IlipoishiaHuko mahala pa siri, nataka kupajua. Nataka kujua hatma ya Familia yako Benjamin”  alisema Malkia Zandawe kisha alimsogelea ndege Gola, akazungumza naye kwa lugha za  ndege kisha akampatia ile kamba kama alama ya wapi ilipo Black Site. Kisha ndege huyo  akaruka kwa spidi, akiwa ameishikilia ile kamba mguuni. 

“Gola ataleta majibu ni wapi ilipo Black Site” akasema Malkia Zandawe kisha akampa  tabasamu zito Benjamin ambaye alijawa na Bumbuwazi zito, midomo yake ikawa mizito  kiasi kwamba hakuweza kusema chochote. Endelea 

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Elizabeth na Mzee Kimaro wakiwa wamepoteza fahamu waliswekwa ndani ya chumba  kimoja, walikua sakafuni wakiwa hawajitambui. Elizabeth alikua wa kwanza kugutuka  kutoka kwenye Usingizi mzito, mahali alipo hakufanikiwa kupajua lakini kwa hakika alijua  amewekwa sehemu nyeti kwa ajili ya mateso. 

“Mzee Kimaro” aliita Elizabeth huku akimtikisa Mzee Kimaro ambaye aliamka haraka baada  ya kutikiswa. Wote walistaajabu namna eneo hilo lilivyo kimya 

“Tupo wapi?” 

“Unafikiri tupo Mwambisi? Kwanini ulijisalimisha?” Bado Elizabeth alikua akijiuliza swali  hili, Mzee Kimaro akamwambia Elizabeth 

“Tungefia pale kwa mashambulizi makali Elizabeth, hatukua na silaha za kutosha za  kupambana na kikosi kile, ilikua ni sawa na kazi Bure” alisema Mzee Kimaro akiwa  anajikagua mikononi, alikua na alama nyingi za kamba. 

“Ungekamatwa wewe, Mimi nikasonga mbele, sasa sote tumenaswa ni nani atatusaidia  kutoka hapa, kama ulikua hujui hapa ndiyo tumejichimbia Kaburi, mwisho wetu ni hapa”  akazidi kusema kwa hasira na lawama Elizabeth. 

Mazungumzo yao yalikatishwa na sauti ya kufunguliwa kwa mlango wa chumba hicho, kila  mmoja alipeleka macho yake mlangoni kuona ni Nani aliyekua akiufungua mlango huo,  tokea wamefika hapo hawakupata kumwona Mtu yeyote wala kusikia sauti yeyote ile.

Wote macho yao yalimwona Mwanamke wa shoka, Bi. Sandra akiwa amevalia gauni refu  jekundu, wakajikuta wakimdadisi Mwanamke huyo aliyegoma kuzeeka kabisa, kwanza  alikua akitabasamu huku akitembea kwa madaha kama anashiriki shindano la kusaka  walimbwende.  

Mwisho alisimama karibu nao, kisha akachuchumaa, kwa sauti ya mapozi iliyojaa kebehi  nzito akawasalimia 

“Hatimaye tumeonana marafiki zangu, natumaini mmeyapenda makazi yenu mapya”  alipomaliza kusema alijikung’uta vunbi kama vile alikua ameingia stoo ya vyakula, akaagiza  kitambaa ili ajifute vizuri kisha akawaambia 

“Hapa mlipo siyo sehemu nzuri, mtapata mafua. Nyinyi ni wageni muhimu sana hapa hivyo  hampaswi kua hapa, oooh! Sijui ni nani aliyewaweka hapa, naomba tafadhali muwatoe hapa”  akasema kwa kebehi kisha mwisho akamalizia kwa kuikaza sauti yake. 

Halafu yeye akatangulia mbele wakati huo walinzi wakiwatoa akina Elizabeth ndani ya  chumba hicho, wakaingizwa kwenye chumba kimoja chenye visima vidogo viwili katikati,  minyororo mikubwa ikiwa inaning’inia kwenye kila kisima. 

“Hebu waweke wanapostahili” akasema Bi. Sandra huku akiwa anaketi kwenye kiti, chunba  hicho kilionekana kua ni chumba cha mateso kwa namna ambavyo vitu vilikua  shaghalabaghala tena pakionekana kua ni eneo hatari sana 

Michirizi ya damu ilikua imetapakaa kila kona ya chumba hicho, nyoyo za digidigi hawa  wawili zilianza kwenda mrama, wakafungwa minyororo mikononi kisha wakatoswa ndani ya  visima, kila mmoja akatoswa kwenye kisima chake. 

Visima vya duara vilivyojengwa kwa mawe, havikua visima virefu sana lakini vilitosha  kuwatesa, maji yakafunguliwa kisha yakaanza kujaa ndani yake, taratibu walianza kujikuta  wakianza kutapatapa. Kisha Bi. Sandra na walinzi wengine wakatoka ndani ya chumba hicho,  minyororo haikuwapa nafasi ya kufanya chochote tena kibaya walifungwa kwa nyuma. 

Bi. Sandra akaagiza kahawa na kuketi nje ya jengo la Black Site akiwa anautazama msitu  ulioizunguka kambi hiyo ya siri, macho yake yakatua kwenye Mti mmoja, mti huo ulikua  mrefu kiasi na ulikua karibu zaidi na jengo hilo lililojengwa kwa kiasi kikubwa na vioo  vigumu. 

