IlipoishiaUsiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani,  alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwa  la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahi  kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijicheka  akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodi  Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao. 

Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasi  kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipiki  alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywa  sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani. Endelea 

SEHEMU YA NNE

“Lucia kwanini umekunywa hivi Mwanangu jamani” alisema Mama  Lucia akiwa anamuingiza Lucia ndani, alimpeleka hadi chumbani  Kwake, alimuweka kitandani 

“Lucia umepatwa na nini leo? Sijapata kukuona ukiwa umekunywa  kiasi hiki” Alisema Mama yake Lucia huku Lucia akiangua  kicheko kisha alisema kwa ulevi 

“Ukiwa mzima kila Mtu atakupenda lakini kosa lako uumwe au  ufe, kila Mtu atakuwa adui wa Maisha yako Mama” Alisema Lucia  kisha alibeuwa kidogo, Mama yake alitamani kufahamu ni  kwanini Lucia alisema hivyo 

“Kwanini unasema hivyo?” Alihoji Mama Lucia 

“Mama sisi Binadamu ni wabaya sana, tunacheka mbele kisha  nyuma tunanuna ha!ha!ha!” Alisema kisha alicheka lakini Mama  Lucia alihisi Mtoto wake pengine amekutana na jambo zito  sana, ni kweli Lucia alikutana na janbo zito mno 

“Pumzika Lucia tutaongea kesho” Alisema Mama Lucia kisha  alitoka chumbani humo, baada ya Mama kutoka Lucia alichukua  simu yake akampigia Noela, alihitaji msaada kutoka kwa Noela 

Wakati simu hii inapigwa usiku huo, Noela alikuwa amelala na  Desmond, Mara moja Noela alishtuka akaipokea huku akiwa  mwingi wa Usingizi 

“Hello?” Alisema Noela kwa sauti ya Usingizi, Desmond alikuwa  amelala 

“Noela nahitaji msaada wako” Alisema Lucia 

“Msaada gani huo?” Aliuliza Noela huku akinyanyuka kitandani  na kwenda dirishani ili tu asimpigie kelele Desmond

“Nataka msaada wa kisheria kwa mgonjwa wangu…ipo hivi….”  Lucia alimuelezea Noela alichotaka kusaidiwa 

“Hivi una uhakika na unachokisema? Unaonekana umelewa sana  kwanini tusiongee kesho hili jambo?” Aliuliza Noela, Lucia  alikubali kuzungumza na Noela kesho yake. 

Simu ilikatika, kwa Mshituko Noela alipogeuka alimuona  Desmond 

“Eeeeh Joshua umeamka?” Alihoji Noela kwa mshtuko maana  hakutegemea kama angemkuta akiwa amemsimamia nyuma 

“Ulikuwa unaongea na nani?” Aliuliza Desmond 

“Aaah ni mteja wangu alikuwa anahitaji msaada wa kisheria,  usijali Mpenzi twende tukalale” Alisema Noela, hakujuwa kama  msaada alioombwa na Lucia ulimuhusu Mtu aliyekuwa naye Usiku  huo, Ndiyo!! Lucia alihitaji msaada wa kisheria kwa Mandy  maana alichokiona pale kilimtisha sana. 

Asubuhi mapema sana Lucia alienda Hospitalini kama kawaida  yake, safari hii alikuwa makini zaidi na Mandy maana alijuwa  kuna jambo linachezwa nyuma ya ufahamu wake, alitembea  taratibu akizunguka kitanda cha Mandy huku akijiuliza afanye  nini kuzuia jambo hilo kutokea au kuwa baya zaidi. Alipata  wazo fulani, alimfuata Daktari Mkuu wa Hospitali akamuomba  Mandy aongezewe Huduma zaidi ili kuharakisha afya yake irejee  kama mwanzo maana ilionekana kuwa na uwezekano wa Mandy  kupona japo haikujulikana atapona lini licha ya wasiwasi kuwa  hata kama kiamka hatoweza kukumbuka chochote au anaweza  kukumbuka lakini akawa hawezi kuzungumza wala kufanya  chochote kile. 

“Kwanini umekuja kuniomba kuhusu hilo jambo?” Aliuliza  daktari Mkuu wa Hospitali 

“Ni jukumu langu Kuhakikisha Mandy anakaa sawa haraka kuliko  ilivyo dhaniwa, naomba sana” Alizidi kuomba Lucia 

“Aah Lucia hilo jambo ni lazima tumshirikishe Mume wake, kama  unavyojuwa yeye ndiye msimamizi wa kwanza wa Mandy” Alisema  Daktari huyo 

“Hakuna haja ya kumuleza Desmond kuhusu hili jambo, naomba  asijuwe chochote kile” Alisema Lucia na kumfanya Daktari  ashangae, akamuuliza

“Kwanini hutaki ajuwe?” Nani atazilipa hizo gharama za  ziada?” Aliuliza 

“Kumbuka Mandy ni mfanyabiashara mkubwa sana hivyo akiamka  atalipia hizo gharama” Alisema Lucia katika hali ya kuendelea  kumuomba daktari akubali. 

