Huu ni miongoni mwa ile michezo ambayo itaangaliwa na mashabiki wengi wa soka hapa Tanzania haswa wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga kutokana na kuwa ni mechi inayowakutanisha wachezaji kutoka mitaa ya Twiga na Jangwani hapa unamzungumzia Aziz Ki akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso pamoja na Djigui Diarra golikipa wa timu ya taifa ya Mali.

Mali wanaingia katika mchezo huu wa 16 bora kusaka hatua ya robo fainali kama timu pekee kutoka kundi lao kushinda mchezo 1 na kusare michezo 2 na hatua hii ya 16 bora ni mara yao ya 3 mfululizo wanaingia. Burkina Faso wao walimaliza nafasi ya pili katika kundi lao ambalo alikuwepo Algeria aliyeshindwa kufuzu hatua ya 16 bora.

TAKWIMU

Ingawa michuano ya AFCON msimu huu imekua na matokeo ya kushtusha na kustaajabisha lakini mchezo wa leo anapewa nafasi kubwa zaidi ya ushindi ni Mali kutokana na uwezo wao ulivyo mkubwa tofauti na Burkina Faso.

  • Katika michezo mitano ya mwisho iliyowahi wakutanisha Mali dhidi ya Burkina Faso, Mali ameshinda michezo 4 huku akisare 1 pekee na hii ni kuonesha Burkina Faso hajawahi kushinda mbele ya Mali.
  • Kwa upande wa magoli ni kuwa Mali wamefunga mabao 18 na kuruhusu mabao 6 katika mashindano yote ya AFCON dhidi ya Burkina Faso.
  • Mali na Burkina Faso wamekua wakishiriki katika michuano hii ya AFCON toka mwaka 1972 na mwaka 2013 na wameshiriki zaidi ya mara 13 katika michuano.

 

TUNABETIJE?

Kutokana na takwimu kuna njia hizi zifuatazo za kubashiri mchezo huu

  • Mali anashinda mchezo huu
  • Magoli zaidi ya 2 yaani (Over 2 Goals)
  • Mali kuwa wa kwanza kufunga goli (Team to score first goal Mali)
  • Mchezo kuwa na kona zaidi ya 3 kipindi cha kwanza (First Half Total Corners Over 2.5)

 

Wachezaji wa kuangalia: Mshambuliaji wa Auxerre, Lassine Sinayoko, alifunga magoli mawili kati ya matatu ya Mali katika hatua za makundi moja kila mmoja dhidi ya Afrika Kusini na Tunisia, yote yakitokea kwenye uwanja ule ule ambapo mchezo huu utachezwa. Wakati huo huo, wenzake wa Burkina Faso walifunga bao moja tu kutoka mchezo wa wazi, huku Bertrand Traoré akifunga mara mbili kutoka kwa penalti.

Takwimu muhimu: Mechi tano kati ya sita za hatua za makundi kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly zilizalisha jumla ya mabao chini ya 2.5.

SOMA ZAIDI: Mkeka wa leo jumanne wenye odds 100

 

1 Comment

  1. Pingback: Morocco vs South Africa, Takwimu Na Jinsi Ya Kusuka Mkeka - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version