“Ilipoishia” Roho ya Elizabeth ilifukuta kwa maumivu Makali sana, hapo alipaswa kufanya kazi mbili, moja ni kumwokoa MUHONZI Kutoka mikononi mwa mwenyekiti wa chama cha Upinzani na pili alipaswa kutoisalimisha ile flash Muhimu aliyoificha kwenye chupi yake.

Dakika Moja walizungukwa kila upande “Mikono juu” ilisema sauti komavu iliyojaa hasira, ilikua ni sauti ya Brigedia Antony, kila upande walizungukwa na kikosi kazi, Hatimaye Elizabeth aliamini ameshafikia mwisho baada ya siku Tatu za Hekaheka nzito.  Endelea MSALA SEASON 3 

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Chozi liliendelea kumbubujika Elizabeth, alishakiona kifo mbele yake, mwili wa Msichana  huyu ulitweta ghafla. Alikosa nguvu, Moyoni alimwona Mzee Kimaro kama Msaliti, aliona  Mzee huyo hakupaswa kujisalimisha kirahisi vile, Uamuzi ule ndiyo ukapelekea  Makomandoo kuzidi kuwazunguka kila kona.  

Brigedia Antony alikua wa kwanza kusogea hapo akiwa na Bunduki yake mkononi,  alishachoka dharau na kebehi za Bi. Sandra, alijawa na hasira. Alilizunguka Jiwe na  kuwakuta Mzee Kimaro pamoja na Elizabeth wakiwa wameketi. Macho ya Brigedia Antony  hayakutulia, kwanza alistaajabu kumwona Msichana mwenyewe, alikua Mdogo siyo wa  kuwasunbua kwa Muda wote huo, pili ni Mtu aliyekua akimsaidia Msichana huyo,  alimtazama kama Mzee Goigoi asiyeweza lolote. 

Akachuchumaa akimkodolea macho Elizabeth, mara akaja Komandoo mmoja kabla hata  Brigedia Antony Kesi hajasema chochote. 

“Tuna maagizo ya kumchukua sasa hivi” alisema Komandoo huyo aliyemsimamia Brigedia  Antony kwa nyuma, Brigedia alipogeuka alikutana naye uso kwa uso, mazungumzo yalikua  yakifanyika kwa sauti kubwa kwasababu ya kelele ya panga boi za Helkopta zilizotanda juu. 

Brigedia Antony hakua na sauti, akasimama ili Elizabeth achukuliwe japo aliona kama  amedharaulika mbele ya wanajeshi wengine lakini alijua maelekezo hayo yalitoka Ikulu kwa  Rais, hakuna aliyekua na taarifa kua tayari Rais aliuawa. 

Makomandoo waliwaswamba Mzee Kimaro na Elizabeth ili wawaingize kwenye Helkopta,  Elizabeth akaweka ngumu baada ya kusimama mbele ya Brigedia kisha akamwambia 

“Unafanya kosa kubwa sana, utalijutia siku moja” baada ya kusema hivyo alisukumwa kwa  nguvu kuelekea kwenye Helkopta, Hatimaye Elizabeth na Mzee Kimaro walinaswa. Taarifa  ya kunaswa kwao ilifika Ikulu kwa Waziri Mkuu Haji Babi mwenye tamaa na Madaraka,  nyuso za Tabasamu ziliwajaa. 

Dakika moja, Helkopta zilianza kuondoka eneo hilo la mpaka wa Kiluvya, Uelekeo ukawa ni  Black Site kupitia Msitu wa Magoroto Mkoani Tanga, mahali ilipo Black Site ni siri nzito  sana. Mara moja wakapigwa na kupoteza fahamu ili wasijuwe wanapopelekwa. 

** 

Gari nyeusi isiyo na namba ya Usajili iliyokua ikitumiwa na Zagamba ilifika eneo la  Godauni, mshale wa saa yake ulikua ukisoma saa 11:15 Alfajiri, Dakika kadhaa baada ya 

tukio la kunaswa kwa Elizabeth. Uso wake ulijawa na Hasira sana, akaelekea kwenye  chumba alichohifadhiwa Muhonzi. 

