Baada ya mechi 2 za robo fainali hapo jana ambapo Nigeria na DR Congo zilifuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la mataifa barani Afrika, hii leo tunawatazama Mali wakimenyana na wenyeji wa mashindano ambao ni timu ya taifa ya Ivory Coast ambapo mshindi wa hapa anakutana na Watoto wa Lubumbashi DR Congo.

TAKWIMU

Timu zote 2 mara ya mwisho kukutana ilikua ni AFCON ya mwaka 2019 ambapo Ivory Coast walishinda bao 1:0 na hii leo Mali atakutana na changamoto kubwa ya mashabiki soka vichaa wa Ivory Coast katika dimba la Bouake.

  • Mali wameshinda mara 1 dhidi ya Ivory Coast wakipata sare 2 na kupoteza mara 2 katika mechi 5 za mwisho kukutana baina yao.
  • Katika mechi 11 za mwisho za mashindano yote, Mali hawajafungwa huku wakipata ushindi mara 8.
  • Ukiachilia mbali kuwa na wachezaji wengi wenye vipaji lakini Mali hawajawahi kushinda ubingwa wa AFCON ingawa waliwahi kumaliza nafasi ya 3 na nafasi ya 4.
  • Ivory Coast wamewahi kuwa mabingwa wa AFCON mara 2 ambapo ilikua mwaka 1992 na mwaka 2015 huku mwaka 2006 wakiwa wa 2.
  • Mali wameshinda mara 3 na kusare mara 2 katika mechi zao 5 za mwisho huku Ivory Coast wao wameshinda mara 3 na kupoteza mara 2 katika mechi zao 5 za mwisho.

TUNABETIJE?

Kumekua na matukio mengi ya kushangaza katika michuano hii lakini kutokana na kiwango walichokionesha Ivory Coast katika mchezo wa mwisho ni wazi wanataka kurudisha heshima nyumbani kwani wao ndio waandaaji wa michuano hii.

Utabiri Kutoka Kijiweni uko hivi:

  1. Ivory Coast anashinda mchezo huu
  2. Magoli zaidi ya 2 katika mchezo (Total Goals Over 2)
  3. Ivory Coast kuwa wa kwanza kufunga goli.
  4. Mali kupata goli ( Mali Goals Over 0.5)

SOMA ZAIDI: Mkeka wa leo Jumamosi Odds 100

1 Comment

  1. Pingback: Cape Verde vs South Africa Ukibetia Hivi Ni Uhakika - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version