IlipoishiaMfukuzano ulikua mkali kwa hatua kadhaa, kisha ghafla yule Mwanaume alisimama,  aligeuka kisha aliliweka lile Brifkesi chini, akatabasamu na kumwambia Elizabeth 

“Najua umekuja kwa ajili ya Nyaraka M21, hiyo hapo lakini unapaswa kunimaliza kwanza”  alisema kwa kujiamini sana, aliongea kwa sauti iliyojaa Bashasha kama walikua kwenye  utani, Elizabeth akajua hapo haitokua kazi rahisi kupambana na huyo Mtu, akaangalia saa  yake.. Endelea 

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

Alibakiza dakika chache za kutoka ndani ya jengo hilo vinginevyo vikosi vitafika hapo na  kunaswa. Akageuka nyuma kuona kama Muhonzi alikua karibu ili kazi ya kupambana na  Mwanaume huyo isiwe ngumu lakini palikua patupu, ilimpasa yeye mwenyewe alichukue  Brifkesi hilo.

Akajiweka sawa ili kuupima uwezo wake kwa Mwanaume huyo asiye mfahamu, wakati  anamtafakari akaona kwenye shati palikua na namba za utambulisho, akagundua kwa wepesi  kua Mtu huyo alitokea Ikulu kwa Rais Mbelwa. Pengine hiyo ilikua ni silaha ya siri ya Rais  Mbelwa ndani ya Jengo hilo 

Elizabeth akajiandaa kumshambulia kwa kasi ya kicheche ili amalize kazi mapema kuliko  kawaida, lakini kila pigo alilolipeleka kwa Mwanaume huyo lilikumbata na upepo, yote  aliyoyarusha hayakumfikia aliyakwepa. Kisha alimpa tena tabasamu, Elizabeth akaona hizo  ni dharau za kutosha, akajikunjua na ngumi mbili alizozipangilia 

Zote zilikwepwa na mwanume huyo ambaye baada ya kukaa sawa alirusha mapigo matatu ya  mguu wa kushoto, mapigo mawili yakatua kwenye bega la Elizabeth, wakati anapepesuka  yule Mwanaume akadandia ukuta na kuachia pigo lingine 

Pigo hilo lilikua maalum kwa ajili ya kukita sehemu ya kifua cha Elizabeth lakini kwa haraka alijivingirisha na kujiokotanisha. Elizabeth akapanga tena pigo, safari hii hakutaka kwenda  kwa pupa sababu alishagundua Mwanaume huyo ana ujuzi mkubwa wa Mapigano. 

Akawa anatupa mapigo kwa akili kubwa sana, angalau sasa akaweza kumgusa Mwanaume  huyo kwa ngumi ya kuparaza iliyopita mbavuni hadi akakata kifungo cha Shati la mwanaume  huyo. 

Yule Mwanaume akabonyea kidogo kama Mtu mwenye kibiongo halafu akawa anachezesha  kichwa chake kama nyoka Cobla, mtindo huo ukawa unamchangaya sana Elizabeth akajikuta  akiambulia vichapo vya kufwatana hadi akaanguka chini, hakuweza kumsoma kabisa  Mwanaume huyo ambaye alikua akibadilika sana kwenye mapigano. 

Damu ikaanza kumtoka mdomoni, akazidi kupandwa na hasira akajikuta akikurupuka kwenye kurusha mapigo, akawa anapigwa kwa kila pigo alilokua anarusha hadi akabamizwa  ukutani kwa nguvu sana, akashindiliwa na pigo zito la shingo, likampeleka chini, kisha yule  Mwanaume taratibu akamsogelea Elizabeth na kuanza kumkagua 

“Nilikwambia hutoweza kupata M21” alisema Mwanaume huyo, kisha alisimama na  kunyanyua Mguu wake ili aikanyage sura ya Elizabeth, lakini ghafla alikutana na teke zito  lililomtupa mita kadhaa, mbele yake alimwona Kijana mwemye umbo kama lake, Kijana  huyo alikua ni Muhonzi 

Kwanza yule Mwanaume hakuamini kama teke hilo zito lilitoka kwa Kijana huyo  Mwembamba ambaye ukimtazama kwa haraka utaona ni namna gani alikua mlegevu, jambo  la kwanza alihitaji kujua kuhusu hali ya Elizabeth Mlacha. 

