Tarehe 15 mwezi wa Aprili 1452 kwenye viunga vya kitongoji cha Anchiano ndani ya nchi ya Italia alizaliwa Mwanasayansi,Injinia na mchoraji nguli aliyepewa jina na wazazi wake la Leonardo Di Ser Da Vinci, huyu ni moja ya mtu ambaye alikuja kufanya tukio kubwa sana ndio kati ya mwaka 1503 mpaka 1506. 

Da Vinci alituletea mchoro maarufu sana na ghali ambao ulijulikana kama Monalisa, mchoro ambao umeshika rekodi nyingi toka nyakati hizo mpaka sasa japo mchoro huo ulikuwa na asili ya Italia lakini kwa sasa unamilikiwa na serikali ya Ufaransa.

Monalisa ni mchoro ambao umeendelea kushika rekodi nyingi na kulindwa kwa gharama kubwa sana na kuvunja rekodi mbali mbali na mpaka sasa hapajatokea mchoro kama huo wa Da Vinci duniani karne japo ya kupita kwa karne na karne lakini umeendelea kubaki hapo ulipo. 

Wakati mwaka 1503 Da Vinci anatutengenezea mchoro wenye gharama miaka zaidi ya 480 baadae M/Mungu alituletea Lionel Messi ambaye ni moja ya kazi kubwa ya sanaa iliofanywa na M/Mungu kwenye Dunia huyu ni moja ya kazi ambayo M/Mungu aliifanya ili kuburudisha wanadamu wake.

Siku ya 24 ndani ya mwezi wa sita ya mwaka 1987 kwenye viunga vya mji mdogo wakati huo wa Rosario ndani ya nchi ya wahuni na wauza ngada wa kusini mwa Amerika yaani Argentina, kama ilivyo kwa mchoro wa ajabu wa Da Vinci ndivyo Mungu alivyotupa Lionel Messi mtu mfupi aliyekuwa na tatizo la kukua na kuhitaji gharama za kukua zitoke hospitali lakini hapa Mungu alitaka kututhibitishia uwezo wake bora kwenye kuumba. Messi alikuwa mfupi haswa na huenda dunia isingeweza kuamini kile ilichokuja kuona kwenye miguu yake kwa umbo lake lakini tukumbuke kuwa M/Mungu alikuwa kashakamilisha mchoro wake ghali kwenye umbo la mfalme Leo Messi. 

Messi ametupa burudani kwa zaidi ya miaka 15 akitupa ngono ya soka na tukaendelea kuiba muda kwenda kuangalia ngono yake, Messi aliuita mpira na mpira ukaitika, ukafanya anachotaka, kwenye miguu yake tuliwatukana sana mabeki wetu bora na kuwadharau, nani asiyejua ubora wa Sergio Ramos, John Terry, Thiago Silva, Maicon, Cannavaro, Roberto Carlos, na wengine wengi lakini messi aliwalaza na viatu, nani asiyejua kimo kikubwa cha Vidic na Rio pale United Lakini messi alipiga kichwa katikati yao, huyu ndio Monalisa aliyevunja rekodi na kuweka zake ngumu.

Huyu ni binadamu wa kwanza kuwa mchezaji bora wa mechi kwenye mechi za kombe la dunia 5 mfululizo, binadamu pekee ambaye aliweza kukupa uwiano sawa wa kufunga na kutoa pasi za magoli, nani ameisahau MSN pamoja na kuwapikia magoli mengi lakini bado Messi alikuwa kwenye nafasi ya mfungaji bora namba 2 nyuma ya mhuni Suarez. 

Messi anaondoka siku zake za kucheza soka zinakimbia kwa kasi kutoka soka la ushindani Ulaya hadi kwenda Marekani, Messi amemaliza lakini bado atabaki kuwa Monalisa kama ambavyo picha ya Monalisa ilivyoweka mlima mkubwa kwa picha nyingine kuvunja rekodi za dunia dhidi yake ndivyo hivyo hivyo Messi alivyoweka mlima mkubwa wa vijana wa kisasa kufikia rekodi zake, makombe 34 ngazi ya klabu, ikiwa na UEFA 4, Kombe la bara 1, na kombe moja la Dunia huku akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 8 zaidi messi amewaachia homework nzito vijana, kama ambavyo mona lisa imeendelea kuwa picha pora ya muda wote ndivyo ambavyo messi atabaki kuwa mchezaji bora muda wote kwa nyakati nyingi zijazo.

SOMA ZAIDI: Michezo Hatari Zaidi Duniani

1 Comment

  1. Pingback: Msimshangae Mwakinyo Yuko Sahihi Katika Maisha Ya Ndondi - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version