IlipoishiaNdani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika Kijijini  hapo. 

Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuata  Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenye  gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyo  alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo,  alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangaza  huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbani  anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu,  hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. Macho  ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond alienda  hadi alipojificha Sanga 

“Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapo na Sanga.  Endelea  

SEHEMU YA TATU 

“Ndiyo Desmond! Uchunguzi unaendelea hivyo ni lazima tutoe  taarifa kila hatua” Alieleza askari huyo kwa njia ya simu,  Desmond alitamani kumwambia Askari huyo asirushe chochote  lakini alishindwa sababu angeulizwa kwanini anataka taarifa  zisiruke alafu angekosa jibu la kumpa, alikata simu  akairudisha kwenye mfuko wake. 

Siku zilienda, Desmond na Noela walipanga kuvishana pete ya  uchumba ili mahusiano yao yatambulike, japo Desmond alikuwa  na Mke tena aliyefunga naye ndoa kanisani ila hakutaka kusema  chochote kile, akili yake ilizidi kumwambia kuwa Mandy  atakufa muda wowote ule, walipanga siku ya tukio hilo, hofu  ya Desmond ikawa kwa Lucia kama atapewa hiyo taarifa alafu  akahudhuria sherehe hiyo fupi ya kuvishana pete na kama  unavyojuwa Lucia alikuwa akifahamu kuwa Desmond ana Mke tena  yupo Hoi Hospitalini. 

Miongoni mwa Watu ambao Noela aliwaarika alikuwa ni Lucia  sababu alikuwa ni rafki yake wa zamani, Desmond alimwambia  Noela hana sababu ya kuarika Watu wengi hivyo sababu ni  sherehe fupi ambayo inawahusu wao na baadhi ya ndugu. 

“Sijawahi kuvishwa pete katika Maisha yangu Joshua, wewe  ndiye Mwanaume wangu wa kwanza kunipeleka kwenye ulimwengu  huu hivyo ni fahari kwangu kuona marafiki zangu wanakuja  hapa” Alisema Noela siku moja baada ya Desmond kulalamika  kuwa anaarika Watu wengi. 

“Najuwa Mpenzi wangu lakini tukio hili ni la kushuhudiwa na  Watu wachache sana, Aaah…” Alisema Desmond huku bado  akitafunwa na hofu ya Lucia kuarikwa 

“Joshua nimearika marafiki wachache sana, usiwe na wasiwasi  kuhusu hilo. Nakuelewa Mume wangu mtarajiwa” Alisema Noela  kisha alisema

“Naenda chooni mara moja” Aliaga kisha aliondoka lakini  aliacha Kitabu chenye majina ya Watu walioarikwa kwenye  shughuli hiyo, haraka Desmond alikifunua, kama alivyofikiria  ndivyo ilivyokuwa, Lucia aliarikwa kwemye shughuli hiyo, jina  lake lilikuwa la tatu kutoka juu akimaanisha kuwa ni miongoni  mwa Watu muhimu zaidi kwake, kijasho kilimtoka Desmond,  alifikiria haraka haraka afanye nini ili kumzuia Lucia  asiende kwenye tukio hilo la kuvishana pete maana kama Lucia  ataenda basi mambo mawili yatajulikana, kwanza ni jina lake  halisi ambalo siyo Joshua na pili ni kwamba ana Mke hivyo  haruhusiwi kuowa Mke mwingine kwa mujibu wa sheria za dini ya  Kikristo. 

Walikuwa kwenye moja ya Bustani nzuri wakizungumza, Desmond  alikaa kwenye kiti akiwa amechoka mwili na akili, akakumbuka  Maswali aliyoulizwa na Lucia juu ya jaribio la kutaka kuuawa  kwa Mandy, moja kwa moja alijuwa mambo mengi yanaenda  kujulikana kama ataruhusu Lucia kuwepo kwenye Shughuli hiyo,  akiwa anaendelea na tafakari Noela alirudi akamkuta Desmond  akiwa katika hali ya mawazo sana 

“Kulikoni Bebe?” Alihoji, kijasho kilikuwa kikimtoka Desmond,  Noela alimpa kitambaa Desmond ili ajifute jasho 

“Unaumwa?” Aliuliza tena Noela 

“Ndiyo ghafla tu sijisikii vizuri, usijali nitakuwa sawa”  Alisema Desmond kisha alijifuta jasho alafu akashushia maji  ya baridi, Noela aliketi, aliona kitabu kimefunguliwa 

“Au kwasababu umeona nimearika idadi kubwa ya Watu Joshua?”  Aliuliza Noela akiwa mwenye wasiwasi huwenda Desmond ana  hasira 

“Hapana Noela ni tofauti na ufikiriavyo, ni ghafla tu  najisikia vibaya” Alisema Desmond, Noela alisema 

“Ngoja nimpigie rafiki yangu ni nesi” 

“Rafiki yako nesi?” Alihoji Desmond akiwa katika hali tofauti  kabisa hata Noela alishangaa maana Mtu ambaye alionekana kuwa  na hali mbaya 

