Mara baada ya kuwa nchi ya kwanza ya kiarabu ikiliwakilisha bara la Afrika kutinga hatua ya nusu fainali kombe la dunia baada ya kuwa na mwendo wa kusisimua iliyoshika vichwa vya soka duniani, Morocco kwa sasa wanatakiwa kuonesha kuwa hawakufika hatua ya nusu fainali kombe la dunia kwa bahati mbaya na kwa sasa wanatakiwa kufua rekodi ya kushindwa mara kwa mara.

Presha kubwa waliyonayo kwa sasa ni kuonesha wana kitu gani wamekiandaa katika michuano hii ya AFCON inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Ivory Coast Jumamosi hii baada ya kupita takribani miezi 12 toka kufika kwao hatua ya nusu fainali kombe la dunia lilofanyika nchini Qatar.

Wakati wa maandalizi ya michuano hii ya AFCON kocha mkuu wa timu ya taifa ya Morocco Walid Regragui, alisema kuwa kufika kwao hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia imewafundisha namna bora ya kucheza michuano mikubwa japokua michuano ya mataifa barani Afrika mara nyingi kwao huwa ni migumu kila mara wanaposhiriki.

Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya Morocco kushiriki michuano hii na kupewa kipaumbele kikubwa cha kuibuka mabingwa wa michuano hii lakini siku zote AFCON sio michuano ambayo unaweza Kwenda na matarajio yako kwani huwa kuna mambi ambayo hayatabiriki.

Changamoto Kubwa Kwa Morocco Ni Ipi?

Kwa ubora mkubwa ambao wameuonesha katika michuano ya kombe la dunia ni wazi kuwa timu nyingi zitataka kuwaonesha kuwa wao wana uwezo pia lakini pia kuwashusha chini kwani wanatarajiwa kukutana na changamoto kubwa kutoka kwa wenyeji Ivory Coast lakini pia Ghana, Nigeria na mabingwa watetezi ambao ni Senegal.

Katika michuano ya msimu uliopita walitabiriwa sana kuwa mabingwa lakini wakaja kutolewa na Misri katika hatua ya penati ambapo Senegal aliibuka bingwa pia kwa kumfunga Misri kwa penati.

Njia ngumu pia kwa Morocco itakua kukutana na wenyeji Ivory Coast kwani watakua na nguvu kubwa ya mashabiki kutoka ardhi ya nyumbani ambao watakuwepo huku Morocco wao kama kawaida yao wakiwa na mashabiki ambao watakua wamesafiri kutoka nchini Morocco licha ya kwamba timu ya mwisho kuchukua ubingwa wa AFCON wakiwa katika ardhi ya nyumbani ni Misri.

Uwepo wa timu ya taifa ya Nigeria ambayo katika makaratasi unaweza kusema kuwa ni moja kati ya timu bora pia miongoni mwa zile ambazo zimefuzu katika michuano ya mwaka huu ukizingatia pia na kiwango bora walichokionesha katika mechi zao zilizopita.

Mabingwa Waliopita Wanatisha Nao

Ukizungumzia mabingwa wa AFCON kwa misimu kadhaa iliyopita basi huwezi kuacha kuwataja kama Cameroon, Demokrasia ya Kongo, Afrika Kusini na Zambia. Uwepo wa timu hizi ni presha kwa Morocco kufanya vyema katika michuano hii kwani nao wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa huu kama ambavyo walifanya.

Msimu huu wa AFCON Kumekuwa na msisitizo mkubwa juu ya hali ya viwanja ambavyo viliharibu mashindano yaliyopita huku wataalamu wakisafirishwa kutoka Ufaransa kusaidia kuhakikisha maeneo ya juu ya kuchezea yanakua katika ubora wa hali ya juu.

Moja ya tukio kubwa zaidi ambalo lilifanyika katika sekta ya michezo nchini Ivory Coast kabla ya kuanza kwa michuano hii ni kuwa maafisa kadhaa wakuu wa serikali walifutwa kazi mwezi Septemba baada ya mechi ya kirafiki kati ya Ivory Coast na Mali kulazimika kuachwa kwa sababu ya uwanja uliojaa maji katika uwanja mpya wa Stade Olympique Alassane Ouattara katika kitongoji cha Abidjan Ebimpe. Ikumbukwe kuwa huu ni uwanja ambao maonesho ya ufunguzi wa AFCON yatafanyika lakini pia na mchezo wa fainali utachezwa hapo pia.

Awali michuano hii ilipangwa kufanyika Juni mwaka jana lakini ikarejeshwa kwa miezi sita kutokana na hofu ya athari za msimu wa mvua na sasa inaangukia tena katikati ya msimu wa ligi barani Ulaya, hali inayowashangaza makocha wengi.

Kwa namna maandalizi na kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kilivyo mpaka sasa unaona nafasi yoyote ile ya wao kufanya vizuri katika michuano ya AFCON ya mwaka huu nchini Ivory Coast?

Endelea kusoma taarifa mbalimbali kuhusu AFCON kwa kubonyeza hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version