Baada ya kutolewa kwa timu ya taifa ya Senegal na wenyeji Ivory Coast kwa sasa timu ya taifa ya Morocco inapewa chapuo kubwa la kuwa mabingwa wa michuano hii ambayo mpaka sasa imekua migumu kutokana na kutokea kwa matokeo ambayo hayajawahi kufikiriwa kabisa.

DONDOO:

Katika mechi za hatua ya makundi Morocco wamefanikiwa kushinda michezo 2 ambao ni dhidi ya Tanzania kwa bao 4:0 na dhidi ya Zambia kwa 1:0 huku wakisare na DR Congo kwa bao 1:1 huku South Africa wao wamepoteza mchezo mmoja dhidi ya Mali kwa bao 2:0, wakishinda kwa kumfunga Namibia bao 4:0 huku wakisare dhidi ya Tunisia 0:0.

TAKWIMU:

  • Katika michezo 9 ambayo imewakutanisha ni kuwa Morocco ameshinda michezo 3 huku South Africa akishinda michezo 3 na kupatikana sare 3 kwahiyo mpaka sasa anatafutwa mbabe kati yao.
  • Mara ya mwisho kukutana ni mchezo wa kufuzu AFCON hii ya nchini Ivory Coast ambapo South Africa alishinda katika ardhi ya nyumbani kwa bao 2:1 ilikua Juni 2023.
  • Morocco wametinga hatua ya robo fainali katika mechi zao mbili kati ya 3 zilizopita za AFCON
  • South Africa imeshinda michezo mitatu pekee kati ya 13 iliyopita ya michuano ya AFCON huku wakipoteza michezo 7.

TUNABETIJE?

  1. Morocco anapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda mchezo huu kutokana na ukubwa wao walionao ingawa kama kawaida AFCON msimu huu imekua na matokeo ya kushangaza kwelikweli.
  2. Mechi hii sitegemei timu zote mbili kufungana (Both Team to score NO)
  3. Kwa wale wanaopenda kubetia kuhusu magoli unaweza kuweka kipindi cha kwanza kusiwe na magoli zaidi ya 3 kipindi cha kwanza (1st Half Under 2.5 Goals).

SOMA ZAIDI: Mali vs Burkina Faso tunausuka hivi mkeka.

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Nottingham Forest vs Arsenal Takwimu Na Dondoo Za Mkeka - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version