Lionel Messi amefunga magoli 10 katika michezo minane kwa niaba ya Inter Miami na alifunga penalti yake walipoibuka washindi katika matuta kwa mara ya pili ndani ya siku nne
Inter Miami walitoka nyuma kwa magoli 2-0 na kufika fainali yao ya pili tangu Lionel Messi ajiunge na timu ya MLS mwezi uliopita.

Mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 36, alitoa pasi mbili katika nusu fainali ya kusisimua ya Kombe la US Open dhidi ya FC Cincinnati, ambayo ilimalizika kwa sare ya 3-3 baada ya muda wa ziada.

Ilikuwa mara ya kwanza Messi kutofunga goli kwa niaba ya Miami, katika mchezo wake wa nane akiwa na klabu hiyo, lakini alifunga penalti yake walipoibuka washindi kwa mikwaju ya penalti 5-4 huko Ohio.

Miami pia iliwashinda Nashville kwa mikwaju ya penalti na kutwaa Kombe la Leagues Jumamosi iliyopita.

Hiyo ilikuwa heshima kubwa ya klabu tangu kuundwa kwake kama timu mpya mwaka 2020.

Sasa watashiriki mara ya kwanza katika fainali ya Kombe la US Open, mashindano ya soka ya kuvutia ya kuondoa timu, ambayo yalianza tangu mwaka 1913.

Miami itakuwa mwenyeji wa Houston Dynamo mnamo tarehe 27 Septemba baada ya Dynamo kuiangusha Real Salt Lake 3-1 baada ya muda wa ziada.

Cincinnati walikuwa kileleni mwa msimamo wa MLS wakati msimu ulisimama kwa ajili ya Kombe la Leagues mwezi Julai huku Miami ikiwa chini kabisa.

Lakini Miami haijapoteza mchezo wowote katika michezo minane tangu kusajili Messi na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona, Sergio Busquets na Jordi Alba.

Cincinnati waliongoza 2-0 wakati zilipobakia dakika 22 baada ya magoli kutoka kwa Luciano Acosta na Brandon Vazquez kabla Messi hajatoa michezo miwili ya juu kichwa kwa mshambuliaji wa Ecuador Leonardo Campana aliyefunga kwa vichwa – bao la kusawazisha likifungwa katika dakika za mwisho za muda wa ziada.

Josef Martinez aliiweka Miami ya Gerardo Martino mbele mapema katika muda wa ziada kutokana na pasi ya Benjamin Cremaschi, kabla ya Yuya Kubo kufanya iwe 3-3 dakika ya 114.

Katika matuta huku ikisawazishwa 4-4, kipa wa Miami Drake Callender aliokoa penalti ya Nick Hagglund kabla ya Cremaschi aliyezaliwa Miami, mwenye miaka 18, kufunga penalti ya uamuzi.

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version