Mashindano ya AFCON 2023 yataanza rasmi Januari 13 nchini Ivory Coast kwa mchezo wa ufunguzi utakaowakutanisha wenyeji Ivory Coast wakikutana na Guinea-Bissau. Leo hii tutazame wachezaji wa kuchungwa kutokana na ubora hasa kwenye uwezo wao kupachika mabao.

Kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kwa msimu huu kuna majina ya wachezaji 8 wanaocheza nafasi za ushambuliaji ambao huenda mmoja wapo akawa mfungaji bora na hii ni kutokana na viwango bora ambavyo wamevionyesha katika Ligi wanazocheza na hii ni orodha ya wachezaji wa kuchungwa AFCON 2023;

1. Mohamed Salah,huyu ni nahodha wa Misri na kila mmoja anajua moto wake ambao ameuwezesha katika kupachika mabao kwani anauwasha pale EPL na klabu yake ya Liverpool akifunga goli 14 kabla ya kutimkia AFCON.

2.Victor Osimhen, Huyu ni mchezaji bora wa bara la Afrika akichukua tuzo hiyo mwaka jana lakini pia ni moja ya washambuliaji bora kwa sasa barani Ulaya akiwa anaichezea Napoli. Osimhen alifunga goli 10 katika harakati za kufuzu AFCON 2023 na Taifa Lake la Nigeria.

3. Sadio Mane,Katika michuano ya AFCON iliyopita ambayo Senegal waliibuka mabingwa aliibuka kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo. Pale Ligi Kuu ya Saudi Arabia amefunga goli 8 katika michezo 18 aliyoichezea Al Nasri huku michezo ya kufuzu AFCON amefunga goli 5 kwa timu yake ya Taifa ya Senegal.

4. Vincent Aboubakar,Huyu ni mchezaji mkongwe katika Taifa la Cameroon akiwa na umri wa miaka 31.Katika micuano ya AFCON iliyopita alikuwa mfungaji bora akiweka nyavuni goli 8.

5. Mohamed Kudus, Huyu anaichezea timu ya Taifa ya Ghana na ni moja ya mawinga hatari wenye uwezo wa kufunga kwani katika ligi kuu ya Uingereza ana magoli 8 katika mechi 18 alizoichezea klabu yake ya West Ham.

6.Peter Shalulile,Ukimzungumzia huyu huwezi kuacha kuitaja Mamelodi Sundowns lakini pia akiwa ni straika kiongozi katika timu ya Taifa ya Namibia. Wakati wa mechi za kufuzu AFCON amefunga goli 4.

7. Sehrou Guirassy huyu ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Guinea,anacheza kwenye ligi kuu ya Ujerumani katika klabu ya VFB Stuttgart ambapo mpaka sasa amefunga magoli 17.

8. Sebastian Haller anacheza timu ya Taifa ya Ivory Coast,na ni moja ya washambuliaji hodari pale Bundesliga katika Ligi Kuu ya Ujerumani akiitumikia klabu ya Borrusia Dortmund.

Endelea kufuatilia udambwiudambwi na taarifa zaidi kuhusu michuano ya mataifa ya barani Afrika kwa kugusa hapa.

1 Comment

  1. Pingback: Wafahamu Wafungaji Bora Wa AFCON Wa Muda Wote - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version