Maguire bado hali ni tete! Lakini kwa upande mwingine Mason Mount anafanyiwa uchunguzi wa matibabu Manchester United leo kabla ya kuhamia kwa pauni milioni 60 kutoka Chelsea.

United wametoa mkataba wa miaka mitano kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England na chaguo la kuongeza mwaka mmoja.

Baada ya makubaliano ya kumsajili Mason Mount, United wanatarajiwa kuangazia usajili wa mshambuliaji na mlinda lango.

Wakati huo huo, Manchester United wanatamani kumuuza Maguire, Scott McTominay, na Anthony Martial, ripoti ya The Sun inasema.

Maguire ambae hakuwa na msimu mzuri United yuko njiani kutemwa katika kikosi hicho.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa kocha wa United, Erik ten Hag, pia ana imani ya kumuuza Fred kwenda Fulham kwa pauni milioni 15.

Mason Greenwood anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu – na The Sun inadai kuwa kocha wa Roma, Jose Mourinho, amewasiliana na mchezaji huyo kumpa nafasi nyingine.

United wanafanya uamuzi kuhusu ikiwa wabaki na mchezaji wao wa akademi na wanaendesha uchunguzi wa ndani.

Greenwood anaweza kupelekwa kwa mkopo kwa mwaka mmoja au mkataba wake unaweza kusitishwa.

Kwa taarifa zaidi za usajili tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version