“Mbona umeshtuka sana niliposema nampigia rafiki yangu nesi?  Si wewe ulikuwa katika hali ya homa?” Kiukweli Noela alizidi  kumshangaa Desmond 

“Hukuwahi kuniambia kama una rafiki yako Nesi” Alisema  Desmond, Noela alitabasamu akagundua ni kweli hakuwahi 

kumwambia Desmond istoshe alikutana na rafiki yake huyo siku  chache zilizopita 

“Oooh ni kweli, ni rafiki niliyesoma naye. Tulipotezana muda  mrefu sana ni majuzi tu ndiyo tumeonana. Hata hivyo  nimemuarika kwenye shughuli yetu lakini nakumbuka kama  niliwahi kukwambia, atakuja utamuona anaitwa Lucia” Alieleza  Noela kisha alimpigia Lucia lakini kabla hata simu haijaita  Desmond alimkatisha Noela 

“Huna haja ya kumsumbua nitakuwa sawa tu” Alisema Desmond  huku akitafakari kuhusu Lucia, aliona wazi vita kubwa inaenda  kupigwana mbeleni 

“Hivi unajua Joshua sikuelewi, unatokwa jasho namna hiyo lafu  hutaki nimuite Lucia?” Aliuliza Noela 

“Nimesema nitakuwa sawa, tunaweza ondoka hapa” Alisema  Desmond kisha alisimama, Noela naye alisimama japo kwa  kuchukia kisha waliongozana hadi kwenye gari ya Desmond,  walianza safari ya kuondoka pale kuelekea nyumbani anakoishi  Noela, baada ya kumaliza mizunguko yote alirudi kwenye nyumba  aliyokuwa akiishi na Mandy. 

Kuna dokumenti alizihitaji akaenda kufungua kabati la Mandy  ambalo alikuwa akiweka baadhi ya vitu vyake muhimu kisha  alitoa Mkataba wenye umiliki wa Mali za Mandy yakiwemo  Mashamba, kampuni ya Kuuza Vipuri vya Magari na Mgodi mmoja. 

Alipozipata nyaraka hizo muhimu alizipitia, alithibitisha  ndizo alizokuwa akizihitaji kwa wakati huo, kisha alimpigia  Mtu mmoja simu akasema 

“Joel ninazo, nakuja ofisini kwako” Alisema Desmond kisha  alikata simu, aliingia kwenye gari akaelekea kwa Joel ambaye  alikuwa ni Mwanasheria wa Mandy. 

Alifika ofisini kwa Mwanasheria huyo aliyeitwa Joel, alikuwa  ni Mtu makini aliyefahamu kilichotokea kati ya Mandy na Mume  wake Desmond, walitazmana huku nafsi zao zikizungumza,  walionesha kujuwa hasa walichodhamiria kufanya. Haraka  Desmond alizama kwenye mkoba wake akatoa zile nyaraka muhimu  za Mandy. 

Joel aliketi akazipitia kisha akamwambia Desmond baada ya  dakika kadhaa za ukimya kupita 

“Ni zenyewe” Alisema hivyo huku akizidi kutafakari jambo,  Desmond aligundua kisha akamuuliza

“Unafikiria nini Joel?” Alimuuliza Mwanaume huyo mweupe  mwenye mvi kiasi ambaye umri wake ulienda kidogo 

“Nafikiria kuhusu Mandy, tunachofanya ni kumzika akiwa hai,  nakumbuka mengi ya zamani” Alisema Joel huku akifuta chozi  jicho moja 

“Wewe ni mshamba sana Joel, hukuzaliwa kuwa masikini. Huoni  aibu? Huhisi haya machoni pako? Mwaga wino hatukuanza leo”  Alisistiza Desmond huku akizidi kumshangaa Joel, basi Joel  alichukua peni akaiweka juu ya nyaraka hizo akamwambia  Desmond 

“Hiki ninachokifanya kinaenda kubadili kila kitu katika  Maisha yangu, uadilifu na uaminifu wangu kwa Mandy unazikwa  baada ya kutia saini nyaraka hizi Desmond. Natamani kurudi  nyuma na kuzuia hili lisitokee” Alisema Joel huku akizidi  kujilaumu 

“Mandy ni wa leo wa kesho, unataka afe ili nihangaike na  familia yake si ndiyo?” Alisema Desmond kisha alimlazimisha  Joel kutia saini ya makubaliano kuwa Mandy amempa mali hizo  Mume wake Desmond, kwa Mamlaka aliyonayo Joel alitia saini 

“Ooooh!! Sasa umefanya kwa upande wako, kilichobakia ni kule  Hospitali, twende tukamalize mchezo” Alisema Desmond kisha  alisimama 

“Desmond una uhakika kuwa Mandy atakufa?” Joel aliuliza 

“Asipokufa atakuwa na mapungufu kwenye ubongo wake, ni lazima  atapoteza kumbukumbu tu” Alisema Desmond kwa kujiamini 

“Baada ya hapa nitakupatia kiasi kikubwa cha pesa kisha  utakuwa na jukumu la kuitunza siri hii” Alisema Desmond kisha  walitoka wakaelekea kule Hospitalini. 

