IlipoishiaMiili ya Wanakijiji ilisambaa kila kona ya Kijiji, haikuchukua hata dakika mbili zile Helkopta zilianza kudunguliwa moja baada ya nyingine, pakawa kimya kabisa, halafu sauti ya Helkopta ikasikika ikipaa na kukatisha juu ya Kijiji ikatokomea kusikojulikana baada ya kufuta Ushahidi.

Elizabeth alikua amefukiwa na mchanga. Tukio zima la Kijiji kuteketea lilikua mikononi mwa Rais Mbelwa aliyekalia kiti cha Ikulu akiwa na washirika wake ambao walikua na uhakika kua walimmaliza kirusi aliyewasumbua. 

Endelea 

SEHEMU YA KUMI

Masaa 72 yaliyopita, usiku mmoja

Gari ndogo ya kifahari aina ya Mecedes Benz 360 ilikua ndani ya uzio wa Ikulu ikiwa inacheza cheza, ndani ya gari alikuwamo Rais Mbelwa akiwa amekaliwa kwa juu na Msichana wakiwa wanafanya mapenz*, suti ya Rais Mbelwa ilikua imekunjwa na kuwekwa pembeni, Msichana aliye juu ya Rais Mbelwa alikua ni Elizabeth Mlacha. Ufundi wake ukamfanya Rais amuulize Elizabeth

“Unataka nini?” Elizabeth akazidi kukoreza uno la Kinyaturu, akiikata ndizi ya Rais Mbelwa kwa fujo sana.

“Aaaaaahhh Bety wangu, fundi Aaah” Rais Mbelwa alizidi kuweweseka huku gari ikizidi kudundika, mita kadhaa kutoka lilipo gari walikuwepo walinzi wa Rais wenye silaha kali za moto wakiwa wanalikodolea macho gari hilo. Japo Elizabeth alikua akimpa dozi Rais Mbelwa lakini macho yake makubwa yenye kope bandia yalikua hayatulii kama Bendera, alikua akikodoa huku na kule hasa mahali ambapo palikua na Brifkesi.

“Griii!! Grii! Grii!” sauti ya simu ilikatisha zoezi hilo, Elizabeth akajitosa pembeni akiwa anamdadisi zaidi Rais

“Yes..” alisema Rais akiwa mchovu huku akiwa anahema sana

“Namtuma Mtu sasa hivi, kumbuka hii ni siri” alisema Rais kisha akavalia vizuri, mara moja wakashuka kwenye gari, kama hukuona gari ilivyokua ikicheza basi ukiwaona unaweza sema hakuna walichofanya. Rais Mbelwa alijikokota na Brifkesi lake kisha wakaingia ndani.

“Mgeni wangu, mkirimu” ilikua ni sauti ya Kibabe iliyotolewa na Rais Mbelwa akiwa anamtazama Mke wake aliyeenda Umri, alikua amesimama mbele ya Rais na Elizabeth, sura ya Mke wa Rais ilibeba mazito aliyokua anafanyiwa na Rais Mbelwa.

“Sawa Baba” alisema Mke wa Rais, kisha aliuchukua Mkoba wa Elizabeth na kwenda nao chumba cha wageni ndani ya Ikulu, Rais Mbelwa hakua akimheshimu Mke wake, alikua Mbabe, Mkorofi ambaye jambo dogo alimwangushia kipigo Mke wake.

Mapenzi yake aliyaweka zaidi kwa Elizabeth Mlacha. Baada ya kumaliza kutoa maagizo alimwambia Elizabeth

“Nisubirie nina jambo la kiofisi sasa hivi” alisema Rais Mbelwa, akamtandika Busu Elizabeth kisha akaelekea ndani ya Ofisi yake hapo Ikulu, ulinzi ndani ya Ikulu ulikua Mkubwa sana. Bado macho ya Elizabeth yalilitazama Brifkesi hilo kama fisi anapoutazama mnofu, alishuzha pumzi kisha aliketi

Walinzi wawili wenye silaha walikua kando yake, akajichekesha kidogo kisha akaomba aelekee chooni, Mlinzi mmoja akaongozana na Elizabeth hadi mlango wa chooni na kumwacha Elizabeth akiingia humo. Baada ya kuingia Chooni aliongeza uharaka na umakini, akaelekea chini ya sinki la kunawia maji, chini hapo akapapasa na kutoa nailoni moja yenye kifaa kidogo, baada ya kukitoa akakiwasha kikawa kinawaka taa nyekundu, kisha akapapasa chini kwenye moja ya tailizi akaifunua na kutoa simu ndogo, akaiwasha haraka na kupiga mahali

“Muhonzi, tageti namba moja” baada ya kuzungumza aliirudisha ile simu chini ya Tailizi, kisha akakirudisha kile kifaa chini ya Sinki, haraka akafungulia maji, akanawa kidogo na kufunga maji, akatoka akamwonesha tabasamu yule Mlinzi.

