Manchester United wanajaribu kumsajili mshambuliaji Mzaliwa wa Brazil, Geyse, kutoka Barcelona.

United wanatafuta kumrithi Alessia Russo, ambaye aliamua kuondoka katika klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

Vyanzo vya karibu na klabu vilieleza kwamba Geyse, ambaye alishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa kwanza na Barca, ni mmoja wa wachezaji wanaopewa kipaumbele.

Geyse ana mwaka mmoja uliobaki katika mkataba wake, hivyo United itahitaji kukubaliana na Barcelona kuhusu ada ya uhamisho.

Mshambuliaji huyo alimaliza wa pili kwa kutoa asisti katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na pia kuwa na rekodi ya Mchezaji wa tatu mwenye kasi zaidi.

Geyse, ambaye alianza kwa kucheza timu ya taifa ya Brazil akiwa na umri wa miaka 19, anatarajiwa kucheza jukumu muhimu kwa nchi yake katika Kombe la Dunia msimu huu.

United wanatafuta kuimarisha kikosi chao baada ya kumpotezaa Alessia Russo na Ona Batlle katika wiki mbili zilizopita.

Wachezaji wote walikuwa muhimu katika kuhakikisha United inashiriki Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza lakini United haikuweza kuwabakisha kwa mikataba mipya.

Inaeleweka kuwa wawakilishi wa Russo walikuwa na mshangao na jinsi mchakato wa mazungumzo ulivyokuwa mrefu na mgumu.

Polly Bancroft, Mkuu wa soka la wanawake wa United, alikuwa ameanza mazungumzo kabla ya Sam Barnett, anayesimamia mikataba upande wa wanaume, kuja kusaidia.

United walikuwa na imani kwamba walitoa kwa mshambuliaji huyo ofa nzuri, ambayo ingemfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya klabu.

Lakini sasa anatarajiwa kujiunga na Arsenal, ambao walikataa ombi la rekodi ya dunia mwezi Januari, kwa uhamisho huru.

Kwa taarifa zaidi za usajili tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version