Hii leo klabu ya Yanga imezindua tawi jipya la mashabiki wa klabu hiyo lilopewa jina la YANGA EXPERIENCE MASAKI.

Kwenye uzinduzi wa tawi hilo licha ya mashabiki kujitokeza lakini pia msanii Dulla Makabila alikuwepo kuwapa furaha wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi wa tawi hilo.

 

Aidha wakati akizungumza na mashabiki waliojitokeza katika tukio hilo la uzinduzi Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga ,Ali Kamwe amesema kuwa kuelekea mechi dhidi ya Al Ahly wamejipanga kuonesha namna gani wao ni wakubwa pia katika mashindano haya ya kimataifa.

“Sisi ndio mashabiki bora, sisi ni wakubwa pengine CAF hawana hizi taarifa tunapaswa kwenda kuujaza uwanja ili kuthibitisha hilo ukifika uwanjani, piga picha kisha post halafu uwatag CAF ili waujue ukweli” Ally Kamwe.

Yanga wanakwenda kucheza mchezo wa 2 wa makundi klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini Algeria kwa kufungwa mabao 3 kwa 0 mbele ya CR BELOUIZDAD

 

 

Leave A Reply


Exit mobile version