Ilipoishia “Upande wa pili, Muhonzi alikua akiteseka ndani ya Godauni, Zagamba alimshikilia ili aipate Nyaraka M21 kutoka kwa Elizabeth, Alikua ndani ya chumba kimoja chenye dirisha dogo tena liko juu sana, hewa ilikua nzito lakini kibaya zaidi alipaswa kujisaidia ndani ya Chumba hicho, Mikono yake ilifungwa kamba ili asifanye ujanja wowote ule.
Akili yake ilishashtuka mapema kua kuna lililompata Elizabeth ndiyo maana Zagamba alikua mwenye hasira sana, tumaini la yeye kuendelea kua hai aliliona kua finyu kabisa, akaanza kutafuta namna ya kujisaidia hapo ili aweze kuokoa uhai wake.
Kabla hajafanya chochote akakumbuka tukio moja… ENDELEA
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Ndani ya PIZA HUNT
Muhonzi alikua chini ya Ulinzi wa walinzi wa eneo la chini la Piza Hunt, mahali ambapo Nyaraka M21 ilikua imehifadhiwa kwa Maagizo rasmi ya Rais Lucas Mbelwa, Walinzi hao walionekana wazi kua hawakua Raia wa Tanzania, Rafudhi yao ilikua ya Kikongo. Kiswahili chao pekee kilimfanya Muhonzi atambue kua eneo hilo halikua eneo salama kwake.
Walimzunguka mara baada ya kuufungua Mlango wa eneo lenye mfanano na Maktaba, kisha mmoja ambaye alikua mweusi tii, akiwa na Bunduki alimuuliza Muhonzi
“Ni kipi kimekuleta hapa, huonekani kama Mtu wa hapa” alimalizia kwa kumnyooshea Bunduki Muhonzi, jicho la Muhonzi lilimtoka Pima, alianza kumkagua Mlinzi huyo mwenye sare nyeusi
“Nakuuliza tena Kijana, nini kimekuleta hapa?” safari hii aliikaza sura yake ngumu yenye vipere vingi, tena kwa Msisitizo alimtolea macho
Muhonzi mkononi alikua na kisu, kiuno chake kilikua na Bastola, akaporwa vyote. Kisha akakamatwa na kuingizwa ndani zaidi, hakuamini macho yake, aliona Madawa mengi ya kulevya yakiwa yanawekwa kwenye mifuko, palikua na kitu mfano wa Maabara kubwa,
walinzi hawakutaka Muhonzi atazame zaidi akasukumizwa mbele hadi kwenye chumba kimoja.
Chumba hicho kilikua na meza na Kiti kimoja, pia palikua na taa iliyoshushwa karibu zaidi na kiti na meza, akakalishwa hapo kisha yule Kiongozi wa wale Walinzi akaketi pia huku mikono yake akiwa ameiegemeza kwenye ile meza.
Walinzi wengine wakatoka na kuufunga mlango, wakabakia wawili tu ndani ya Chumba hicho, yule kiongozi akamtazama Muhonzi kisha akatabasamu na kuachia kicheko kidogo
“Niambie nini kimekuleta hapa, wewe ni Nani?” akayatupa maswali mawili kwa Mkupuo, Muhonzi hakujibu chochote, muda wote aliwaza namna Maisha yake yataishia mikononi mwa Mwanaume huyo, akayaruhusu Macho yake kucheza kama pia
Akaona wazi kua nafasi pekee ya yeye kua hai ni kujitetea hapo, Yule Mlinzi kiongozi alipoona hajibiwi chochote akazunguka na kumfwata Muhonzi kwa hasira, akamnyanyua kama vile ana mnyanyua Mtoto mdogo. Haraka Muhonzi akaiyona peni kwenye mfuko wa shati la yule Mlinzi akaipigia mahesabu mazito baada ya kuona Mwanaume huyo amehamanika
Akanyoosha mkono haraka na kuifungua kisha akamkita nayo eneo la shingo, alilenga mshipa muhimu zaidi, damu nyingi zikamruka yule Mlinzi, akapepesuka na kuanguka chini huku akikoroma na kutapatapa, pumzi zikamkaa sawa Muhonzi akaishika shingo yake iliyokua imekutana na dhoruba kali muda mchache uliopita
Akaichomoa Bastola kiunoni kwa yule Mlinzi kisha akaiweka sawa, kitu cha kwanza alichowaza ni kupata lile faili, kama hatofanikiwa kulipata basi pengine watalikosa kabisa. Alikua na uhakika kua faili lipo ndani ya eneo hilo la chini, akaruhusu kumbukunbu zake zihesabu idadi ya walinzi aliowaona, walikua zaidi ya Walinzi tisa wenye silaha kali za moto.