“Unasikia wewe Mshenzi, Elizabeth amenaswa Muda mchache uliopita” alisema Zagamba  akiongea kwa hasira kisha akamwonesha video ya kunaswa kwa Elizabeth, moja ya Askari  walio eneo la tukio walimtumia video hiyo kwa siri sana. Muhonzi alishtuka sana,  alichokiona kilimduwaza, akajikuta akipepesa macho yake kama fundi saa aliyepoteza nati. 

Hakujua aseme nini, mikono yake ilifungwa kwa nyuma hivyo hakuweza hata kunyanyua  chochote. Alijitingisha lakini hakuweza hata kusogea, mara akavutwa kwa nguvu 

“Sema ni wapi ilipo M21!” Aling’aka Zagamba akilihitaji faili la siri la Rais Lucas Mbelwa,  Mara simu ya Zagamba iliita, alimkata jicho kali Muhonzi wakati anaitoa simu yake  mfukoni. Kisha aliondoka eneo hilo kwa ajili ya kuzungumza na Simu 

**  

Jua lilikua tayari limeshatua, palionekana kua na hali ya kawaida sana siku hiyo lakini  palikua na siri nzito juu ya kifo cha Rais Mbelwa, Waziri Mkuu Haji Babi na washirika wake  walifanya kikao cha siri ndani ya Ikulu, kikao hicho kilikua na ajenda kuu moja, ni jinsi gani  watafanya mapinduzi baada ya kifo cha Rais Mbelwa, kitu cha kwanza walichokipa  kipaumbele ni nyaraka M21 ambayo ilikua na siri nyingi za Rais Mbelwa na baadhi ya  viongozi wengine wa ngazi za juu akiwemo Bi. Sandra ambaye alikua Mshirika mkubwa wa  Rais Mbelwa, hata yeye Waziri Mkuu kuna siri zilikuwamo ndani ya Nyaraka hiyo kumhusu. 

Jukumu la kupatikana kwa nyaraka akakabidhiwa Bi. Sandra ambaye aliaminika kua ni Mtu  hatari sana, akaondoka Ikulu asubuhi hiyo kwa Helkopta tayari kuelekea Kitengo nyeti cha  Black Site. 

** 

Jua lilikua linawaka kwa wastani, asubuhi tulivu ilimkuta Benjamin Kingai akiwa ameketi  juu ya jiwe moja ndani ya Msitu wa Magoroto, mazingira hayo yalimfanya Benjamin ajisikie  vizuri, mbele yake palikua na bwawa dogo ambalo alikua akilitupia vijiwe vidogo vidogo  ambavyo vilikua vinatoa sauti nzuri vinapoingia ndani ya Maji. 

Mara alikuja Malkia Zandawe na kuketi kando ya Benjamin, hakua na hofu tena na Binti  huyo baada ya kuona mambo makubwa ambayo Binti huyo aliyafanya.  

“Unajisikiaje?” aliuliza Zandawe akiwa ni mwenye kutabasamu, Benjamin naye aliachia  tabasamu lisilo na uhakika wa kipi anachokifurahia, akamjibu Malkia Zandawe 

“Vizuri, nipo ndani ya Msitu wako” kisha alisindikiza kauli yake na kicheko kidogo, akatupa  tena vijiwe ndani ya bwawa. 

“Usiwe na wasiwasi Benjamin, utaondoka ndani ya Msitu muda siyo mrefu, kwasasa angalia  zaidi kuhusu hatma ya Maisha yako baada ya kutoka hapa” akasema Malkia Zandawe huku  naye akitupa vijiwe, wakaufanya huo kua ni mchezo kwao.

“Asante kwa kusaidia Maisha yangu, sijui bila kunisaidia ningekua wapi sasa hivi, pengine  ningekua nimeshauawa.” Akasema Benjamin akiwa analengwa na chozi 

“Unafikiri ni kwanini huyo Msichana alikua na hizo nyaraka? Na hizo nyaraka zinahusu nini  hasa?” akahoji Malikia Zandawe akiwa anamtolea macho zaidi Benjamin 

“Inaonekana kuna taarifa za siri sana kumhusu Rais, lakini sijui kwa hakika zaidi ni kwanini  aliziiba”  

“Basi huyo Msichana kama atakua hai basi atakua sehemu ya hatari zaidi, kwa Msako ule  sidhani kama atapata mahali pa Kujificha” akasema Malkia Zandawe 

“Lakini yule Msichana anaonekana kua zaidi ya Msichana, si Mtu wa kawaida. Ana mambo  mengi ya siri anayoyaficha, kingine ni mjuzi wa mbinu za kivita” alisema, pakawa na ukimya  wa kutosha kisha Zandawe akatupa swali lingine 

“Umewaza kuhusu Hatma ya Mtoto wako na mpenzi wako, nyuma yako kuna nini  kitawakuta?” swali hili lilimpa nyakati ngumu Benjamin, akashindwa kulizuia chozi  likamtoka likashuka hadi kwenye mashavu yake Madogo. 