**

DAKIKA CHACHE BAADAE

Nje ya Ikulu, mita kadhaa ilisimama pikipiki moja iliyopanda hewani, alishuka Mwanaume mweupe, mwembamba aliyevalia mawani ya macho, umri wake ilisogea kidogo mbele ya Elzabeth, huyu ndiye Muhonzi aliyepigiwa simu na Elizabeth kutoka Ikulu, akiwa hapo aliiyona gari moja ikitoka Ikulu.

Ilitoka bila Msafara wowote ule, naye akawasha Pikipiki yake na kuanza kuifwata kwa nyuma.

Gari hiyo ndogo nyeusi iliyofungwa vioo vyeusi visivyoonesha ndani iliishika barabara ikiwa inatembea kwa mwendo wa kawaida, haikua gari ya kawaida, ilikua na kizuia risasi. Muhonzi aliifukuzia kwa nyuma hadi ilipofika maeneo ya Kamata, hapo ilisimama ikipisha treni iliyokua ikiingia kituo kikuu ya Treni

Muhonzi alisimama kando ya gari hiyo huku akijionesha kua alikua katika safari zake za kawaida, treni ilipomaliza gari zilianza kufanya safari usiku huo, gari ile iliyotoka Ikulu ilikunja kulia huku ikiipa mgongo kituo cha treni, ilipofika PIZA HUNT ilizama ndani ya Maegesho ya Hapo Piza Hunt

Muhonzi naye aliingia maegesho huku akili yake akiiwekeza kutazama ni Nani atashuka ndani ya gari hiyo, alishuka mwanaume mmoja mnene akiwa na Brifkesi nyeusi aliyotoka nayo Ikulu, mara alifika Mwanaume mmoja akaichukua kisha akaingia nayo eneo la chini ya jengo hilo la kuuzia Piza, halafu yule Mtu kutoka Ikulu alirudi ndani ya gari kisha akaondoka eneo hilo bila kuonesha wasiwasi wowote.

Muhonzi alishusha presha yake, baada ya Wamaume kuzama na Brifkesi wakatokea Wanaume wengine wawili wakiwa na silaha wakasimama eneo hilo la kuingilia eneo la chini ya jengo la Piza Hunt, Muhonzi akawasha Pikipiki yake na kuondoka hapo huku akiwaacha walinzi wakiwa makini eneo lile.

Safari ya Muhonzi akiwa na Pikipiki iliishia kwenye nyumba moja iliyopo Ilala Bungoni, nje alikutana na Waarabu kadhaa ambao walikua wakimiliki nyumba hiyo iliyopakana na nyumba ambayo Muhonzi alihitaji kufika, akawasalimia kisha akaiweka Pikipiki yake ndani ya geti, dakika tano baadaye zilimkuta akiwa kwenye chumba kimoja akitazama karatasi moja nyeupe yenye maandishi ya siri

Karatasi hiyo ilikua ya Mkataba wa makubaliano kati yake, Elizabeth na Chama cha Upinzani cha TUYTA, chama ambacho kiliwapatia ofa akina Elizabeth ya zaidi ya Bilioni 30 endapo watafanikiwa kunasa nyaraka za siri za Rais Mbelwa. Kilikua ni kipindi ambacho Tanzania ilikua ikijiandaa na Kampeni za Uchaguzi Mkuu, Mgombea wa Urais wa TUYTA alihitaji nyaraka hizo ili kumdondosha Rais Mbelwa.

Muhonzi alikuna kichwa chake, mahali zilipo nyaraka za ufisadi na mauwaji ya Rais Mbelwa ilikua kizungumkuti kupafikia, japo walikubali ofa hiyo na kupewa kitita cha pesa ya awali lakini bado hapakua na dalili ya wao kufanikiwa.

