IlipoishiaDesmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwa  na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha Desmond  alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafika  eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawa  huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake Noela 

“Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” Aliuliza 

“Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee na  majukumu mengine” 

“Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingia  kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na pia  ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipanga  kuonana na Noela. Endelea

SEHEMU YA PILI

Waliagiza chakula kwa pamoja kisha walianza kula huku  wakizungumza masuala yao ya kimapenzi, japo Desmond alikuwa  akicheka ila akili yake ilikuwa kule Hospitalini alipo Mke  wake, ucheshi wa hapa na pale uliendelea huku wakinyweshana  na kulishana, ghafla simu ya Desmond iliita, kutokana na hofu  aliyonayo alijikuta akiangusha glasi ya Juisi ikamwagikia  kwenye nguo ya Noela 

“Oooh samahani mpenzi naomba nipokee simu” Alisema Desmond 

“Usijali Joshua, naenda chooni mara moja” Alisema Noela kisha  alinyanyuka akaelekea chooni kwa ajili ya kujisafisha. 

Aliingia chooni akajisafisha vizuri lakini wakati anatoka  alikutana na Nesi Lucia, walikuwa ni marafiki wa zamani sana,  basi walipoonana walikumbatiana kwa furaha 

“Eeeh za Maiaka Noela?” aliuliza Lucia 

“Nzuri, jamani Lucia umekuwa mzuri hivyo jamani” Alisema  Noela kisha alimkumbatia tena Lucia 

“Oooh Miaka mingi imepita Maisha yapoje?” aliuliza Lucia 

“Mungu anasaidia, kuna kipindi nilisikia umekuwa Mwanasheria  mzuri sana Nchini” 

“Yeah!! Mimi ni Mwanasheria pia mpelelezi nina kampuni yangu  Binafsi japo bado nipo serikalini, wewe je?” Alisema Noela  kisha alitupa swali kwa rafiki yake huyo wa zamani 

“Namshukuru Mungu mimi ni Nesi napambana na wagonjwa” Alijibu  Lucia kisha walicheka kwa pamoja, walipeana namba za simu  kisha Lucia aliuliza 

“Kumbe unakujaga hapa kula?” 

“Ndio mara nyingi sana ila leo nipo na Shemeji yako” 

“Oooh! natamani kumuona jamani, hapana shaka ni mzuri kama  wewe mwenyewe” Alisema Lucia 

“Ha!ha!ha! hujaacha utani tu, haya twende ukamuone” Alisema  Noela 

“Haya twende mara moja, ni muda sana aisee kweli Maisha  yanabadilika” Alisema Lucia kisha stori zao zingine  ziliendelea, Desmond alikuwa bize na simu hivyo hakujuwa kama  Mpenzi wake ameongoznaa na nesi anayemuhudumia Mke wake  Hospitalini.

Bahati nzuri ile anageuka anawaona Lucia na Noela wakienda  alipo, Desmond aliinama chini 

“Ina maana Nesi Lucia na Noela wanafahamiana, oooh  nimeshaharibu hapa, vipi kama Lucia akimwambia Noela kuwa  nina Mke?” alijiuliza Desmond, aliponyanyua tena kichwa  alimuona Noela akiwa peke yake, alishangaa sana wakati  sekunde chache alikuwa ameongozana na Lucia, Noela aliketi 

“Mwenzio yupo wapi?” alihoji Desmond kwa umakini sana 

“Ni rafiki yangu yule kumbe ulimuona, anaitwa Lucia ni nesi,  nilisoma naye kitambo” Alijibu bila wasiwasi Noela lakini  hakutatua kiu ya Desmond ya kutaka kujuwa alikuwa ameenda  wapi 

“Yupo wapi sasa?” Alihoji Desmond 

“Amepigiwa simu kuwa kuna Mgonjwa amerudisha fahamu hivyo  ameelekea Hospitali” Kusikia hivyo Desmond alijuwa moja kwa  moja ni Mke wake Mandy 

“Amerudisha fahamu, hajataja chochote?” aliuliza Desmond kama  Mtu aliyeingiwa na kichaa 

“Kutaja chochote? Nani unamzungumzia” 

“Aah samahani, siwezi kuendelea kuwa hapa mpenzi” Alisema  Desmond kisha aliondoka hapo mbio mbio 

“Hivi huyu Mwanaume anan nini siku hizi mbona amekuwa na  tabia za hovyo? mara hapokei simu mara anazungumza vitu  sivielewi” Alijiuliza Noela kwa sauti iliyoambatana na kilio  kidogo. 