Walipofika walimkuta Lucia akiendelea kumuangalia Mandy maana  ndiyo jukumu lake kuu alilopewa, Lucia aliwatazama Desmond na  Joel Mwanasheria. 

“Samahani Lucia kuna jambo Mwanasheria wa Mandy amekuja  kufanya” Alisema Desmond, Lucia alishtuka akamuuliza Desmond 

“Unahisi Mandy hatoweza kuamka?” Alihoji akiwa kama muuguzi  namba moja wa Mandy, alihisi kuna jambo lisilo la kawaida  ndiyo maana Mwanasheria huyo alienda Hospitalini. Desmond  alimvuta pembeni Lucia akamwambia

“Siyo kila jambo linaendeshwa kimihemko Lucia, mambo mengine  unapaswa kuyaangalia tu. Wewe ni nesi na utabakia kuwa nesi”  Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa ukomavu huku akiwa  amemshika mkono kwa nguvu Lucia 

“Hata kama Desmond, nimemungalia Mke wako kwa kipindi kirefu.  Lipo tumaini ndani yake, kuwa na subra” Alijibu Lucia 

“Unajuwa nini wewe Lucia? Unajuwa nini kuhusu familia yangu!?  Kumuuguza Mandy ni jukumu lako sababu unalipwa msharaha  hufamyi bure hapa” Alisema Desmond kwa sauti ile ile 

“Desmond! Desmond vuta subra Mkeo ataamka tena” Alisema Lucia  akionesha kuumizwa sana, mara nyingi Mtu anapokuwa mgonjwa  sana alafu Mwanasheria akaja basi kunakuwa na uwezekano  Mkubwa sana kuwa kuna mjadala wa mali za mgonjwa, Lucia  aliligundua hilo 

Basi Desmond na Lucia walirudi huku Lucia akitaka kusema kitu  lakini Desmond hakutaka kumsikiliza Lucia, Mwanasheria Joel  alitoa wino kisha alipakaza kwenye kidole cha Mandy. Akaweka  saini kwenye zile karatasi, Desmond alikabidhiwa karatasi  hizo kisha alizisoma tena, Lucia alichungulia kuona kulikuwa  kumeandikwa kitu gani kwenye karatasi hizo. 

Aliona maandishi yaliyosomeka 

“MAKABIDHIANO YA MALI KATOKA KWA MANDY KWENDA KWA DESMOND” 

Alishtuka sana Lucia, alimtazama mara mbili mbili Desmond,  jinsi alivyokuwa amemchukulia Mwanzo aliona kabisa  alimchukulia tofauti kabisa kwa jinsi alivyo sasa, alimuona  Desmond kuwa ni mkatili na jambo ambalo alikuwa analifanya  pale lilijaa tamaa za kutosha, alishindwa hata aseme nini.  Baada ya kumaliza Desmond na Mwanasheria Joel waliondoka  Wodini, Lucia alichoka roho na mwili huku akihisi kabisa  viungo havifanyi kazi tena. 

Alijikutana akikaa chini taratibu huku akijawa na mshangao  mno, aliona kabisa kitendo kile kilifanywa bila ridhaa ya  Mandy. Alifuta chozi lake lililoanza kumdondoka kisha  alijishangaa ni kwanini alikuwa akilia, alinyanyuka kisha  alimtazama sana Mandy, alimuonea huruma. Alitamani aamke ili  ashuhudie kilichokuwa kinafanywa na Mume wake, akili ya Lucia  ikamwambia 

“Basi Desmond anaeeza akamuuwa Mke wake kama ameweza  kumsainisha akiwa hoi kitandani basi anaweza akaondoa uhai  wake” Akili ya Lucia ilifika ukomo wa kutafakari jambo hilo.

Usiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani,  alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwa  la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahi  kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijicheka  akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodi  Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao. 

Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasi  kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipiki  alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywa  sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani. 

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNE

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

5 Comments

  1. “Kuna mpango mkubwa unaoandaliwa na mataifa makubwa kuirudia na kuigawanya Africa kama walivyofanya katika mkataba wao wa Berlin miaka ya 1884-1885 na mara hii kutaka kuiangamiza kabisa…..

    ….Hatimaye msichana ambaye ana asili ya kiafrika anayechukua masomo yake katika mojawapo ya mataifa yao anagundua na ANAAMUA KUUZUIA MPANGO HUO!!!!”

    Hahahah JE HII ITAKUA ZAIDI YA ILE YA MAYA WA ULAYA???? USIIKOSE HII KITU CHALII YANGU!!!

    https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/665

    Like moja hapa kisha follow channel kama bado usiikose hii ….
    hivi karibuni usiikose!!!

Leave A Reply


Exit mobile version