicho cha Kitalii.

Haraka alielekea moja kwa moja ndani ya Kijumba hicho chenye hadhi kubwa ya Mapumziko ya Viongozi wa Nchi, alishtuka alipokutana na sura tatu alizozifahamu, sura ya kwanza ilikua ya Waziri wa mambo ya Ndani Ignas Zakaria na sura ya pili ni ya Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia bwana Juma Nguvu Mbili na sura ya tatu ambayo ilibaki kidogo apepesuke kwa mshituko ilikua ni ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Hawa wote ni watu wa karibu zaidi na Rais Lucas Mbelwa, alijiuliza kwanini walikusanyika hapo Mbudya

na Waziri Mkuu Haji Babi.

Waziri Mkuu akasimama baada ya Bi. Sandra kuingia kisha wote walisimama. Hii ikampa ishara ya haraka Bi. Sandra kuwa Wote walikua chini ya Waziri Mkuu.

“Karibu Sandra” alisema Waziri Mkuu, alivuta kiti ili Bosi wa Usalama wa Taifa akae, yeye ndiye aliyekua akisubiriwa, aliangaza huku na kule, aliyatupa macho yake kwa Wanaume hao wanne walio ndani ya Chumba kimoja.

“Najua unashangaa kwanini nimekuita hapa, pengine unashangaa hata kwanini umekutana na hawa Watu, au unashangaa kwanini nipo Kisiwani Usiku huu?” alisema waziri Mkuu, naye alivuta kiti na kutulia kando ya Bi. Sandra aliye kimya huku maswali mengi yakiwa yanazunguka kichwani pake.

“Nimekuita kwasababu ya Mpango maalum, kwasababu ya manufaa yetu kwa pamoja” alisema Waziri Mkuu kisha alitabasamu huku taa ikiwa inampiga upande mmoja wa sura yake

“Unamaanisha nini kusema mpango Maalum?” alihoji Bi. Sandra, ukimtazama mara moja tu unagundua ni Mtu makini kwa kiasi gani, kisha aliibana miguu yake vyema.

“Faili la M21 lililoibiwa kutoka hazina ya siri ya Rais Mbelwa, ina siri zako pia, siri za Mauwaji uliyoyafanya Kagera dhidi ya Mgombea Ubunge, haitoshi, namna ulivyo mwaga damu za Watu wasio na hatia kule Butiama wakati wa operesheni ya Kumsaka Jasusi Katumbo, mbaya zaidi ni ufisadi ulioufanya kwa kushirikiana na Rais Mbelwa pale Benki kuu ya Tanzania” Yalikua ni maneno yenye ncha kali yaliyomfanya Bi. Sandra azidi kutulia, pakiwa na ukimya Waziri Haji Babi alisimama na kumshika Bega

“Hawa wote ni miongoni mwa Watu walio ndani ya Faili M21, kuibiwa kwa faili kumetokana na uzembe wa Rais Mbelwa kama yule Ngoswe wa kwenye kitabu. Sisi tuna mpango wa kujisafisha sababu haiwezekani hadi sasa yule Msichana asipatikane” alisema Waziri Haji Babi, mara Bi. Sandra alisimama kutoka kitini kama Mzimu, akaisimamisha shingo yake na macho yake akayakaza vizuri kisha akatupa swali

“Una mpango gani?” Ukimya wa sekunde kadhaa ulikuja na jibu la kutisha na kushtua sana, Waziri akajibu

“Mpango wa kumuuwa Rais kwanza, kama aliweza kumsaidia Msichana kutaka kuitoroka Tanzania, hawezi kushindwa kumsaidia wakati huu, yule ni Rais dhahifu sana kutoka katika chama chetu, ni lazima Auawe Usiku huu, kisha Sisi tutaendesha operesheni ya kumnasa Elizabeth” alisema Waziri Haji Babi, macho ya Bi. Sandra yaliwatazama wote walio ndani ya chumba palikua na baadhi ya viongozi wakubwa wa Nchi, hakua na jibu zaidi ya kujikuna nywele zake

“Wewe ndiye utakaye ifanya hii kazi ya kummaliza Rais Mbelwa Usiku huu kabla hapajakucha” alisema Waziri Haji Babi. Bi. Sandra akainamisha kichwa chini akaipokea kazi ngumu ya Kummaliza Rais Mbelwa Mtu ambaye alikua akielewana naye kwa mambo mengi kwa muda mrefu.

Alisimama na kutoa Heshima kisha aliondoka akaelekea kwenye Chopa, kabla hajaingia ndani ya Chopa alipiga simu Makao makuu ya Usalana wa Taifa kwa vijana wake aliowaamini zaidi, kisha aliingia ndani ya Helkopta akaondoka zake.

RAIS LAZIMA AFE

Chozi lilimbubujika Bi. Sandra, alikumbuka nyakati nzuri alizokua nazo na Rais Mbelwa, alibakisha kilomita kadhaa kurejea Ikulu kutekeleza agizo la Waziri Mkuu ili kuendelea kuficha maovu yao.

