UEFA EURO ni moja ya michuano mikubwa sana barani Ulaya inayohusisha timu za taifa ambayo inafanyika kila baada ya miaka minne (4), michuano hii ina historia kubwa sana na lukuki ndani ya bara kwnye kila aina ya vifaa na kila rasilimali inayohitajika michezo viwanja bora na vifaa vya mazoezi ni sehemu tu.

Kumbukumbu bora ya michuano hii ilianza kwenye  Karen ya nyuma kabisa huko na mpaka sasa imeshashuhudia mabingwa 11 tofauti ndani ya mataji 17, huku timu za taifa ya Ujerumani pamoja na Spain zikiwa vinara wa kuchukua kombe ilo mara nyingi zaidi ambapo kwa pamoja kila mmoja amechukua mara 3 tu.

Italia na Ufaransa yanafuata kwa kila mmoja kuchukua mara 2 ambapo Italia alichukua mwaka 1968 akimfunga Yugoslavia 2-0 na 2020 akimfunga England kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1, huku kwa upande wa Ufaransa akifanya hivyo mwaka 1984 akimbamiza Uhispania 2-0 na 2000 akimfunga Italia 2-1.

Mataifa ya Uholanzi, Czech, Russia, Greece, Denmark na Ureno wote kwa pamoja wakichukua mara moja kwa kila taifa ambapo, Russia aliibuka bingwa 1960 kipindi ikiwa inajulikana kama USSR 2-1 dhidi ya Yugoslavia,

Hata hivyo kikosi cha Czech alishinda akimfunga West Germany  kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2, mwaka 1988 akifanya hivyo Uholanzi kwa ushindi wa 0-2 dhidi ya USSR, Denmark mwaka 1992 akimfunga Ujerumani 2-0, hata hivyo Greece akichukua mwaka 2004 kwa kumshushia kipigo cha goli 1-0 timu ya taifa ya Ureno na Taifa la mwisho linalomiliki kombe ilo mara moja ni taifa la Ureno lililoshinda mwaka 2016 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Ufaransa.

Ukubwa ni dawa na ndiyo maana timu za taifa za Hispania pamoja na Ujerumani ni mabingwa mara nyingi wa michuano hiyo kwa kila taifa kushinda mara 3 kwa kila taifa.

Ujerumani alichukua mwaka 1972 akimfunga USSR 3-0, 1980 akimfunga Ubelgiji 2-1 na mwaka 1996 akimbamiza Czech 2-1. Huku upande wa Hispania akifanya hivyo mwaka 1964 baada ya kumfunga USSR 2-1, 2008 akimfunga Ujerumani 1-0 na mwaka 2012 akimbamiza Italia goli 4-0.

 

Timu inayoongoza kuingia fainali mara nyingi zaidi ni timu ya taifa ya Ujerumani ikifanya hivyo mara 6 ambapo ni mwaka 1972, 1976, 1980, 1992, 1996 na 2008 huku akifatiwa na Hispania ambaye ameingia fainali 4 ambazo ni mwaka 1964, 1984, 2008 na 2012 pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa ambayo imeingia fainali mara tatu 1984, 2000 na mwaka 2016.

Mpaka sasa timu zilizochukua mara nyingi zipo kwenye michuano hiyo ambayo kwa mwaka huu inafanyika nchini Ujerumani.

Upande wa wafungaji bora mpaka sasa anaongoza Cristiano Ronaldo wa Ureno ambaye amefunga jumla ya magoli 14, akifatiwa na Michel Platini wa Ufaransa ambaye aliwahi kuwa Raisi wa FIFA akifunga magoli 9, na watatu ni Antoine Griezman wa Ufaransa ambaye ana magoli 7 huku Alvaro Morata na Romero Lukaku wote wakiwa na magoli 6.

Orodha hiyo ya wafungaji bora ni Cristiano Ronaldo, Antoine Griezman, Alvaro Morata pamoja na Romero Lukaku wana uwezo wa kuongeza magoli hayo kwani ni sehemu ya Vikosi vya mataifa yao kwenye mashindano ya Mwaka huu.

SOMA ZAIDI: Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

1 Comment

  1. Pingback: Ratiba Kamili Ya EPL 2024/2025 Hii Hapa

Leave A Reply


Exit mobile version