Ilipoishia Muhonzi, kuna dili lakini ni dili la kifo, narudi Dar Mchana wa leo” alisema Elizabeth kwa kujiamini kabisa mara baada ya simu kupokelewa, kisha akaikata bila kusikiliza upande wa pili kwani  Aliiona harufu ya Utajiri.

Mishale ya saa tano ilimkuta akiwa anamaliza kuweka nguo zake ndani ya Begi lake kubwa lenye Matairi, akalikokota akiwa anafunga zipu ya begi, akalivusha mlangoni kisha kwa haraka akashuka kwa kutumia lifti kuelekea chini, kichwa chake kilikua kinawaza kitita cha pesa atakachovuna, alijiamini anaweza kufanya kazi hiyo kwa mafanikio

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA NNE

Akiwa ndani ya Tax tayari safari ya kuelekea Uwanja wa ndege imeanza alijikuta akipata mashaka juu ya safari yake hiyo, haikua rahisi kumwamini Mtu aliyezungumza naye tu kwa njia ya simu, kazi yake ya Ujasusi wa siri ilimtengenezea maadui wengi.

Akaiacha Mwanza akiwa ndani ya ndege, kitu cha kwanza kufanya ndani ya ndege ilikua ni kuandika kila alichofikiria kuhusu Mtu aliyezungumza naye muda mchache uliopita, kisha akayaruhusu Macho yake kuuangalia ubunifu wa Mungu namna alivyoiumba anga nzuri inayovutia Mawingu mazito yalikua yametanda mfano wa Barafu, tayari ndege ilikua imeshaliacha anga la Mwanza.

Iliwachukua takribani zaidi ya dakika sitini kuanza kuona mandhari nzuri ya kupendeza wakati ndege ilipokua ikishuka kutoka anga ya juu.

Hali ya ukijani ulioiva ilimfanya anene kwa sauti kuu

 “Mungu ameipendelea Tanzania” aliachia na tabasamu huku ndege ikizidi kushuka, sauti ya kuwataka wafunge mikanda yao iliposikika ilikua ni ishara kuwa ndege ilikua ikijiandaa kugusa Ardhi ya Jiji la Dar-es-salaam.

Elizabeth aliwasili Jijini Dar-es-salaam, eneo la maegesho palikua na gari iliyokua ikimsubiria, aliingia humo akakutana na Muhonzi.

Wote walikua vijana wenye kufanana umri, kisha safari ilianza kuelekea kwenye makazi yao “Umesema kuna kazi?” aliuliza Muhonzi akiwa anaipita kwa kasi scania moja iliyobeba vifaa vya Ujenzi maeneo ya Sido

“Tunatakiwa kufikiria zaidi kabla ya kuichukua hii kazi, ni kazi hatari sana Muhonzi, aliyetoa amedokeza kuwa ni kazi ya kuingia Ikulu na kuiba nyaraka za siri” alinena Elizabeth akiwa anaperuzi simu yake

“Oooh Mungu wangu, hivi anafikiria sisi hatuyataki Maisha yetu? Elizabeth hii kitu siyo rahisi kama anavyofikiria bwana”

“Ndiyo hivyo Mzee Baba, hofu yangu unaweza kua mtego. Kwanza nimekuja kuonana na Mtu aliyenipigia simu”

Safari yao ndefu iliyojaa mazungumzo iliishia kwenye nyumba moja huko Ilala. Walijadili kwa kina sana wakafikia makubaliano ya kumpigia simu mhusika aliyetoa kazi hiyo na simu ilipokelewa haraka sana ilionekana kuwa Mhusika alikua akiisubiria simu hiyo

“Tunaweza kuonana?” alihoji Elizabeth huku akimtazama Muhonzi aliyejawa na mchecheto

“Kesho saa 9 jioni tukutane Diamond Jubelee Upanga” akasema Mtu huyo kisha alikata simu.

“Oooh fuc**, unamwamini?” akahoji Muhonzi aliyevalia prova ya njano, pensi nyeusi na soksi ndefu, alikua akiranda randa

“Tunapaswa kumwamini, amesema atatoa kitita kikubwa cha pesa tunayoitaka”

“Kama ni mtego?”

“Hatuwezi kunasa kwenye mtego kirahisi, kwasasa wacha tumwamini”

**

Usiku kucha walikesha kwenye mtandao kutafuta taarifa za mpigaji wa simu, walijaribu kuidukua namba ya Mpigaji ili iwe rahisi kwao kumtambua Mtoaji kazi kabla ya kukutana naye, dakika ziliyoyoma, kazi nzito waliifanya wakiwa kwenye chumba maalum walichokitengeneza kwa ajili ya kazi hiyo lakini waliambulia patupu.