**

“Mkuu zimefika” alisema Mwanaume mmoja Mweusi akiwa amesimama mbele ya Rais Mbelwa.

“Kazi nzuri, hakikisha kila kitu kinaenda kama ilivyopangwa”

“Sawa Mkuu” aliitikia kisha aliondoka ofisini, hekaheka ndani ya Ikulu zilikua kubwa kwa kipindi hicho, ingia toka zilikua nyingi kuhakikisha kila jambo linaenda kama lilivyopangwa, Rais Mbelwa alihema kisha akajigeuza geuza kama chapati juu ya kiti alichokalia, kando palikua na chupa ya Mvinyo akaivuta na kumimina kiasi kidogo kisha akapiga funda zito kabla ya kuachia sauti ya kupita kwa mvinyo huo usiochakachuliwa.

Zaidi ya dakika sitini zilipita, Elizabeth alikua ameketi sebleni akisubiria Rais Mbelwa atoke Ofisini, walinzi walikua wakimkodolea macho mrembo huyo aliyefanywa mchepuko na Rais Mbelwa. Akiwa hapo Mke wa Rais Mbelwa aliufungua mlango kisha akampa ishara fulani tata sana Elizabeth halafu Elizabeth akaijibu kwa ujanja bila hata Walinzi kushtuka

“Ooh samahani nahitaji kutumia choo tena” alisema Elizabeth akiwa amelishikilia tumbo lake dogo, walinzi wakapeana zamu, mmoja akamsindikiza hadi Mlango wa Choo, Usalama ndani ya Ikulu ulikua wa kutosha bila kujalisha kua alikua ni kimada wa Rais.

Alipofika haraka alifanya kilichompeleka ndani ya choo hicho, akaitoa ile simu na kile kifaa maalum cha kunasa mawasiliano, bila kifaa hicho unapoingia Ikulu huwezi kuitumia simu yako kufanya mawasiliano kutoka ndani kwenda nje au kutoka nje kwenda ndani, Rais Mbelwa alihakikisha hata Mke wake hawasiliani na yeyote yule

Alipowasha tu, mara moja simu iliita

“Muhonzi” aliita

“Yes Mam” ulisema upande wa pili

“Umefanikiwa kujua mahali ilipo hamishiwa ile Brifkesi?”

“Yah!! Ni Piza Hunt, inaonekana Rais anaficha vingi huko” alisema Muhonzi, ghafla mlango wa chumba cha Choo uligongwa.

“I’ll call u Back” alisema Elizabeth kisha haraka alirudisha vitu mahali palivyokua, akajiweka sawa kisha akaenda kufungua mlango. Alikutana na sura mgumu ya Mlinzi wa Ikulu

“Rais anakuhitaji” alisema, Elizabeth akaitikia kwa kichwa kisha taratibu kwa mwendo wa Kinyonga alitembea akiwa amevalia viatu vyake virefu, aliitwa Ofisini kwa Rais Mbelwa

Rais Mbelwa alikua dhaifu sana kwa Elizabeth, aliuthibitisha ule msemo wa waswahili usemao penzi kitovu cha Uzembe. Japo Rais alikua na nguvu sana ndani ya Nchi lakini Kitengo cha Usalama wa Taifa kilipanga kummaliza Elizabeth wakiamini udhaifu wa Rais kwa Msichana huyo unaweza sababisha Nchi kuingia kwenye hatari, Rais alikua akiifahamu hiyo taarifa

“Bety” aliita Rais Mbelwa

“Abee” kwa kisauti chake kama Wema Sepetu aliitikia Elizabeth, ukimwona unaweza fikiria ni Msichana dhaifu sana lakini alikua na wasifu mkubwa na wa kutisha, akiwa na miaka 21 tayari alikua amezunguka takribani mataifa sita ikiwemo Iraq, Uingereza na Jamhuri ya Ireland

Alihitimu mafunzo maalum ya Ujasusi, ujeshi na mapigano ya judo na kareti, wachache sana walimtambua Msichana huyo kama Misenari anayefanya kazi kama Jasusi wa kukodiwa. Mikono yake aliiweka kwa adabu mbele ya Rais Mbelwa huku dimpozi zake zikichanua vyema.

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Kumi Na Moja ya MSALA hapa KIJIWENI

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

13 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version