Baada ya kuchukua ubingwa wa dunia ngazi ya vilabu klabu ya Man City walirejea na ushindi ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Everton na Sheff Utd mabingwa watetezi wa kombe la FA wanarejea kuutetea ubingwa wao kwa kucheza dhidi ya klabu ya Daraja la kwanza Huddersfield Town.

Katika mchezo wa leo tegemea kocha mkuu wa City akifanya mabadiliko ya kikosi chake nah ii ni kutokana na kile alichonacho cha kutofungwa mechi 6 mfululizo ambapo ameshinda mechi 4 na kusare mechi 2 na mechi ya mwisho ya FA kucheza ameshinda mabao 5:1.

Ikumbukwe kabla ya mchezo huu katika mechi 10 ambazo City amecheza mechi moja pekee ndiyo ambayo hakuruhusu nyavu zake kutikiswa na mpinzani kwani na hii ni nje ya mechi za klabu bingwa ya dunia alizocheza kwani ameshinda mechi 5 kupata sare 4 na kufungwa mechi 1.

Hudders wanaingia katika mchezo huu wakitoka kupoteza dhidi ya Leicester kwa kipigo cha bao 4:1 siku ya mwaka mpya iliyopelekea kuendelea kuwa na muendelezo wa matokeo mabovu zaidi msimu huu katika ligi ya Championship kwani katika mechi 8 za mwisho kucheza ameshinda mchezo mmoja pekee akisare michezo mitatu na kupoteza michezo minne.

VIDOKEZO VYA UBASHIRI

Muendelezo bora wa matokeo alionao City mpaka sasa ni wazi mchezo huu ataingia kwa lengo kuu moja ambalo ni kushinda mchezo (City Win)

Hudders msimu huu wamefungwa mabao 44 katika mechi 26 zote walizocheza leo wanaweza kufungwa zaidi ya magoli 3 Kwa wale wa ushindi na magoli wanaweza kumpa Man City ashinde kwa zaidi ya goli 3 ( City win and Over 3 goals)

Ikumbukwe mechi 5 walizokutana City dhidi ya Hudders kumekua na magoli 16.

 

Endelea kusoma zaidi kuhusu utabiri na vidokezo vya kuandaa mkeka kwa kusoma hapa.

 

 

Leave A Reply


Exit mobile version