IlipoishiaAbee” kwa kisauti chake kama Wema Sepetu aliitikia Elizabeth, ukimwona unaweza fikiria ni Msichana dhaifu sana lakini alikua na wasifu mkubwa na wa kutisha, akiwa na miaka 21 tayari alikua amezunguka takribani mataifa sita ikiwemo Iraq, Uingereza na Jamhuri ya Ireland

Alihitimu mafunzo maalum ya Ujasusi, ujeshi na mapigano ya judo na kareti, wachache sana walimtambua Msichana huyo kama Misenari anayefanya kazi kama Jasusi wa kukodiwa. Mikono yake aliiweka kwa adabu mbele ya Rais Mbelwa huku dimpozi zake zikichanua vyema. 

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Rais alikuna kichwa chake

“Unatakiwa kuondoka Tanzania ndani ya siku mbili zijazo, tayari kila kitu kipo sawa kwa ajili yako. Utaenda mapumzikoni Uskochi” alisema kisha alivuta pumzi zilizoambatana na mafua kwa mbali, kisha akasugua pua yake

“Nitaenda nawe huko?”

“Hapana, utaishi huko hadi pale nitakapokwambia urudi Tanzania, nafanya hivi kwa ajili ya usalama wako” alisema Rais Mbelwa, Elizabeth hakutaka kuonekana kushangaa sana, alionesha tabasamu lililochanua vyema, meno yake mawili ya mbele marefu yakaonekana vyema.

Akapewa Paspoti na taarifa zingine muhimu

Akaitwa dereva ambaye atamchukua Elizabeth hadi makazi ya siri kabla ya kuanza safari ya kuelekea Uskochi, akapewa kadi maalum kwa ajili ya matumizi atakapokua Uskochi, Rais akamaliza kwa kumwambia

“Hii ni safari ya siri Bety, hakikisha unaishi kwa siri sana huko” alisema kisha Bety akachukuliwa na dereva kuelekea nje, akakutana na Mke wa Rais mlangoni, akampatia Bety Mkoba kisha akamwambia

“Nakutakia mafanikio” Elizabeth akatabasamu

“Asante” akasema kisha wakaondoka hapo wakiwa na gari ndogo nyeusi aina ya Toyota Crown, safari ya Elizabeth ilikua ya siri sana.

**

BLACK SITE, Siku husika.

“Mnanitesa, mtaniuwa, Mnanitesa sijui chochote” chozi jeusi lilishuka kutoka machoni, wingu zito lilitanda ndani ya Maisha yangu. Yalikua masaa machache yaliyojaa mateso makubwa sana, nililazimishwa kusema najua nini kuhusu M21

Mara mlango ulifumguliwa, nilitupiwa kipande cha gazeti kisha Mlango ulifungwa tena, wakati maumivu ya kidole yakizidi kukolea, nilitakiwa kujivuta kwa ajili ya kuchukua kipande cha gazeti nilichotupiwa, nilijivuta kwa shida hadi nilipokifikia

Nilikutana na habari mbaya iliyonifanya nipepese macho yangu, Mtoto wangu wa kiume anayeitwa Nathan alikua amepotea, gazeti hilo liliandika taarifa hiyo ya kupotea kwa Mtoto wangu, lilikua pigo kubwa sana kwangu zaidi hata ya kunaswa kwa mpenzi wangu Suzan.

 

Kidogo pumzi zilinibana kwa mshituko, walifanya makusudi ili kuzidi kunitisha, kwakua tayari walishamnasa Suzan sikuona kama ni ajabu kua watakua wamemnasa na Mtoto wangu wa miaka mitano aliyekua akiishi Kizuiani kwa Bibi yake

Roho iliniuma mara tatu zaidi ya maumivu ya kawaida, nililia kwa uchungu sana, niliteswa na kuteseka kwa jambo nisilolifahamu kabisa, nilitamani masaa yangerudi nyuma ili nisimpe msaada tena yule Msichana anayeitwa Elizabeth, huruma yangu ndiyo iliyonileta huku.

**

Mwambisi, dakika ishirini Baada ya Shambulio.

Kijiji kilifuka moshi, hakuna kilichoonekana zaidi ya moshi na Moto, miili mingi iliyofumuliwa na mabomu ilikua imetapakaa kila kona ya Kijiji, hapakua tena na sura ya Kijiji.

