Kumekua na maandiko mengi mtandaoni haswa baada ya kile ambacho amekiandika mchezaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya DR Congo na klabu ya Pyramids kutoka nchini Misri Fiston Kalala Mayele,haswa kuhusu namna ambavyo amekua akipokea kauli za matusi kutoka kwa mashabiki wa soka wa Tanzania na akaja wazi na kusema kuwa anawafahamu kuwa wenye hiyo tabia ni mashabiki wa klabu ya Yanga.

Utakua unajiuliza kama mimi kwanini inafikia hivyo na mpaka anawasema mashabiki ambao wamempa heshima na thamani kubwa baada ya mafanikio makubwa ambayo klabu ya Yanga imeyapata hivi karibuni ikichagizwa na kiwango chake kikubwa ambacho amekionesha na kuisaidia klabu hii.

Kuna jambo ambalo ngoja niliweke wazi na nadhani ni kwamba bado Mayele hajakijua kuhusu mpira wa bongo ni kuwa siku zote ukiondoka katika ligi ya Tanzania usianze mbwembwe hazisaidii kitu wewe fanya kazi yako ukimaliza umepata timu nyingine nenda kafanye kazi huko pia kama ambavyo ulikua ukifanya ukiwa Tanzania.

Mashabiki wa soka bongo wanajua kukuza na kuwafanya wachezaji mastaa na jambo kama hili Mayele amelipata kwahiyo ni wakati wake sasa kuvumilia kwa kile ambacho alikua akipitia kuliko kukiweka mtandaoni na kuzua taharuki kwangu mimi nimemuona mchezaji wa kwanza kufanya hivyo na hii ni kuwakosea heshima mashabiki wa klabu iliyokutambulisha vyema alipo sasa.

Kuna kitu kinaitwa laana ya ligi kuu, mchezaji akishapita bongo hakuna namna anaweza kutoboa ligi nyingine Afrika na sababu ni moja tu, hype na heshima anayopewa na mashabiki wa klabu mbili za Kariakoo haipo sehemu yoyote. Mayele awaige Chama na Miquissone arudi nyumbani Inawezekana kuna watu wamemjaza maneno ya fitna kwa siku nyingi leo ndio kaamua kulipuka

SOMA ZAIDI:Ligi Kuu Imerejea Marefa Kuweni Na Msimamo

2 Comments

  1. Pingback: Ningeshangaa Sana Kama Simba Wasingeshinda - Kijiweni

  2. Pingback: Ahsante John Bocco Umeiona Fursa Kwa Soka La Tanzania - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version