Mhariri katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na chapisho la mchambuzi lakini pia ni shabiki wa klabu ya Simba Farhan Kihamu ambapo anasema haya yafuatayo:

MCHAKATO WA MABADILIKO, hapa nazungumzia mfumo ambapo sasa ifike wakati tufahamu wapi tumefikia na mkwamo upo wapi, mwaka wa nne sasa simulizi ni zile zile ila klabu haiwezi kusajili Wanachama wapya, hii ni sehemu moja wapo muhimu sana.

Simba inapoteza watu wangapi wenye uwezo wa kuwa Viongozi wa hii timu kwa vigezo vya kukosa kadi? Simba inapoteza mawazo mengi mapya haswa kutoka kwa vijana ambao vision yao ni mpya, matokeo yake kwa zaidi ya miaka 20 sasa sura ni zile zile hakuna watu wengi wa mawazo mapya kwenye hii dunia mpya.

Mfumo wa mabadiliko utaleta Wanachama wapya wa kizazi cha kuhoji kwa mifano na takwimu na sio kwenda kula korosho na maji tu vikaoni, as long as klabu haitokamilisha huu mchakato basi mkwamo utakuwa mkubwa eneo hili kwakuwa Shabiki ana kazi mbili tu kushangilia na kuzomea, ila Mwanachama ndio ana uwezo wa kuhoji.

SERA YA USAJILI, Sijui Viongozi wameshasahau kuwa Simba ile bora ilikuwa mseto wa Wachezaji wengi bora wazawa ambao ndio wengi zaidi kwenye timu yoyote Tanzania, tulikuwa na MO Ibrahim, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, John Bocco, Aishi Manula, Tshaba, Kapombe, Mkude Jonas, Ndemla! Kila staa wa Kitanzania alisaini Simba.

Tumekuwa wazifo kunasa saini za Wazawa wale ambao bora, soko lina Mchezaji kama Pascal Msindo kasaini tena Azam, soko lina wakina Feisal Salum, Kagoma na wengine wengi ila tumepoteza power ya ushawishi? Ama pesa? Kuna sera tumeziacha ikiwemo hii ya Wazawa bora.

PROPAGANDA, Tunaishi sana kwa maneno maneno na propaganda nyingi tunasahau mambo yetu ya msingi! Tumetolewa na Al Ahly tunasahau hii ni robo fainali ya tano tunatoka, wapi tunakwama? Wapi tuongeze nguvu? Nani anategea? Ila wote tunaiwaza na kumcheka Yanga kutolewa, Simba alikuwa na ndoto ya Nusu na Yanga alikuwa na ndoto ya makundi, nani wa kumcheka mwenzake?

Tumeenda Misri tupo busy na Fiston Mayele, makosa yale yale ya Cesar Manzoki yanajirudia tena! Asiposaini Simba? Waandishi tukiwachana tunaitwa tumetumika lakini klabu inatumia muda mwingi kwenye propaganda, tunapaswa kubadilika! Mbaya wanajua mashabiki wao wanapenda nini, ndio ubaya.

Nipo tayari kusahihishwa, nipo kwenye safari ya kujifunza na hayo ni maoni yangu.

MAONI YAKO NI YAPI MDAU WA KIJIWENI? Niandikie hapa chini

14 Comments

  1. Heisgrammy Michael on

    Viongozi wa simba wapo kwa ajiri ya maslahi yao binafsi hawajitoi kwa timu kama viongozi wa yanga wanavyojitoa
    Wachezaji wengi simba hawatufai lakini cha ajabu wanawangangania
    Hatumtaki try again

  2. Ndabilenze Ndabilenze on

    Nimeona kwenye chapisho ametajwa MANGUNGU wa msovero lakini ukweli ni kwamba mashabiki wenyewe hasa nyie mnaojiita wachambuzi ndio mnamuangusha mzee wa watu..

    Tujiulize 🤔
    simba inaweza kuishi bila chama??
    ~Ndio
    kama ndio, mashabiki wapo tayari kujenga timu kwa process bila chama kuwepo kikosi I??
    ~hapana
    Kama ni hapana..
    *MANGUNGU anaweza kuwa anapewa lawama ambazo si zake kwa sababu tu ni kiongozi na uongozi ni jalala

    *Tukubali tukatae chama ni muhimili WA Simba ila Simba kwa kumtegemea chama itakuwa inaishia robo.. kwanini???
    1.chama ni mchezaji ambaye ni WA mechi ambazo hazina matumizi makubwa ya physic,, that’s why kwenye mechi zinazohusisha timu za jeshi , mechi za Derby na timu nyingine zenye physic hawezi kuonekana
    2.kuanzia robo inahitajika team work zaidi kuliko uwezo binafsi kwasababu unakutana na timu zinakuzidi Hadi dhambi

    Swali la kizushi
    ⁉️Ni kocha gani alikuja Moja kwa Moja Simba akafika anamkubali chama???
    Jibu ni hakuna,, kwanini kwasababu chama Hana nguvu

    Re: yanga
    Hakuna mchezaji ambaye akikosekana ni pengo..
    Unajua kwanini??
    ~teamwork
    ~kwa sababu mashabiki wenyewe wanajua kibwana si yao lakini ni mchezaji WA yanga watamuunga mkono tu,,

    Kumbuka 🧠🤯
    *Kuna kipindi chama aliondoka akaenda uarabuni .. Nini kilitokea?? Aliludi .. MANGUNGU na wenzake hawakuwa tayari kujenga timu bila chama?? Walikuwa tayari.. kipi kilisababisha wamrudishe?? Mashabiki

    Note;
    $ Simba inatakiwa ijengwe upya kwenye kila nafasi ya uwanja Ili kuwe n’a uwiano WA viwango kati ya anayeanza na anayekaa benchi
    &. Simba waache kukariri mbinu siyo kila game inataka 4:2:3:1 na siyo kila game inahitaji ushinde kwa sifa za goli nyingi

    But,, mkipenda pizieni, kwasababu niliyeandika ni shabiki WA Yanga 🖐️bye🖐️🖐️🖐️💪

  3. Kwa maoni yangu. Simba na yanga inabidi ielewe maana ya solidality na kuacha kuleta mambo ya kuchekana.
    Pia hizi timu ziendapo nje zijifunze ku Focus na swala lililo wapeleka . na sio mambo mengine

    Kwa nyongeza timu zote mbili zinahitaji mabolesho katika safu ya washambuliaji

  4. Pingback: MO Dewji Rudi Tena Kazini Uwape Furaha Wanasimba - Kijiweni

  5. Pingback: Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba Sc - Kijiweni

  6. Simba imekua stabbed at backside ukiangalia kiukweli kabisa nguvu na uwezo wa wachezajiwa simba ndipo ulipofikia ndo ukomo wao hakuna miujiza mingine tena yakusema Jose Luis bado ajawaka atawaka freddy,Jobe,Barbaca ndio product ilee wanayo offer kwa simba. Sasa kwa kufikili kiundani chanzo cha crisis na decline ya simba inatoka mbali sio kwenye end product ambayo tunaiona kwenye pitch. Vipi kwa yale ambayo atuyaoni sisi tuliopo nje ya taasisi yapo sawa?
    NB:KUJIUZULU KWA WALIOSHINDWA KUONGOZA TIMU NI BUSARA KULIKO MASLAHI BINAFSI

  7. Tumechoka sasa
    Na story za mabadiliko ya simba embu leta story zingine hata kuhusu gwaride la ubingwa wa yanga

Leave A Reply


Exit mobile version