Kuelekea hamasa za mchezo wa makundi klabu bingwa barani Afrika utakaowakutanisha klabu ya  Simba dhidi ya Wydad kutoka Morocco Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kuwa Katika uzinduzi kutakuwa na burudani nyingi kutoka kwa King Faida, Doto na balaa kubwa zaidi litasindikizwa na Miso Misondo.

Ahmed amesema kuwa wana mpango wa kufanya hamasa kubwa ambayo haijawahi kutokea na uzindui wake utafanyika tarehe 16 Disemba Mbagala Zakhiem na msafara utaanzia uwanja wa mkapa na magari. “Tuna mpango wa kufanya hamasa kubwa ambayo haijawahi kutokea. Uzinduzi utafanyika tarehe 16 Desemba, 2023 eneo ni Mbagala Zakhem. Msafara utaanzia Uwanja wa Mkapa na magari.

Kuhusu Miso Misondo, Ahmed anasema kuwa wamemchukua yeye Pamoja na madansa wake , “Jumamosi naomba Wanasimba mjitokeze kwa wingi mje mpate show ya Miso Misondo. Wale wazee wa kucheza hiyo siku mtawaona vizuri na Ijumaa tutaachia remix kwa ajili ya Simba.

Aidha Miso Misondo ameishukuru klabu ya Simba kwa kumpa nafasi kwani alikua anatamani kufanya kazi na klabu hiyo Naishukuru Simba kwa kunipa nafasi hii, nilikuwa natamani siku moja kufanya kazi na klabu hii.”

Endelea kusoma kuhusu taarifa mbalimbali za michezo na makala kwa kugusa hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version