Tuko katika kipindi ambacho ligi mbalimbali duniani zinaelekea ukingoni huku zipo ligi ambazo mabingwa tayari wamekwishajulikana lakini zipo ligi ambazo mabingwa bado hawajajulikana na ndio kipindi ambacho mchezaji au wachezaji hujituma kuhakikisha kuwa wanaipa mafanikio klabu ambayo wanaichezea.

Hivi sasa tupo ukingoni kabisa mwa ligi lakini pia ndio kipindi ambacho timu zinafikiria namna ya kuboresha vikosi vyao kulekea msimu mpya unaofata katika kuhakikisha kuwa wanatekeleza malengo yao ambayo unaweza kukuta katika msimu husika wameshindwa kuyatekeleza au wameyatekeleza lakini wanataka kuboresha zaidi.

Hiki ndio kipindi ambacho pia kumekua na tetesi nyingi sana kuhusiana na mchezaji au wachezaji ambao wanakua wamemaliza mikataba yao au inakaribia kuisha lakini pia ndio kipindi ambacho kumekua na tetesi kuhusiana na klabu ambazo zimekua zikiwahitaji wachezaji flani huku kukiwa na taarifa mchezaji huyu anaenda timu gani.

Swali langu ni dogo sana kwako mwana KIJIWENI kutokana na tetesi ambazo umekua ukizisikia lakini pia kuhusu mchezaji ambae yupo katika timu ambayo wewe unaishabikia unadhani kwenye timu yako mchezaji gani akiondoka kwako fresh tu na wala haina shida na akiondoka katika timu yako akaenda kwenye timu ambayo huikubali yaani huishabikii bado utaendelea kumsapoti mchezaji huyo?

Lakini pia ukipata nafasi ya kuongea na uongozi wa timu yako utatamani nani asajiliwe?

Unapenda SIMULIZI? Gusa Hapa Sasa Kusoma KOTI JEUSI   

23 Comments

  1. mlekwa sungwa on

    Kwa yanga ni metacha
    (Alaf bwana Admin pandisha mzigo wa koti jeusi mate yametutoka hukuu😂😂)

  2. Daniel cupa official on

    Kama mwana Yanga
    : ~lomalisa
    : ~mwamyeto

    Hao umri usha kataa kwa sasa , ila wengine wabaki maana watacha pengo

  3. Achana na habari za wachezaji bhana sisi inatuuma alivyoondoka agent daudi mbaga bhana fanya kweli admin

  4. Wachezaji kinda kama nkane wapelekwe Kwa mkopo timu nyingine ili wapate nafas ya kuonesha kiwango chao admin

  5. Kwa yanga aondoke metacha na lomalsa lakn wasajili kiuongo mkabaji,full back wa kushoto n mshambuliaji mmoja

  6. Mm kama shabiki wa yanga mwamnyeto na metacha sioni sababu yao kubaki kwenye timu kwan hawana pengo kwenye timu

  7. Kwa yanga mm naona aondoke pacome na 😋 na kwa simba naona aondoke clatous chama😁 …fresh tu mwanetuu

Leave A Reply


Exit mobile version