Paris Saint-Germain wako karibu kukubaliana na makubaliano ya Luis Enrique kuwa kocha wao mkuu mpya.

Mabingwa hao wa Ufaransa wanatarajia kumteua Mhispania huyo baada ya kumfuta kazi Christophe Galtier, ambaye kuondoka kwake kuliwekwa wazi siku ya Jumatano asubuhi.

Luis Enrique alikuwa kwenye orodha fupi ya Chelsea na Tottenham kwa nafasi za ukufunzi za hivi karibuni na hakuwa na kazi tangu alipoondoka Hispania mwezi Desemba baada ya kutolewa katika hatua ya 16 ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco huko Qatar.

Kazi ya mwisho ya klabu  kwa kocha huyo  mwenye umri wa miaka 53 ilikuwa na Barcelona, ambapo alishinda mataji matatu mwaka 2015.

Meneja wa zamani wa Roma na Celta Vigo sasa anaonekana kuwa atamrithi Galtier licha ya mwenye umri wa miaka 56 kuiongoza PSG kutwaa taji la Ligue 1 msimu uliopita.

Hata hivyo, matokeo ya PSG yalishuka baada ya Kombe la Dunia na walipata kushindwa mara 10 katika mechi 28.

Walifungwa na Bayern Munich katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa, na pia walishtushwa na kushindwa katika hatua ya 16 dhidi ya wapinzani wao Marseille katika Kombe la Ufaransa.

Galtier amefutwa kazi na mwaka mmoja bado kwenye mkataba aliokuwa amesaini na PSG baada ya kuteuliwa mwezi Julai 2022.

Taarifa ya klabu ilisema: “Kikosi kizima cha Paris Saint-Germain kinapenda kumshukuru Christophe Galtier, pamoja na wasaidizi wake Thierry Oleksiak na João Sacramento, kwa weledi na kujitolea kwao kwa msimu mzima, na tunawatakia kila la kheri katika maisha yao ya baadaye.”

Ingawa PSG walitoa salamu za heri kwa Galtier, anatoka klabuni huku akiwa na utata. Ijumaa, aliitiwa wito kuja kujibu mashtaka mwezi Desemba kuhusu mashtaka ya unyanyasaji wa kisaikolojia na ubaguzi kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubaguzi wa rangi katika klabu yake ya zamani Nice.

Mfaransa huyo na mwanae, John Valovic-Galtier, walikamatwa kwa mahojiano siku ya Ijumaa asubuhi. Baada ya mwanae kuachiliwa bila mashitaka, Galtier – ambaye anakanusha madai hayo – alipelekwa kwa ofisi ya mwendesha mashtaka kushtakiwa huko Nice tarehe 15 Desemba.

Leave A Reply


Exit mobile version