Haraka haraka Desmond alifika Hospitalini ambako Mandy  alikuwa amelazwa, alikuwa amechoka mwili na akili yote huku  hofu yake ikiwa kwa Mandy kuwa ameamka, alipofika wodini  alimkuta Mandy akiwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua,  pembezoni kukiwa na daktari, wahudumu wote wa afya ndani ya  Hospitali hiyo walikuwa wakimfahamu Desmond, yule Daktari  alimuuliza 

“Mbona upo hivyo Desmond” Aliuliza akiwa anafanya kazi yake,  Desmond alitikisa kichwa chake kisha alitoka wodini humo  akiwa amechoka sana, kiasi fulani alishusha pumzi zake baada  ya kugundua kuwa Mandy alikuwa hajazinduka, alishika sehemu  ya moyo wake kama ishara ya hali yake ya wasiwasi. 

************

Jioni Noela aliporudi nyumbani kwao alijikuta akikosa raha,  mvua ilikuwa ikinyesha hivyo alijifungia chumbani kwake,  alianza kupitia mafaili ya kazi zilizo mbele yake. Kila  alichokisoma hakikuingia kwenye akili yake, alijiona ana  mzigo mzito kichwani pake. 

Alijilaza kitandani akiwa hoi kwa mawazo, Desmond  alimchanganya sana kwa jinsi alivyobadilika ghafla, hakujuwa  jambo zito lililo kichwani pa Desmond ambaye yeye alikuwa  akimfahamu kama Joshua, wakati anawaza baadhi ya mambo  alijikuta akikumbuka tukio la mchana alivyokutana na rafiki  yake wa zamani ambaye ni nesi Lucia. Alifikiria amtafute  maana baada ya kupeana namba ule mchana hakuna aliyemtafuta  mwenzake, alinyanyua simu yake akampigia, simu iliita kwa  kitambo kidogo kabla ya kupokelewa. 

“Hello Lucia” Alisema Noela 

“Abee kipenzi! nilitingwa kidogo nikasema nikutafute baadaye”  Alisema pia Lucia 

“Oooh nafikiri hiyo baadaye ndiyo hii, hebu subiri vipi hali  ya huyo Mgonjwa wako uliyemkimbilia?” Aliuliza Noela maana  alipoachana na Lucia ule mchana alikuwa alikimbilia Hospitali 

“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri sana, sijui shem wangu  japo sikubahatika kuonana naye” Alisema Lucia 

“Naye yuko poa Lucia, usijali utamuona siku moja” Alisema  Noela 

“Anaitwa Nani vile?” aliuliza Lucia, Noela alikaa kimya kwa  sekunde chache kisha akamjibu 

“Anaitwa Joshua” 

“Ohooo ana jina la kipekee, natumaini ni mzuri kama wewe”  Alisema Lucia kisha wote walicheka kisha waliagana kwa  kutakiana jioni njema na mara moja simu ilikatwa. 

Noela alishusha pumzi zake, angalau kidogo alijiona hana  mzigo mzito kichwani. 

Mara mlango wa chumba chake uligongwa, alijisomba kitandani  akaenda kuufungua, alikuwa ni Mama yake aliyezoea kumuita  Mlami 

“Vipi Mlami?” Alihoji Noela, alimtazama Mama yake alikuwa  ameshikilia kikombe cha Maziwa

“Na hii baridi nimekuletea maziwa ya moto Binti yangu, vipi  ulizungumza na Joshua?” Aliuliza Mama yake Noela akiwa  anampatia Noela kikombe chenye maziwa, Noela alikipokea kisha  alimjibu Mama yake akamwambia 

“Ndiyo Mama! Lakini Joshua siku hizi simuelewi elewi” Alisema  kisha alipiga maziwa kidogo 

“Humuelewi? Kwani amekuwaje!” Aliuliza Mama Noela 

“Wee Mlami acha tu, nitakueleza vizuri Mama. Nikutakie jioni  njema” Alisema Noela kisha alifunga mlango, hali hii  ilimfanya Mama yake Noela kupata mawazo ya jambo lipi  lililokuwa likimsibu Binti yake. 

Siku iliyofuata mapema sana Desmond alikuwa ofisini kwake  akiendelea na kazi, alionekana kuwa bize sana siku hiyo  kuliko hata kawaida yake. Akiwa anaendelea na kazi alisikia  simu yake ikiita, alipotupa macho kwenye kioo aliona ni  askari ambaye alikuwa alichunguza tukio la kifo cha Mama  Mandy ambaye alionana naye kule Hospitalini, ndiye aliyekuwa  akimpigia Desmond. Aliishika simu akiwa ana tafakari huku  akijiuliza askari huyo alikuwa akitaka kusema nini? 