“Uko sawa?”  

“Faili iko kwnye hilo Brifkesi” akasema Elizabeth akiwa anajivuta aketi vizuri, Brifkesi  lilikua chini, kazi ilikua ni Nani anayeweza kuliokota Brifkesi kwa haraka. Wote wakaiwahi  Brifkesi lakini kuiokota haikua jambo la urahisi, alipozubaa kidogo tu Muhonzi akalambwa  mtama wa nguvu kisha yule Mwanaume akaliokota Brifkesi, alishajua kupambana na  Muhonzi siyo jambo rahisi, alichofikiria hapo ilikia ni kutimka.

Akaanza kukimbia kuuelekea Mlangoni lakini Muhonzi akafyatua risasi ikamchapa  Mwanaume huyo Mguuni akaanguka chini, Muhonzi akasogea hapo na kuliokota Brifkesi,  kisha akamtandika risasi nyingine tatu za kumnyong’onyeza. Haraka akarudi kumfwata  Elizabeth, wakaongozana ili waondoke lakini walipofika mlangoni walisikia michakacho,  wakajua haraka kua kuna askari waliofika hapo. 

“Tunafanya nini?” akauliza Muhonzi, Elizabeth akautoa mkoba wake mdogo aliouvaa  mgongoni, akatoa baruti, akaziwasha zikaanza kutoa moshi mzito kisha haraka akaufungua  mlango na kuziachia, zikasababisha moshi mzito. Walinzi wakajikuta hawaoni chochote,  muda huo Elizabeth na Muhonzi wakautumia kupambana na walinzi wachache kisha  wakazivaa nguo zao na kutoka nje ya jengo la Piza Hunt, huko nje tayari Watu walishaanza  kujaa baada ya milio ya Risasi kusikika, Muhonzi na Elizabeth walitoka wakiwa wameziba  sura zao kwa Mask ambazo wale walinzi waliingia nazo. 

Hakuna aliyewashitukia, wakavuka barabara na kuingia kwenye gari ambayo Elizabeth  alifika nayo, wakaishika barabara ya kuelekea njia panda ya Keko, wakatokomea. 

** 

Taarifa ya kutoweka kwa Elizabeth na Muhonzi ilizidi kupasua kichwa cha Rais Lucas  Mbelwa, kibaya zaidi tayari mafaili yalikua yameshaibiwa ikiwemo nyaraka M21 ambayo  ilikua na siri za kutosha za Rais Mbelwa. Akaagiza Wasakwe kila koja ya Nchi, tena Msako  ufanyike kimya kimya ili usije leta taharuki. 

“Hatuna muda wa kuendelea kua hapa Muhonzi, cha Msingi kwasasa ni kukutana na  Mnunuzi tumpatie taarifa kisha tusunde kibunda cha pesa tutafute Nchi tukafurahi” alisema  Elizabeth baada ya kufika yalipo Makazi yao ya Siri, maeneo ya Ilala Bungoni. 

Tabasamu pana likaipamba sura ya Muhonzi 

“Nina imani tutaishi Maisha ya kifahari sana, kwanini tusiende Moroco my love?” akauliza  Muhonzi 

“Popote utakapo, nitaambatana na wewe” mara simu ya siri ilianza kuita, hakua mwingine bali Zagamba, alishapewa taarifa na Mke wa Rais Mbelwa kua tayari faili limeibiwa,  Elizabeth akaipokea simu hiyo. 

“Uko wapi?” akahoji Zagamba kwa sauti iliyotoka bila salamu. 