Akasogea mlangoni taratibu na kuanza kuufungua mlango, akaona viatu vya kijeshi pande zote mbili yaani kulia na kushoto kwa ule Mlango, walinzi hao hawakushtuka kama mlango umefunguliwa kwa namna ambavyo Muhonzi aliufungua mlango huo kitaalam sana.
Akairejesha Bastola kiunoni kisha akapiga mahesabu namna ya kukabiliana nao, umbo la Muhonzi lilikua jembamba tena dogo kiasi kwamba Mtu hawezi kufikiria kama anaweza hata kurusha ngumi, akausogeza mguu wa kulia na kisha wa kushoto, hapo akapiga mahesabu ya kukita shingo za Walinzi hao kwa wakati mmoja, akayapiga mahesabu yake vizuri ni sehemu gani aziguse
Akachomoka kama Kipanga kisha akawapiga vifuti vya maana maeneo ya shingo, akawazimisha wote kwa wakati mmoja kisha akawaburuza hadi ndani ya chumba na kuwafungia humo, akatoka na kukutana na korido moja fupi lenye vyumba vitatu vilivyokaribiana.
Taratibu akaanza kutembea kwenye korido hiyo iliyo tulivu sana, hakuna Mtu mwingine aliyekutana naye ndani ya Korido hiyo hadi anafika korido nyingine , hapo akajiuliza ni kwanini pako kimya sana, akapata wazo la kufungua chumba kimoja baada ya kingine. Kila chumba alichokifungua kilikua kitupu.
Ukimya ulizidi kumzoga Muhonzi hadi akaanza kupatwa na woga, akaendelea mbele zaidi kutafuta chumba ambacho kina hizo nyaraka za Siri, pasipo kujua kumbe tayari walinzi wote walishapewa taarifa ya kutoka ndani ya Eneo hilo ili sumu isambazwe. Moja ya vitu ambavyo vilikua havitakiwi katika eneo hilo ni purukushani, ili kuendelea kuliweka eneo hilo salama ilikua ni lazima waweke mfumo wa sumu ili kama kutatokea uvamizi basi haraka wawamalize maadui zao kimya kimya.
Walinzi na viongozi walitoka ndani ya jengo, kisha wakawa wanasubiria maelekezo maalum kutoka juu yaani kwa Rais ambaye alikua akilitazama tukio la uvamizi akiwa Ikulu, mkononi alikua na kikombe cha Kahawa kilichokua kinafuka moshi.
Kila mmoja alikaa kimya kusubiria agizo la Rais ambaye naye alikua makini sana kumtazama Muhonzi kwenye kompyuta. Akayavuta mate kisha akayapitisha kooni
“Achia sumu sasa hivi” alisema Rais Lucas Mbelwa, mara moja wataalam wa Ulinzi wa pale Piza Hunt waliachia Sumu iliyokua inafuka kupitia chemba za hewa, kila mmoja alikaa kimya kuangalia namna Muhonzi atakavyoteketea, Mke wa Rais Mbelwa alikua hapo akiangalia tukio hilo nyeti, huku akitabasamu kwasababu yeye ndiye aliyeutoa mpango wa kuibiwa kwa hizo nyaraka.