Alikua akimtazama ndege mmoja mkubwa mweupe, ndege huyo alikua na kamba miguuni,  alitabasamu kumwona ndege huyo ambaye baada ya muda mfupi aliruka. Namna alivyoruka  ilimpa tabasamu Bi. Sandra, ndege huyo alikua ni Gola. 

Ndege aliyetumwa na Malkia Zandawe kwa lemgo la kuichunguza Black site, kwanza kujua  mahali ilipo sehemu hiyo nyeti ambayo Benjamin alimwacha Mpenzi wake, kisha Bi. Sandra  akarejea ndani hadi kwenye chumba cha mateso. 

Mzee Kimaro alikua akielea tu ndani ya kisima hicho, ueleaji wake uliashiri Mzee huyo  alikua tayari amefariki kutokana na maji kumzonga, uzee wake haukumfanya awe na nguvu  ya kukabiliana na adhabu hiyo, kisha akakitazama kisima cha pili, bado Elizabeth alikua  akihangaika namna ya kujinasua na mtego huo wa kifo.

“Ooh masikini, Mzee wako ameshindwa kuhimili, yeye ameaga mashindano mapema sana.  Namtakia mapumziko mema” alisema huku Walinzi wakiutoa mwili wa Mzee Kimaro  kutoka ndani ya Maji. Akaagiza pia Elizabeth atolewe ndani ya maji, kisha akaangalia saa  yake na kuona alitumia dakika kumi na tano kuwaacha wawili hao ndani ya maji. 

Elizabeth alikua amechoka vibaya mno, maji yalikua yakimvuja. Kisha akakalishwa juu ya  kiti kimoja cha chuma. Alikua amelegea sana, Masikini alikua akitapika maji mengi  aliyoyanywa. Mwili wa Mzee Kimaro ulitiwa ndani ya mfuko maalum kisha walinzi hao  waliondoka na mwili wa Mzee kimaro wakaupeleka hadi ndani ya chumba kimoja. 

Wakautia mwili huo kwenye moto mkali uliokua ndani ya Pipa moja kubwa, wakaufunika  humo ili kuupoteza mwili na mabaki yake, Maisha ya Mzee Kimaro yakaishia ndani ya  Kitengo hicho cha Siri kilicho ndani ya Msitu mmoja. 

“Elizabeth, najua unajua ni kwanini upo hapa, sasa tafadhali usije ukanisumbua. Nipatie M21  na utando wote unaohusiana na M21” alisema Bi. Sandra, hata sura ya Mama huyu  ilibadilika, alinyoosha mkono wake ili apatiwe M21. Elizabeth alipokua katika Dudumizi la  maji mazito yenye mateso, ndani ya kile kisima alikutana na Malaika Mtoa roho, kisima kile  kilikua ni zaidi ya shimo refu lenye moto mkali unaowaka bila kupunguza makali, bado  masikio yake yalisikia zaidi sauti za Maji yaliyomtesa 

“Unanisikia?” akafoka Bi. Sandra, akaitoa sauti yake kali aliyokua akiificha muda wote, sauti  iliyopasua ngoma za Masikio ya Elizabeth. Kisha Bi. Sandra akamwambia Elizabeth 

“Vita vyote umevipigana ukiwa ndani ya hilo dela? Najiuliza mengi yasiyo na majibu kuhusu  wewe, ni Jasusi kutokea wapi?” Bi. Sandra akazidi kumchimba Elizabeth lakini ukimya wake  ulimjaza hasira akampa kibao kikali kilichomkwarua shavu lake la kulia kwa pete ya Bi.  Sandra. Damu nzito ikamvuja mdomoni Elizabeth, kwa hasira akamtusi Bi. Sandra 

“Malaya wewe” alisema kwa hasira sana, haraka Bi. Sandra akaagiza Elizabeth ateswe zaidi  ndani ya Jengo hilo la siri. Mateso Makali yalimfanya apige ukunga ambao uliwafanya ndege  walio karibu na Jengo hilo kuruka. 

** 

Mwili wa Rais Mbelwa ukawekwa kwenye Jokofu ndani ya eneo lake la siri la mateso, bado  siri ya kifo cha Rais ikabaki Ikulu, hakuna Mtu aliye nje ya Ikulu aliyeifahamu siri hiyo, hata  viongozi wengine wakubwa wa Serikali hawakuweza kuitambua siri hiyo, walinzi wote  waliokua wakiilinda Ikulu waliondolewa, Waziri Mkuu Haji Babi akaweka walinzi wapya  kutoka Kitengo cha Black Site. 

Upande wa pili, Muhonzi alikua akiteseka ndani ya Godauni, Zagamba alimshikilia ili aipate  Nyaraka M21 kutoka kwa Elizabeth, Alikua ndani ya chumba kimoja chenye dirisha dogo  tena liko juu sana, hewa ilikua nzito lakini kibaya zaidi alipaswa kujisaidia ndani ya Chumba  hicho, Mikono yake ilifungwa kamba ili asifanye ujanja wowote ule. 

Akili yake ilishashtuka mapema kua kuna lililompata Elizabeth ndiyo maana Zagamba alikua  mwenye hasira sana, tumaini la yeye kuendelea kua hai aliliona kua finyu kabisa, akaanza  kutafuta namna ya kujisaidia hapo ili aweze kuokoa uhai wake.

Kabla hajafanya chochote akakumbuka tukio moja… Ni Tukio Gani? Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

12 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version