Palikua Kimya sana, kwa Mbali ikasikika sauti ikigonga masikio ya Elizabeth aliyefukiwa na mchanga, sauti hiyo iliambatana na fukua fukua. Sekunde chache Elizabeth aliibuka kama mzimu akihema kwa nguvu, macho yake yaliyopukutisha mchanga yalikutana na Mzee Kimaro aliyekua akimtazama

“Twende wanarudi” alisema Mzee Kimaro akiwa ameshikilia Bunduki Mkononi, Elizabeth mwenye wenge alijikuta akisimama kwa kupepesuka huku akipepesa macho yake, masikio yake yalikua yakipiga firimbi, Mzee Kimaro alimvuta wakaanza kusogea mlimani, muda huo magari ya Kijeshi yalikua yakifika hapo yakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulimzi na Usalama Konrad Zuberi

Taratibu akili ya Elizabeth ilianza kukaa sawa, akapata nguvu ya kumhimiza Mzee Kimaro afanye haraka wafike mlimani, dakika kumi ziliwatosha kufika Mlimani na kujificha huko, jua lilikua linaendelea kuwaka kwa fujo.

Magari ya jeshi yaliyojaza askari yaliingia Kijijini hapo yakisindikizwa na Chopa ya Kijeshi, Elizabeth akamvuta Mzee Kimaro wakaushusha mlima kwa upande wa pili, taratibu walianza kuitafuta Picha ya ndege, vikosi vya kijeshi vilizidi kumiminika.

Rais alituma kikosi cha siri kuhakikisha wanatafuta Masalia ya Elizabeth, kila kitu kilisambaratika lakini alihitaji uhakika zaidi kua ameshamuuwa Elizabeth. Tukio hili lilianza kutajwa kuwa ni Ugaidi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama alikua wa kwanza kulitamka hilo mbele ya vyombo vya Habari.

Hali ya tahadhari ikaimarishwa kila kona hasa barabara zinazoingia Dar-es-salaam yaani Barabara ya Bagamoyo na Morogoro, Elizabeth na Mzee Kimaro wakazidi kukata nyika ili wafike Picha ya ndege mahali ambapo aliamini msaada ungewafwata, haikua rahisi kumwacha Mzee Kimaro aliyejitolea kumsaidia Elizabeth, waliongozana 

“Koh! Koh! Koh!” ilikua ni sauti ya kiatu niliyoisikia nikiwa nimeketi sakafuni, ndani ya chumba chenye mwanga hafifu, mbu walikua wakining’ata. Black site ni eneo nyeti ambalo hata sikujua ilikua ni saa ngapi, sikuona mwanga kutoka nje zaidi ya taa zilizokua zinawashwa mle ndani.

Mafua yalianza kuninyemelea, masikio yangu yalipokubaliana na Ubongo wangu kua sauti hiyo ilikua ikija kwenye chumba nilichopo, nilinyanyuka haraka na kusimama. Hisia zangu ziliniambia ukweli, mara sauti ya kufunguliwa kwa geti la chumba ilisikika, hapo nikaiyona sura ya yule Msichana anayenihoji mara kwa mara, ni yeye pekee ambaye alikua akinionesha sura yake wakati wengine walikua wakizificha sura zao.

Nilimeza funda zito la mate lililojaa haraka na shahuku ya kutaka kuongea, mara alinitupia karatasi mbili za Kaki zilizoanguka chini kando ya Mguu wangu wenye damu iliyoganda, niliruhusu macho yangu kutazama chini huku mkononi nikiwa na kipande cha gazeti.

Nilipepesa macho yangu nikiwa natazama, karatasi hizo zilizoambatana na picha mbili, nilitumia sekunde kadhaa za ukimya nikijaribu kuzielewa picha zile, yule Msichana alisimama akinitazama, niligundua zilikua ni picha zilizopigwa eneo lenye kufuka moshi, sikujua ni wapi

“Kwanini umenitupia hizi picha?” nilimuuliza, yule Mwanamke aliufunga mlango wa chumba changu, sikua na wasiwasi kua hatukua wawili pale sababu palikua na kamera juu ya ukuta hivyo palikua na wengine wanaotuona na kutusikiliza

“Unayemtetea na kumlinda ameangamiza Kijiji cha Mwambisi dakika kadhaa zilizopita, ameuwa Wanakijiji wote na kutokomea. Uko tayari kuingizwa kwenye kesi ya Ugaidi?” aliniuliza yule Mwanamke, ilinilazimu kuzirejea zile picha, kisha niliinua kichwa changu na kumkunjia ndita iliyojaa mshangao wa aina yake

“Yule Msichana?” nilimuuliza

 

“Ni Elizabeth Mlacha, unafahamu nini kuhusu yeye? Benjamin, Imetoka amri ya kuuawa kwako baada ya haya mahojiano” alisema yule Mwanamke aliyevalia suruali ya kitambaa na shati jeupe, kichwani alikua na Rasta za kuunga. Moyo wangu ulizima, hofu iliutapakaa mwili wangu kutoka kila kona, pumzi zangu zilijaa ubaridi wa hali ya juu.

