Michuano ya kombe la shirikisho la Azam (ASFC) raundi ya pili msimu wa 2023/2024 imeendelea kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja mbalimbali na matokeo kuweza kuchezwa.

Katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga klabu ya Coastal Union wamecheza dhidi ya Greenland Fc na wagosi wa kaya kuondoka na ushindi wa mabao 2:0 yaliyofungwa na Maabad Maulid Maabad.

Mchezo mwingine uliofanyika katika Uwanja wa Highland Estates , Mbarali mkoani Mbeya ulimalizika kwa Ihefu kuondoka na ushindi wa mabao 3:0 dhidi ya Rospa Fc magoli ambayo yamefungwa na Japhet Kibaya aliefunga magoli 2 pamoja na Rashid Juma aliefunga goli 1.

Aidha katika mchezo uliopigwa Azam Complex uliowakutanisha JKT Tanzania dhidi ya Kurugenzi Fc ulimalizika kwa JKT Tanzania kuondoka na ushindi wa mabao 5:0 mabao yaliyofungwa na Edward Songo aliefunga mabao 3 , Mohamed Kada aliefunga bao 1 na Moud Beka aliefunga bao 1.

Mechi ya mwisho imechezwa katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma umewakutanisha Dodoma Jiji dhidi ya Magereza mchezo ambao walima zabibu wameondoka na ushindi kwa bao 1:0.

Mshindi wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ndio huwa mwakilishi wa klabu za Tanzania upande wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Endelea kusoma zaidi habari zetu mbalimbali za michezo na makala mbalimbali kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version