Chopa yake iliranda randa juu ya Anga kwa nusu saa kisha ilishuka Ikulu, Rais Mbelwa alipomwona Bi. Sandra alitabasamu akiamini Elizabeth amedhibitiwa, alimkaribisha Ofisini kwa Mbwembwe sana, lakini sura ya Bi. Sandra ilimshangaza sana Rais Mbelwa, ikabidi amuulize

“Kuna tatizo, mbona umekuja na sura hiyo?” aliuliza, Bi. Sandra alimtazama Rais, kazi iliyo mbele yake ilikua ni kumuuwa Rais Mbelwa hapo Ikulu usiku huo kama alivyopewa kazi hiyo na Waziri Mkuu. Ilikua inamuumiza Bi. Sandra sababu Rais alikua rafiki yake lakini alitakiwa kumuuwa kwa manufaa yake, akamwambia Rais kwa sauti dhaifu iliyotoka taratibu

“Ndiyo kuna tatizo”

“Tatizo gani, ulisema unahitaji makomandoo kutoka Black Site, sasa ni kitu gani kingine unataka ili kumnasa yule Mpuuzi?” aling’aka Rais Mbelwa, hakujua kua Mshale wa Maisha yake ulikua umefika mwisho.

“Uhai wako Rais” alisema, hapo hapo Rais Mbelwa alibadilika sura, akakunja ndita zake kana kwamba alikua hajamsikia vyema Bi. Sandra, alimjua vizuri Mama huyo kua ni Muuwaji mzuri sana

“Rudia ulichosema”

“Nimekuja kuchukua Maisha yako Rais, samahani sana haikupaswa kuishia hivi Bosi wangu” alisema kisha alimpa heshima Rais kwa kuinamisha kichwa chake. Haraka Rais alichomoa Bastola kutoka katika droo ya Meza, akamnyooshea Bi. Sandra

“Unafanya kazi na Nani?” aliuliza Rais huku akiwa ameshabinyiza kengele ya hatari ndani ya Ikulu kuita walinzi wake, mara moja walifika hapo zaidi ya walinzi kumi na moja wenye silaha kali. Moja kwa moja walinzi walimweka Bi. Sandra chini ya Ulinzi

“Unafanya kazi na Nani?” aliuliza tena Rais Mbelwa, Bi. Sandra wala hakua na wasiwasi, alitabasamu tu kisha alimjibu Rais

“Hata nikikwambia Rais haitosaidia, udongo ndiyo makazi yako muda mchache ujao” alijibu kwa kujiamini sana Bi. Sandra

Haraka Bi. Sandra alizungukwa na Walinzi kila kona, licha ya kuzungukwa bado Rais Mbelwa alikua akiangalia huku na kule, alijua Bi. Sandra ni Mtu mwenye akili nyingi na maarifa ya kutosha, hakua na silaha yoyote aliyoingia nayo Ikulu, hata Walinzi walipomkagua walimkuta Mtupu

Mara ghafla Risasi zilianza kurindima, tayari maafisa Usalama walikua hapo kutekeleza maagizo ya Bosi wao Bi. Sandra, risasi za haraka zilizopigwa ziliwadondosha walinzi wote waliomzunguka Bi Sandra, Rais alipigwa risasi ya Mkono ulioshikilia Bastola

Akaanguka chini na kuanza kugugumia kwa maumivu makali, kisha Bi. Sandra akaikota Bastola ya Rais, Maafisa saba wenye uwezo mkubwa walikua hapo, walishamaliza walinzi wote ndani ya muda mfupi sana, wakafika hadi ofisini kwa Rais

“Kwanini unafanya hivi?” aliuliza Rais Mbelwa akiwa chini anatokwa na damu, Bi. Sandra alisogea na kumjibu

“Kwasababu wewe ndiyo kikwazo cha kupatikana kwa yule Msichana, unapaswa kupumzika Rais wangu” alisema kisha alimtandika risasi sita eneo la kifua, mbili akizipiga kichwani, jumla ya Risasi Nane zilitosha kuifanya Tanzania iwe haina Rais, akafia pale pale sakafuni, kisha akakikalia kiti cha Urais, roho na akili ya Bi. Sandra ikaanza kutamani madaraka.

Hapo hapo akapiga simu moja kule Mbudya kua ameshammaliza Rais Mbelwa, mwili wake ukavutwa hadi eneo la chini ambako alikua akitesa na Kuuwa Watu, huku ndiko alikomfungia Mke wake kama mateka. Sasa mpango ulio mbele ni kuhakikisha anapatikana Elizabeth, Nchi ikawa chini ya Waziri Mkuu ambaye baada ya Kifo cha Rais Mbelwa alielekea ikulu na kuanza kutoa Maagizo ya nini kifanyike.

Nini kitaendelea? Usikose sehemu ya 20 ya MSALA ndani ya SEASON 2 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

6 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version