“Asipoamka?” Aliuliza Daktari 

“Jukumu letu namba moja ni kuhakikisha wagonjwa wanapona, ni  lazima tufanye juu chini kuhakikisha tunasaidia Maisha yake”  Alisema Lucia akiwa anamtazama Daktari huyo ambaye alionekana  kuanza kumuelewa kidogo Lucia 

“Nakuamini Lucia usiniangushe katika hili, nitafanya kama  unavyosema” Alisema Daktari huyo, Lucia aliweka mikono  mdomoni kwa furaha kisha akasema 

“Asante sana Mkuu! Umenipa thamani kubwa sana” Alisema Lucia  kisha alimuaga Daktari akaondoka zake, daktari huyo alikuwa  Mzee na ilionesha ndiye mmiliki wa Hospitali hiyo 

“Aaah” Alisema Daktari kisha alipiga simu alipopajua yeye  akatoa maelekezo ya Mandy kupelekwa hatua ya pili ya  matibabu. 

••••••• 

Baada ya siku kama tatu kupita ilipatikana taarifa kutoka kwa  Askari polisi aliyekuwa akifuatilia kifo cha Mama Mandy,  polisi huyo alimpigia simu Desmond akamwambia kuwa kuna gari  iliyopatikana kwenye Bahari, gari hiyo ilikutwa na maiti ya  Mtu. Desmond alichanganikiwa, alikuwa ofisini kwake  akamuuliza polisi huyo 

“Gari! Maiti! Imefahamika gari ni ya nani na maiti ya Nani?”  Alihoji Desmond akiwa amesimama huku macho yakiwa yamemtoka  pima, alijuwa tu ni ile gari yake aliyomuulia Sanga, haraka  akiwa anasubiria jibu la Polisi huyo alijiuliza kama gari ile  ikitambulika kuwa ni yake itakuwaje? 

“Bado maiti imechukuliwa lakini kimekutwa kitambulisho cha  yule mfanyakazi wako ambaye alikuwa ni mhisiwa namba moja wa  Tukio la Mke wako ila mwili ulikuwa umeharibika hivyo imekuwa  ngumu kumtambuwa kwa macho. Mwili unafanyiwa vipimo kubaini  ni Nani” Alisema Polisi huyo 

“Vipi kuhusu gari imejulikana kuwa ni ya Nani?” Aliuliza  Desmond kama Mtu mwenye haraka ya kutaka kujuwa, polisi hakutia shaka sababu aliamini Desmond alihitaji kufahamu  sababu Mandy ni Mke wake pasipo kujuwa Desmond ndiye  aliyesababisha kila jambo na alikuwa akiwapiga changa askari  ili wasijuwe chochote kile, hata huyo Sanga aliyekuwa  akitafutwa ni yeye ndiye aliyemuuwa Hapo Baharini kwa kutumia  gari yake. 

“Kazi hiyo inafanywa na kitengo husika ili kubaini gari hiyo  ilikuwa ni ya nani, ndani ya dakika kumi zijazo tutajuwa gari  ni ya Nani pia tutapata taarifa juu ya mwili ule kama ni Wa  Sanga au ni wa Mtu mwingine tu” Alisema Polisi huyo kisha  alikata simu baada ya kuhakikisha kuwa alizifikisha taarifa  muhimu kwa Desmond akiamini ni Mtu mzuri anayepaswa kujuwa  kinachoendelea. 

Ofisini kwa Desmond hapakukalika mchana huo kila  alichofikiria hakikumpa jibu la moja kwa moja, alijuwa ni  lazima gari itajulikana kuwa ni ya kwake na polisi watamuhisi  kwa namna moja au nyingine jambo ambalo litasababisha aanze  kuchunguzwa kuhusu matukio taliyotokea, alizunguka ofisini  hapo huku akifikiria afanye nini. 

“Oooshit itakuwaje?” Alijiuliza sana Desmond, aliketi akaamka  akaketi tena huku akitazama saa ya ukutani, alihesabu hadi  dakika kumi alizoambiwa na yule polisi mpelelezi zilipokatika  kisha alishika simu yake huku akisubiria simu hiyo iite,  punde simu iliita na mpigaji alikuwa ni yule polisi, muda  aliosema kuwa atampa taarifa juu ya ule mwili pamoja na gari  uliwadia, taratibu aliipokea kisha aliiweka sikioni akiwa  amefumba macho yake 

“Desmond! Mwili ni wa Sanga mshukiwa namba moja, kesi inazidi  kuwa ngumu na kuhusu gari kuna fumbo zito sana hapa ambalo  linahitaji umakini hasa ukizingatia gari ile…” alisema  Polisi kisha Desmond alidakia 

“Ni ya Nani?” Alihoji kwa hofu kubwa sana, ukimya ulitawala  huku Desmond akisubiria neno kutoka kwa Polisi huyo, alisema 

“Haijulikani, mfumo hauitambui gari hiyo” Alisema Polisi huyo  kitu ambacho kilimshangaza sana Desmond, itakuwaje gari yake  isitambulike? Kibaya zaidi alikumbuka kuwa hakutoa chochote  kwenye ile gari ikiwemo kadi ya Gari kitu ambacho kingekuwa  rahisi sana kufahamika, pia alipokuwa akifanya hivyo alijuwa  wazi kina kile kirefu hivyo gari haiwezi kuonekana 

“Gari haitambuliki?” Alihoji Desmond akiwa na presha 

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TANO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

  

10 Comments

  1. Hee mbona nimesoma kwa dakika mbili leo
    Sehemu ya 4 ni fupi hivi!!?
    Afu Desmond kumbe alipoenda kijijini kwa kina Sanga kumbe alienda kumaliza uhai wake emmmah😢
    Anyway Asante kwa stori nzuri yenye mafunzo na maumivu ndani yake.
    More Love from Kenya ❤️

Leave A Reply


Exit mobile version