Ndani ya Piza Hunt, hatua za taratibu zilikua zikipigwa na Muhonzi tena kwa tahadhari ya hali ya juu kabisa, ghafla alianza kuhisi uzito wa hewa ndani ya Jengo, akatambua kwa haraka kua hiyo ilikua ni sumu, akataharuki, haraka akaanza kutafuta njia ya kutoka hapo.
Alipojaribu kutaka kufungua mlango aliona tayari ulikua umefungwa, akajikuta akianza ‘kuhaha’ kwa kukosa hewa safi, ndani ya dakika moja tu alianza kushindwa kupumua vizuri akanguka chini, hapakua na hewa nyingine aliyokua akiivuta zaidi ya hiyo sumu.
Sasa alijiona akikikaribia kifo alichokitafuta mwenyewe, akaanza kutetemeka huku akizidi kulegea lakini ghafla alikuja Mtu aliyefunika uso wake kwa ‘Mask’
Mtu huyo alikua amevalia koti jekundu alilolitumia kuficha sura yake, akamwinua Muhonzi na kumvisha Mask iliyoanza kumpa hewa nzuri Muhonzi. Nguvu ilimpompata vizuri akajaribu kumtazama usoni, akagundua Mtu huyo alikua Ni Elizabeth Mlacha. Akatoa tabasamu la kuchanua, Elizabeth akageuka na kuitazama Kamera moja iliyo nyuma yao, alishagundua kua walikua wakifwatiliwa kupitia Kamera hiyo.
Rais alishtuka, wote walishtuka. Elizabeth akafunua kofia kichwani pake, akatoa ile Mask ili waiyone sura yake, Rais akatema kahawa kwa Mshituko baada ya kumwona Mchepuko wake, akagundua sasa kua kilichomfanya Elizabeth akawa karibu naye ni hizo faili za siri, papo hapo akapaza sauti Rais akiwaambia walinzi
“Hakikisheni hakuna anayetoka mzima” alisema Rais kwa ghadhabu nzito. **
Elizabeth na Muhonzi wakaanza kutafuta nyakara M21 ndani ya lile jengo, ramani yote tayari Elizabeth alishapewa na Mke wa Rais, ikawa rahisi kufika ilipo shelf maalum ya kuhifadhia nyaraka, kwanza wakaharibu kamera zote ili wasigundulike walipo huku wakijua fika kua muda mchache ujao kutakua na patashika nzito sana.
Elizabeth alikua na simu ambayo ndiyo iliyokua ikiwaongoza kuelekea mahali zilipohifadhiwa Nyaraka hizo, walipofika mlango husika walimwona Mtu mwingine akitoka hapo, Mtu huyo alikua amevalia kofia nyeusi, alikua na Mask usoni na kwa haraka haraka waligundua kua alikua mwanaume, mkononi alikua na Brifkesi ambalo kwa haraka waligundua kua ndimo ilimo Nyaraka M21.
Mtu huyo alikimbia kwa haraka kuifuata korido moja ndefu, haraka Elizabeth alimfwata huku Muhonzi akiingia kwenye chumba ambacho yule Mwanaume alitokea.
Mfukuzano ulikua mkali kwa hatua kadhaa, kisha ghafla yule Mwanaume alisimama, aligeuka kisha aliliweka lile Brifkesi chini, akatabasamu na kumwambia Elizabeth
“Najua umekuja kwa ajili ya Nyaraka M21, hiyo hapo lakini unapaswa kunimaliza kwanza” alisema kwa kujiamini sana, aliongea kwa sauti iliyojaa Bashasha kama walikua kwenye utani, Elizabeth akajua hapo haitokua kazi rahisi kupambana na huyo Mtu, akaangalia saa yake.. Nini kitaendelea?
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
7 Comments
Wa Kwanza hapa kwenye huu msala🤞🤞
Msala ni msala kweli
Ni hatariiii
,
Duuuuh 🔥
Admine Mambo unayafanya yawe pambe saana yàan Ni bul bul dàah🔥🔥
Msala ni msala haswaa