“Kuwaza hatma yao ni sawa na kusema hakuna kifo, nachelea kusema pengine  wameshauawa huko waliko, roho yangu inanisuta ni kwanini niliwakimbia, nilikua mbinafsi  nikasalimisha Maisha yangu bila kuangalia ni Jambo gani litawafika” Alipoimaliza hii kauli  aliangusha kilio Benjamin, Malkia Zandawe akajawa na huzuni sana akamwambia Benjamin 

“Hata ukilia kwasasa haitokua na Msaada, kikubwa ni kujua ni wapi walipo, na je wapo hai?”  

“Kujua walipo ni jambo gumu sana, ile sehemu ni hatari, ni sehemu ya siri sana. Ni ngumu  kujua nini kimewafika, naweza kusema wameshakufa” akasema Benjamin kisha akajiinamia. 

“Nitalichunguza hilo Benjamin, subiria” akasema Malkia Zandawe kisha akatoka spidi  kuzama Msituni, Benjamin hakuelewa ni kitu gani kilimfanya Zandawe azame Msitumi kwa  kasi namna ile. 

Msichana Zandawe, alizidi kukimbia hadi alipofika eneo la Bwawa, hapo aliangaza huku na  kule, eneo hilo ndilo ambalo Benjamin alikua amejitupa Siku ile kwa lengo la kuokoa Maisha  yake kutoka juu ya Helkopta ya Kijeshi. 

Akasogea hadi chini ya Mti mmoja, hapo chini aliziona kamba ambazo alifungwa nazo  Benjamin, kisha akazichukua kamba hizo akakimbia kurudi alipomwacha Benjamin, alikua  msichana wa Msituni anayeutawala Msitu huo hatari unaowasumbua wengi 

Alifika alipomwacha Benjamin akiwa anahema sana, kisha akamwonesha Benjamin zile  kamba, haraka Benjamin akazikumbuka, akashuka kutoka juu ya jiwe hadi aliposimama  Zandawe. 

“Unataka kufanya nini?”

“Subiria uone” akasema Zandawe kisha akapiga mluzi mkali, ghafla ikasikika sauti ya ndege  mmoja akija walipo, ndege huyo alikua mweupe anayefanana na njiwa mzuri wa kufugwa,  alipofika hapo alitua juu ya jiwe ambao Benjamin alilikalia muda mchache ulio pita 

“Huyu ni rafiki yangu anaitwa Gola, ni mpelelezi mzuri anayenipa taarifa nyingi kuhusu hali  ya Msitu, nataka kumtuma” alisema Malkia Zandawe, kila alichokisema kilikua kama ndoto  kwa Benjamin, alijikuta akitabasamu. 

Mambo kama hayo aliyasoma kwenye kitabu, ni Mfalme Suleiman pekee ndiye aliyekua ana  uwezo wa kuzungumza na ndege lakini Msichana Zandawe alikua na uwezo kama ule wa  kuzungumza na ndege. 

“Umtume wapi?”  

“Huko mahala pa siri, nataka kupajua. Nataka kujua hatma ya Familia yako Benjamin”  alisema Malkia Zandawe kisha alimsogelea ndege Gola, akazungumza naye kwa lugha za  ndege kisha akampatia ile kamba kama alama ya wapi ilipo Black Site. Kisha ndege huyo  akaruka kwa spidi, akiwa ameishikilia ile kamba mguuni. 

“Gola ataleta majibu ni wapi ilipo Black Site” akasema Malkia Zandawe kisha akampa  tabasamu zito Benjamin ambaye alijawa na Bumbuwazi zito, midomo yake ikawa mizito  kiasi kwamba hakuweza kusema chochote.  Nini Kitaendelea?

Usikose sehemu ya ishirini na mbili ya MSALA SEASON 3 Kujua kama Elizabeth alipona kwenye Msala huu

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

11 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version