Niliwaza kuhusu kifo, niliwaza kuhusu Mtoto wangu na wengine ninaowaacha nyuma yangu, hakuna atakayeipata maiti yangu na kuizika, nitafutwa na hapatakua na kumbukumbu zangu, hilo lilinimalizia dakika moja iliyonitoa jasho jingi

“Najua kitu kuhusu yeye” nilijikuta nikiropoka, sikutaka kufa mikononi mwa wale askari, sikutaka kuuawa ndani ya lile jumba nisilolifahamu, akili yangu ilinituma kusema Uwongo ili niununue muda wa kuendelea kuishi, nililiona tabasamu mbele ya macho ya yule Mwanamke

“Benjamini, niambie unajua nini kuhusu yeye?” aliniuliza, nilifuta jasho, nilishakata tamaa, kama tayari ilikua imetolewa amri ya kuuawa kwangu basi isingelikua rahisi nikaendelea kuishi. Nilikaa kimya bila kumpa jibu lolote huku nikifiria nimweleze nini wakati nilikua sijui chochote kile, ukimya wangu ulimfanya apenyeze swali jingine

“M21 iko wapi?” swali tata lilipenya kwenye ufahamu wa akili yangu, lilinizindua kutoka kwenye Bumbuwazi, bado nilikua kimya licha ya kua alinizindua, mara waliingia Wanaume wawili wakanitoa pale maana nilikua siwezi hata kutembea baada ya kukatwa kidole, safari hii nilipelekwa kwenye chumba cha Mahojiano

Bado palikua na ukimya wa hali ya juu sana, hata funda langu la mate nililisikia likishuka kwenye koo langu, niliketishwa kwenye kiti na wale wanaume kisha walitoka na kutuacha tukiwa wawili tu, niliangaza huku na kule hapakua na kamera yoyote ile, yule Mwanamke aliketi kwa utuvu sana

Akanitazama huku akipepesa kope zake, alinitazama kwa sekunde kadhaa kabla ya kutamka neno la kwanza

“Benjamin, kama utafanikisha kusema ilipo M21 utasalimisha Maisha ya Mtoto wako, utasalimisha pia Maisha yako. Sina muda wa kuuchezea” alisema, niliivuta midomo yangu yenye tafakari nzito ya niseme nini

“Ni kule Msituni” nilisema kwa kuropoka, nilipiga mahesabu ya kutaka kutoroka japo nilijua haitokua rahisi. Moyoni niliamini bado Elizabeth yupo Msituni pale nilipomwacha, kutokana na ule msako asingeliweza kupiga hatua yoyote kusonga mbele

“Ndiyo, M21 iko pale Msituni?” aliniuliza kwa shahuku kubwa, nikamtikisia kichwa changu, haraka akapiga simu mahali na kuagiza watu waje kunichukua. Wakaingia wanaume wawili baada ya sekunde kadhaa nilikua tayari nimefunikwa mfuko mweusi, eneo lile halikutakiwa kujulikana lilipo.

Nilisukumwa huku nikiisikia sauti ya Helkopta nikajua wananirudisha Msituni kama nilivyowaambia kua M21 iko huko Msituni, kwanza sikujua hata hiyo M21 ni kitu gani ila nilichotaka ni kuangalia uwezekano wa kunusuru Maisha yangu kwanza, kwa namna walivyonitendea ndani ya Black Site nilijua wazi wataniuwa Mimi, Suzan na Mtoto wangu

Sauti ya Helkopta na upepo uliotokana na Panga boi vilizidi kua karibu zaidi, mara nilisukumizwa ndani ya Helkopta kisha dakika hiyo hiyo iliruka kutoka Black site, nilianza kutumia taaluma yangu ya urubani kuhesabu baadhi ya vitu mfano dakika, mitembeo ya Helkopta ili kujua ni wapi tumetoka

Mpango wangu ulikua ni kukimbia Msituni kwasababu kama hawatoipata M21 wanayoitaka basi wataniuwa kama ambavyo niliambiwa kua Rais wa Tanzania alitoa amri ya Mimi kuuawa. Nilitumia zaidi hisia zangu kutambua, baadaye waliniondoa ule mfuko usoni, Helkopta ilikua juu sana kiasi kwamba kama nitajirusha kutoka juu hadi chini sitokua hai tena.

