Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Nigeria Asisat Oshoala ameshinda tuzo ya Mchezaji wa Mwaka wa Wanawake wa CAF 2023 kwa kuweka rekodi ya kushinda tuzo hiyo mara ya sita baada ya kuwashinda Thembi Kgathlana (Afrika Kusini) na Barbara Banda (Zambia) katika tuzo hizo.
Oshoala alikuwa na mwaka bora kwa Super Falcons kwenye Kombe la Dunia la Wanawake FIFA 2023, ambapo alifunga bao la ushindi wakati mabingwa wa Afrika mara tisa Nigeria walipowafunga Australia 3-2 kwenye mchezo wa pili wa Kundi A, Ushindi uliokuwa muhimu katika kuhakikisha wanaingia hatua ya 16 bora kwenye mashindano hayo.
Alicheza pia kwa mafanikio na FC Barcelona wakishinda ubingwa wa Europa ikiwa ni taji lao la pili la Ligi ya Wanawake ya UEFA lakini pia akishinda taji la ligi na timu hiyo akifunga mabao 21 katika michezo 28, mabao mengi zaidi kuliko msimu uliopita.
Tuzo hiyo aliyoshinda ya Mchezaji bora wa Wanawake wa CAF ni ya sita na kuendelea kumuacha kwa mbali Perpetua Nkwocha ambaye ameshinda tuzo hiyo mara nne.
Wengine walioshinda tuzo za Shirikisho la soka barani Africa ni hawa hapa.