“Hapana shaka umesikia kua nyaraka zimepatikana, niambie tunafanyaje makabidhiano”  akauliza Elizabeth, ukimya ukatamaraki kidogo kisha akajibu. 

“Jitahidi ufike Msata, nakutumia Anuani sasa hivi” akasema Zagamba Halafu simu ikakatika,  ikamwacha Elizabeth na wasiwasi 

“Anasemaje?”

“Anahitaji nifike Msata, sijui kwanini, Oooh anuani imeingia” akaifungua anuani, akakuta ni  Msata tena nyakati za Usiku, kwa kiasi kikubwa ilimpa wasiwasi. 

“Sikia Muhonzi, hatuwezi kwenda wote huko, utabaki hapa na nitakupa taarifa ya kila hatua  nitakayoipiga, kama kuna baya basi lisitupate wote, naamini hii itakua kazi ya mwisho”  alisema Elizabeth kisha akayatupa macho yake kwemye Brifkesi. 

“Unafikiria nini?” akauliza Muhonzi akiwa naye analikodolea macho Brifkesi lililo juu ya  meza ndogo 

“Ni lazima tulifungue kwanza, hatuwezi kuifanya Biashara tusiyoielewa” akasema Eizabeth  kisha akafungua droo na kuchukua vifaa kwa ajili ya kufungua Brifkesi hilo lililofungwa kwa  namba Maalum, ikawachukua dakika ishirini kulifungua bila kulivunja, ndani yake  mlihifadhiwa Flashi moja mpya, ndicho kitu pekee kilichotunzwa humo. 

“Nafikiri hii ndiyo yenye kutunza, basi tuiangalie kwanza” akasema Elizabeth, akampatia  Flashi Muhonzi. Baada ya kuiweka kwenye kompyuta yao walianza kuziona taarifa za  kutisha ambazo zilitunzwa ndani ya flashi.  

Giza lilipoingia Elizabeth alianza safari ya kuelekea Msata kwa ajili ya kufanya  Makabidhiano na Zagamba, ndipo Mkasa mzito ulipomkuta huko hadi akakutana na  Benjamin Kingai. 

** 

Muhonzi alipomaliza kukumbuka namna walivyoiba Nyaraka M21, akakumbuka kua alikua  na kazi ya kuhakikisha anatoroka ndani ya Godauni hiyo vinginevyo anaweza akauawa hapo  na Zagamba mwenye hasira. Akajisogeza hadi mlangoni, palikua na eneo la ukuta lenye  ncha, akaanza kufanya jitihada za kukata ile kamba kwa nyuma, aliendelea na zoezi hilo kwa  zaidi ya dakika kumi na tano bila mafanikio hadi akakata tamaa ya kutoroka hapo. 

Upande wa Pili, ndami ya Msitu wa Magoroto. Jua la utosi lilikua likiipiga ardhi hiyo pamoja  na kila kilichomo ndani yake, Malikia Zandawe alikua amesimama juu ya mlima mdogo ulio  pembezoni mwa Msitu huo, macho yake yalikua yakiangalia uzuri wa Bonde la Maji lililokua  likitiririsha Maji kutoka juu ya Kilima hicho. 

Hali ya hewa ilikua nzuri na ya kuvutia sana iliyompa utulivu wa kutosha, mara ndege wake anayemtumia kwa ajili ya Ulinzi alifika hapo, ndege huyo aliyempa jina la Gola alitua  akitokea safari ya Mbali kuitafuta Black Site ambako mateso makali yalikua yakifanyika. 

Haraka Zandawe alipiga goti ili azungumze na ndege huyo kwa Lugha ya ndege ambayo  alikua akiielewa vizuri, akapewa taarifa ya wapi ilipo Black Site, Basi uso wa Zandawe  ukatawaliwa na tabasamu la maana, akampa busu ndege huyo kisha akamruhusu aondoke,  yeye akakimbilia yalipo Makazi yake. 