Wazo langu lilizidi kupiga kelele ndani ya akili yangu, mara walinifunga kamba mikononi, ilikua ni sawa na kuyeyusha ndoto zangu zilizochipuka ghafla, wakalizika zoezi langu la kutaka kutoroka, nilichokua nakiona chini ilikua ni Msitu mnene sana, nilifanikiwa kupiga mahesabu vyema na kujua uelekeo wa eneo ambalo nilikua nikipatiwa mateso, niliwaza kuhusu mpenzi wangu Suzan niliyemwacha kule kwenye mateso, akili yangu ikajaa ujasiri wa kufanya zoezi langu upya

Nilipepesa macho yangu kulia na kushoto, mwote mlikua na askari wenye Bunduki mkononi, nilizivuta pumzi vizuri sababu kuufikia ulipo mlango wa kutokea ilikua ni kitendo cha hatua mbili, hatua ambazo ziliwatosha wale Askari kunifyatulia risasi na kunimaliza

“Ni kheri kufa kishujaa kuliko kukisubiria kifo changu” nafsi yangu ilinisemesha kwa sauti ya juu, midomo yangu ikaanza kucheza huku sauti nyingine ya kifo ikiwa inanipigia kelele, mikono yangu haikuweza kufanya chochote kile isipokua kushikiliwa na zile kamba ngumu.

Hali ya hewa iliniambia kua tulikua juu, kila nilivyojaribu kuchungulia chini nilitishiwa kupigwa risasi. Nilizuga kidogo wakati Helkopta inabadili uelekeo na kulalia upande mmoja nikajinyanyua haraka na kujirusha kutoka juu ya Helkopta nikiwa nimefungwa kamba mikononi

Lahaula!!

Chini niliona maji mengi yaliyotuwama, ni kama ziwa au Bahari au Mto au hata Bwawa, akili yangu haikuweza kung’amua kwa haraka, ilikua kama Bahati kwangu nilizama ndani ya maji, nikaibuka juu nikiwa ninakunywa vikombe vya maji ya lazima, kutokana na ile kamba niliona kifo mbele yangu huku pumzi zikianza kunisaliti maana sikua na utulivu, huku ile Helkopta ikianza kusaka sehemu ya kutua.

Nikazama tena ndani ya maji mithiri ya jiwe, nikafika hadi chini, kumbukumbu zangu za utoto, Maisha yangu niliyoishi vilianza kuonekana mbele ya upeo wa macho yangu, ilikua ni dalili kua naelekea kufa Maji. Nilifumba macho yangu sababu sikua na namna ya kufanya isipokua kufa.

Nilishtuka sana, macho yalinitoka, nilikua nikilitazama jua kali la utosi lililokua likiwaka, nilihisi nimeshakufa, nilitamani kulia. Ghafla niliisikia ile Helkopta ikiranda randa juu, eneo ambalo nilidondokea lilikua limezungukwa na Miti mirefu hivyo haikua rahisi kwa wao kushuka, ndipo akili ilivyonikaa na kugundua kua nilikua sijafa, Mtu mmoja alikua akinivuta kuelekea nje ya yale maji, ndiye aliyeniibua kutoka kule chini.

Alinivuta haraka sana kama vile Mtu aliyekua akijua anachokifanya, akili haikutaka kuendelea kufikiria, macho yalikataa kumtazama yule Mtu, sikujua alikua ni Askari au alikua ni Mtu wa aina gani, kitu pekee nilichokabakiwa nacho kwenye mboni za macho yangu ni Mgongo wake wenye makovu kadhaa.  MWISHO WA SEASON 1 Kukiwa Na Comments Nyingi SEASON 2 Inakuja

Je, Benjamin anaokolewa au anakielekea kifo?

Hatma ya Mzee Kimaro na Elizabeth itakuaje?

AHSANTE!! Kwa kua nami katika season ya kwanza ya Riwaya ya MSALA.

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

 

 

 

 

49 Comments

  1. MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

    Hakika huu ni msala mwanawane ila aliambiwa tukimbie akabisha kilichomkuta mwamba hakika ni SITOSAHAU

  2. Stor nzuri,mwamba umetisha sanana stor inafundisha sana jinsi viongozi wanavyofanya vitu visivyofaa kwa watu wanaowaongoza,big up mwamba

  3. Msala ni adhimu na ambayo imeandikwa kwa ustadi mkubwa inayokisiwa na kugusa kila nyanja ya maisha ya watu na uovu uliopo kwenye jamii hii inakuwa kama ile riwaya ya JOKQ LA MDIMU watu wanakula vya wananchi kwa manufaa yao

Leave A Reply


Exit mobile version