Hakika Siku Imewadia!

Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Leo Machi 24, 2023 itashuka dimbani Kuwakabili Timu ya Taifa ya Uganda, ‘The Cranes’ ambao utapigwa nchini Misri kwa ajili ya Kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayofanyika mwakani Nchini Ivory Coast.

Taifa Stars inahitaji ushindi siku ya leo ili kujiweka katika nafasi nzuri na yenye Matumaini Hai akiwa katika Kundi F la Michuano hiyo kabla ya Mchezo wa marudiano utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 28, 2023. Kwa sasa Taifa stars inahitaji ushindi katika mechi zote mbili dhidi ya uganda ili kufuzu, huku ikiiombea njaa Niger kupoteza Mchezo wao ujao dhidi ya Algeria.

Stars inashika nafasi ya tatu katika kundi F ikiwa na pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Niger mchezo uliopigwa nchini Niger huku mechi ya pili ikipoteza 2-0 na Algeria kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kwa upande wa Uganda ina pointi moja pia baada ya kucheza michezo miwili ambapo kati ya hiyo imetoa sare mmoja na kupoteza mmoja wakati Algeria ndio kinara na pointi sita ikifuatiwa na Niger yenye pointi mbili.

Taifa Stars leo inaingia katika mchezo huu ikiwa na kocha Mpya, Kocha Mkuu Mbelgiji, Adel Amrouche mwenye asili ya Algeria huku Watanzania wengi wakiwa na imani ya kusonga mbele chini ya kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika.

Sasa unajua Shuguli yenyewe iko wapi?

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dk. Pindi Chana ameeleza kuwa Serikali itatoa Shilingi milioni 500 kwa timu ya Taifa ikiwa itafuzu kucheza fainali za mashindano ya AFCON 2023.

Waziri Chana alieleza kuwa serikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa inawaunga mkono Timu ya Taifa ili kufanya vyema kwenye mashindano ya Kimataifa.

Mheshimiwa Waziri aliwataka pia mashabiki waweze kuiunga mkono na kuisapoti timu ya taifa na hata kufika kwa wingi kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Machi 28.

Stars itaumana dhidi ya The Cranes, mchezo utakaochezwa katika uwanja uliopo mji wa Ismailia, Saa 11:00 Jioni.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply


Exit mobile version