Akamkuta Benjamin akiwa anacheza na Sokwe Mkubwa ambaye ni rafiki wa Zandawe,  alifika akiwa anahema huku tabasamu likizidi kuongozeka 

“Kuna nini, mbona uso umechanua kiasi hicho?” aliuliza Benjamin huku akiacha kucheza na  sokwe, akili yote akaihamishia kwa Zandawe.

“Nimejua ni wapi ilipo” 

“Ilipo nini?” 

Basi Zandawe akamsogelea Benjamin na kumwambia 

“Sehemu uliyoteswa” 

“Sehemu niliyoteswa?” akahoji Benjamin kwa Mshangao mkubwa sana, alichokisikia alihisi  kama yupo Usingizini, ndipo akakumbuka kua Zandawe alimtuma ndege kuchunguza ilipo  Black Site. Akanyanyuka alipokua ameketi akamsogelea Zandawe 

“Una hakika?” 

“Nilikwambia, Gola ni mpelelezi wangu nimtumainiye, yeye ndiye anayenipa taarifa  nisizozijua, nzuri na Mbaya, hata siku ulipoanguka kutoka juu ya Helkopta ni yeye ndiye  aliyenipa taarifa” alisema Zandawe, uso wa Mshangao ukamjaa Benjamin Kingai. 

“Kwahiyo imejulikana ilipo, sasa…” Benjamin mwenye wenge zito akakatishwa na kauli ya  Malkia Zandawe 

“Tulia kwanza Benjamin, naamini kama Mtoto wako na Mpenzi wako wapo hai basi  utawapata tu” kisha aligeuka pembeni, japo alisema hivyo lakini alijisikia kuumia ndani ya  nafsi yake, kisha akageuka akiwa mwenye kutabasamu 

“Tutaenda huko kwa ajili ya kuikomboa familia yako” alisema Malkia Zandawe kisha  aliondoka hapo ndani ya Pango, yule Sokwe akamfwata kwa nyuma Zandawe. Wote  walimwacha Benjamin akiwa ana furaha ya ajabu sana. 

** 

Mateso makali yalikua ndiyo sehemu ya Maisha ya Elizabeth Mlacha, kila kona ya mwili  wake ilitawaliwa na maumivu makali, alikua amefungwa mnyororo mikononi akiwa  ananing’inia huku damu iliyoambatana na udenda ikiwa inaendelea kumvuja. Hata nguo  aliyokua ameivaa ilikua imetapakaa damu 

“Iko wapi M21?” aliuliza Bi. Sandra, masaa kadhaa yalipita Elizabeth akiwa anaendelea  kuteswa bila kusema chochote. 

“If you want to Kill Me, just Go ahead, but you’ll find nothing ( Kama unataka kuniuwa  niuwe lakini hutoambulia chochote)” alisema Elizabeth kwa sauti chovu iliyojaa maumivu  makali sana, Bi. Sandra alimtazama Elizabeth, moyoni akajisemea 

“Sijapata kumwona Mwanadamu Mbishi na Mgumu kama huyu” aliutupa mkono wake  uliojaa damu kwa hasira sana kisha akarudi kuketi kitini akitafakari ni namna gani afanye ili  apate taarifa nyeti. Haraka akanyanyuka kutoka kitini kwa hasira akamfwata tena Elizabeth,  akamwambia

“Ukiendelea kuwa jeuri utamfuata Rais alipo” alisema kisha akaondoka ndani ya chumba  hicho, haraka Elizabeth akatambua fika kua Rais alikua ameshauawa na kilichokua kinaenda  kufanyika ni Uasi mkubwa wa kuitawala Nchi. 

Elizabeth akiwa ananing’inia akaukumbuka Usiku wa Heka Heka.

Nini kitaendelea? 

Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

10 Comments

  1. Unajua naisoma mara mbili mbili lakini naona Bado napaswa kuirudia kongore sana Kwa ndugu Mwandishi hakika ni utunzi maridhawa

Leave A Reply


Exit mobile version