Mchezo wa kufuzu kwa Euro 2024 kati ya Ubelgiji na Sweden uliokua katika hatua ya kwanza ulisitishwa wakati wa mapumziko kwa sababu za usalama baada ya watu wawili wa Sweden kuuawa kwa kupigwa risasi mjini Brussels.

Mauaji hayo yalitokea muda mfupi kabla ya mchezo na sasa yanachunguzwa kama kitendo cha ugaidi.

Uamuzi wa kusitisha mchezo ulithibitishwa saa 21:30 BST.

Huku mshambuliaji akiwa bado hajapatikana, mashabiki na wachezaji walipewa agizo la kubaki katika Uwanja wa King Baudouin kwa ajili ya usalama wao.

Zoezi la kuwaondoa watu kutoka uwanjani lilianza saa 22:45.

Timu ya Sweden ilipewa ulinzi wa polisi kuelekea uwanja wa ndege, wakati mashabiki wa Sweden walifuatana na polisi kuingia mjini.

Mnamo Jumanne, polisi huko Brussels walimuua mshambuliaji.

Meneja wa Sweden, Janne Andersson, alisema yeye na wachezaji walipata habari za shambulio la Jumatatu tu wakati wa mapumziko.

Nilipopata habari hizi nilipokuwa kwenye mapumziko, nilihisi ni jambo la kushangaza kabisa. Tunakaa katika ulimwengu upi leo?” alisema.

“Niliingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na wakati timu ilianza kujadili, tulikubaliana kwa asilimia 100 kwamba hatutaki kuendelea kucheza kama heshima kwa waathiriwa na familia zao.”

Bado haijulikani ikiwa waathiriwa walikuwa Brussels kushuhudia mchezo huo.

Ujumbe wa vyombo vya habari vya Shirikisho la Soka la Sweden ulisema: “Fikra zetu zinawaendea jamaa na marafiki wote walioathirika mjini Brussels.”

Akaunti ya timu ya Ubelgiji ilichapisha taarifa iliyosema: “Fikra zetu ziko pamoja na wote walioathirika.”

Video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ilimuonyesha mtu akisema kwa lugha ya Kiarabu kwamba alitekeleza shambulio hilo kwa jina la Mungu.

Baada ya shambulio katika Barabara ya Boulevard d’Ypres, lililotokea saa 18:00 BST (saa 19:00 za eneo hilo), polisi na huduma za dharura zilizuwia barabara za karibu.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander de Croo, alisema, “Nimetuma rambirambi zangu za dhati kwa Waziri Mkuu wa Sweden baada ya shambulio la kutisha la leo usiku kwa raia wa Sweden huko Brussels.

Aliongeza: “Fikra zetu ziko pamoja na familia na marafiki waliofiwa na wapendwa wao. Kama washirika wa karibu, mapambano dhidi ya ugaidi ni jambo la pamoja.”

Mchezo ulikuwa 1-1 wakati uliposimamishwa.

Kapteni wa Sweden, Victor Lindelof, alisema: “Ubelgiji tayari wameshakata tiketi yao ya kufuzu, na sisi hatuna nafasi ya kufuzu kwa Euro, kwa hivyo sina sababu ya kucheza tena mchezo huu.”

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version