“Kwanini ananipigia leo?” Alijiuliza huku simu ikizidi kuita,  aliweka sauti vizuri kisha aliipokea 

“Hallo” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa umakini wa hali ya  juu 

“Mr. Desmond, mtuhumiwa namba moja wa kifo cha Mama Mandy  ameonekana kwenye kijiji kimoja kinachoitwa Pendahili ambacho  kipo kaskazini mwa Mkoa jirani, tukimpata yeye tutakuwa  tumepata ufumbuzi wa kesi hii” Ilisikika sauti ya Askari  huyo, Desmond alishtuka sana akauliza 

“Unamaanisha Sanga?” 

“Ndiyo! Mfanyakazi wenu wa ndani aliyepotea baada ya tukio  lile lililopelekea Mkeo kuwa katika koma” 

“Amekamatwa?” 

“Bado hajakamatwa ila tayari tumetuma polisi kuelekea huko  sasa hivi” Alisema Askari huyo 

“Haya asante kwa taarifa” Alisema Desmond kisha alikata simu  hiyo haraka sana

“Sanga anawezaje kurudi Kijijini kwao wakati tulikubaliana  aende mbali?” Alijiuliza Desmond akiwa ameshikilia simu yake,  akakumbuka jinsi ilivyokuwa siku ya Tukio 

Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiongea na Huyo Sanga ambaye  alikuwa ni mfanyakazi wao wa ndani wakati huo Mwili wa Mandy  ukiwa katika ngazi ukivuja damu. Desmond alikuwa ametapakaa  damu mikononi, alimwambia Sanga akiwa katika hali ya  Kuchanganikiwa sana 

“Polisi watakuja hapa watakukamata Sanga kwasababu kuanzia  sasa wewe ndiye Muuwaji uliyemuuwa Mke wangu! Ukikamatwa  utaozea jela, nakupa pesa uwende mbali sana na usirudi”  Alisema Desmond kisha alipandisha juu akarudi na kiasi  kikubwa cha pesa akampa Sanga 

“Kumbuka hupaswi kwenda Kijijini kwenu wala kujulikana mahali  ulipo” Sanga naye alikuwa amechanganikiwa alipokea pesa hizo  kisha alikimbia nyumbani hapo, kisha Desmond aligeuka  akamtazama Mke wake ambaye aliamini alikuwa amekufa,  alichukua bastola akajipiga begani, aligumia kwa maumivu  akajilaza chini kisha akapiga simu polisi, walipofika polisi  Desmond aliwaambia polisi hao kuwa aliyefanya matukio hayo  alikuwa ni Mfanyakazi wao wa ndani aliyeitwa Sanga. 

Tokea siku hiyo Sanga aliyafutwa kila kona huku akihusishwa  na tukio la kutaka kufanya jaribio la kumuuwa Mandy pamoja na  Desmond, tukio hilo likahusishwa kitaalam na ufichaji wa siri  ya kifo cha Mama Mandy ambacho kilitokea miezi miwili  iliyopita kabla ya tukio hilo. 

Desmond alimaliza kukumbuka kisha alisema 

“Sanga ukikamatwa utatoa siri ya ulichokiona, sitoruhusu hilo  litokee” Mara moja Desmond aliondoka ofisini hapo akachukua  gari yake akaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji hicho  ambacho alitokea Sanga. Aliendesha gari kwa spidi sana ili  awahi kabla ya polisi kumkamata Sanga. 

Upande wa pili, Noela alikuwa akimpigia simu sana Desmond  bila mafanikio ya kupokelewa kwa simu hiyo hali iliyomfanya  azidi kuwa na wasiwasi na mpenzi wake huyo, alimuita Zanda  akampa kazi ya kumtafuta Desmond kwa njia ya mtandao ili  ijulikane mahali alipo Desmond, hofu na mashaka vilianza  kumuingia Noela huku akitafakari mpenzi wake huyo alikuwa  akipitia jambo gani maana alikuwa haeleweki, ndani ya dakika  kadhaa mtandao ulionesha alipo Desmond, alikuwa akitoka nje  ya Jiji hilo.

“Aaas!! Anaenda wapi!?” Alijiuliza sana Noela kisha alichukua  kibegi chake akaondoka ofisini hapo. 

Safari ya Desmond kuelekea Kijijini ilizidi kusonga mbele,  lengo likiwa kumzuia Sanga asiingie mikononi mwa polisi,  alizidi kuunguza mpira kwa spidi kali sana. 

Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika Kijijini  hapo. 

Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuata  Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenye  gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyo  alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo,  alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangaza  huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbani  anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu,  hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. Macho  ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond alienda  hadi alipojificha Sanga 

“Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapo  na Sanga 

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain 

11 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version