Mpigaji wa simu alikua Mtu msiri sana kwa kiingereza wanaitwa ‘Low Profile’

Kukosa taarifa za Mtu huyo kuliongeza chachu ya kupenyeza hisia zao kua huwenda Mtu huyo naye ni Jasusi mbobevu ndiyo maana alizificha sana taarifa zake na haikua rahisi kumdukua.

Waligida Kahawa wakiwa wanatazamana Usiku huo, mtazamano wao uliwafanya wasogeleane na kuanza kunyonyana ndimi zao taratibu huku wakitoa Miguno ya Hapa na pale Kasi yao iliongezeka huku wakiwa wanapapasana na kunyonyana ndimi zao, sekunde chache Muhonzi alikua tayari ameshaitoa pensi ya Elizabeth na kuanza kazi ya kikubwa. 

shughuli ya kivumbi na jasho ikawachukua zaidi ya dakika 15 kabla ya wote kuwa hoi huku akili zikiwakaa sawa na kuanza kumtafakari Mtu aliyewapa kazi ya kuiba faili Ikulu. Usingizi mnono uliwachukua pale pale

 

**

Siku iliyofwata waliamka na wazo moja tu, kuonana na Mtu aliyetoa kazi hiyo ya hatari, iliwapasa kusubiria hadi mishale ya mchana kisha walianza safari ya kuelekea Upanga

“Muhonzi niangalie” alisema Elizabeth,

Ni yeye ndiye aliyepaswa kuzama ndani ili kuonana na huyo Mtu, akaelekezwa sehemu ya siri ndani ya jengo hilo, alipoingia tu alijikuta akiyapeleka macho yake kwenye meza moja iliyo mbele yake, hapo alimwona Mtu mmoja

aliyevalia kofia nyeusi, aliificha sura yake haswa.

Namna alivyo ikampa uhakika Elizabeth kua ndiye anayepaswa kuzungumza naye, taratibu kwa mwendo wa Machale alisogea na kugonga meza. Yule Mtu aliyanyua uso wake, alikua ni Mwenyekiti wa chama cha Upinzani cha TUYTA 

“Keti hapo” alisema, taratibu Elizabeth aliketi hapo, alishaona dalili zote kuwa jambo hilo halikua utani, Mtu huyo alidhamiria kuzipata hizo nyaraka za siri, Wakati Elizabeth anaketi alisindikizwa na maneno kadhaa ya kumwondoa wasiwasi

“Kwanini unazihitaji?” aliuliza Elizabeth akiwa amemtolea macho mwenyeketi huyo wa TUYTA aitwaye Zagamba Edward, mara sauti kutoka nyuma ya Elizabeth ilisikika ikisema

“Kwasababu imetosha kwake na anahitaji kulipa kwa ubaya wake, mateso na dhulma, ubaya na ubabe, wizi na utawala uliojaa kadhia nyingi ambazo zimenifanya nitoke upande wake” ilikua ni sauti ya Mke wa Rais Mbelwa, Mke wa Rais aliketi huku akishuhudia mshangao mkubwa kwa Elizabeth

 

“Najua una maswali Mengi Binti, kwanini nimeichagua njia ya kumuasi Rais, kwasababu Mbelwa amekalia kiti cha Urais hali ya kuwa hatoshi, yeye ni Rais Mchafu aliyevuka mipaka.

Mtu anayeweza kumpa ujauzito mdogo wangu kisha akamuuwa, haitoshi ameigeuza Ikulu kuwa genge la Mauwaji ya watesi wake, Rais anayepanga njama mbaya dhidi ya Taifa hili, huyu hapaswi kukalia kiti cha Urais” alisema Mke wa Rais kisha alimshika Bega Elizabeth

“Madam tumeshafika” ilikua ni sauti iliyomzindua Elizabeth ķutoka katika fikra nzito ya namna alivyokutana na Mke wa Rais hadi kupanga njama za wizi ndani ya Ikulu. Mbele yake aliona Hoteli maalum ambayo Rais Mbelwa alihitaji Elizabeth akae hapo kisiri kwa siku mbili kabla ya kuondoka kuelekea mafichoni Uskochi kukwepa jicho la Usalama wa Taifa ambao walipanga kummaliza. 

Nini kitaendelea? Usikose sehemu ya 14 ya MSALA ndani ya SEASON 2 

Je, Benjamin anaokolewa au anakielekea kifo?

Hatma ya Mzee Kimaro na Elizabeth itakuaje?

AHSANTE!! Kwa kua nami katika season ya kwanza ya Riwaya ya MSALA.

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

 

10 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version