IlipoishiaKumbukumbu ya Desmond iliishia hapo, alitikisa kichwa chake  kisha alielekea ofisini kwa Daktari wa Hospitali, Daktari  alipomuona Desmond alijuwa nini kimemleta, Desmond alianza  kumshambulia Daktari huyo kwa maneno 

“Umeagiza Mke wangu apelekwe Wodi nyingine alafu Mimi  nizuiliwe kumuona si ndiyo? Hivi unajuwa ulichokifanya?”  Alisema Desmond kwa hasira 

“Desmond hebu kaa kwanza tuongee, hili jambo siyo la  kulichukulia jazba, tulichofanya ni kupandisha daraja  matibabu ya Mkeo ili aweze kuamka haraka ” Alisema Daktari  huyo kwa upole sana . Endelea 

SEHEMU YA SABA

“Kuamka haraka? Unajipa kazi ya Mungu si ndiyo? Unafikiri  Mimi sitaki Mke wangu aamke haraka? Nataka ila mlipaswa  kunishirikisha na sio sahihi kunizuia mimi kumuona Mke  wangu…Nitamuhamisha kwenye Hospitali hii haraka sana”  Alisema Desmond 

“Desmond naomba unielewe, Mkeo utamuona lakini siyo kama  zamani kutokana na aina ya matibabu ya sasa pia wodi  aliyopelekwa, nakuomba uwe mpole. Muhimu Ni afya ya Mkeo  Desmond” Alisema Daktari lakini Desmond alizidi kuwa juu 

“Natoa siku mbili Mke wangu awe amerudishwa kwenye wodi yake  aliyokuwa akikaa, vinginevyo nitamuhamisha hapa” Alisistiza  Desmond kisha aliondoka zake, lakini Daktari aliwaza sana  ikiwa Desmond anampenda mke wake kwanini akatae asipatiwe  matibabu kwenye wodi mpya? Kama gharama mbona wao ni  Mabilionea wakubwa tu 

Alipata wazo la kumtafuta Lucia ambaye alitoa wazo la Mke wa  Desmond kuhamishwa Wodi na kupewa huduma za daraja la juuu  zaidi, alimpigia simu akamwambia wakutane nyuma ya Hospitali  hiyo mahali ambapo palikuwa na Bustani. 

Mara moja walikutana huko, Daktari akataka kujuwa nini  ambacho kilikuwa kikiendelea na kwanini Lucia alitoa wazo  lile, ilionekana kuwa ni swali gumu sana kwa Lucia kumjibu  Daktari huyo akamwambia 

“Ni kwasababu ni Mgonjwa wangu ndiyo maana nilitaka apewe  matibabu ya haraka ili kumuamsha mapema” Alijibu akiwa  anatazama chini lakini akili ya uzee ya Dakatari Mkuu  ilimwambia kuwa Lucia alikuwa na jambo lingine kabisa 

“Unajuwa fika kuwa unaniongopea Lucia…Niambie ukweli, Lucia  wewe ni kama Binti yangu wa kumzaa tena hata Mjukuu wangu,  sura yako inaonesha dhahiri kuwa unnificha jambo…nyuma ya  pazia kuna nini?” Aliuliza tena Daktari huyo, alimpa nafasi  Lucia afikirie nini cha kufanya, mwishowe aliona ni bora  amfungukie daktari huyo, alimwambia 

“Nina mashaka Desmond akawa siyo Mtu mzuri kwa Mke wake  Mandy, juzi alikuja na mwasheria akamsainisha Mgonjwa kwa  alama za vidole, nilipouliza nilijibiwa kuwa sipaswi  kuingilia masuala ya kifamilia” Alieleza Luicia 

“Una uhakika?” 

“Nina uhakika na ndiyo sababu ya kukuonba Mkuu mgonjwa  ahamishwe daraja”

“Lakini inafikirisha sana sijui kuna nini nyuma yake. Ndiyo  maana nilikuja kukuuliza sababu Desmond aliwaka sana baada ya  kujuwa kuwa hawezi kumuona Mke wake. Hapo ndipo wasiwasi  wangu ulipoanza….Kaendelee na kazi Luicia tutaongea  baadaye” Alisema Mkuu huyo kisha alimtazama Lucia akitokomea  eneo hilo akiwa ndani ya mavazi ya kihudumu 

Baada ya kupita masaa kadhaa, Desmond alimuarika Mwanasheri  Joel kwenye moja ya Baa zenye hadhi, alihitaji kumueleza  kuhusiana na jinsi mambo yalivyokuwa 

“Kesi hii tukienda kichwa kichwa tunaweza jikuta tunafia  jela…” alisema Desmond akiwa anagida unywaji, joel akauliza 

“Kuna jambo jipya?” 

“Kuhusu gari yangu niliyomuulia Sanga kutokukutwa Eneo la  tukio badala yake kukutwa gari nyingine kabisa ikiwa na mwili  wa Sanga, tafsiri yake kuna Mtu wa tatu ambaye anaijuwa hii  inshu, pili ni kuhamishwa kwa Mke wangu na kupelekwa kwenye  wodi nyingine bila Mimi kupewa taarifa kisha nikazuiliwa  kwenda kumuona, ni ishara kuwa kuna bomu linaenda kulipuka”  Alisema Desmond akiwa anamtazama Mwanasheria Joel 

“Uuuupss!! Hata mimi taarifa ya gari imenivuruga sana, huyo  Mtu wa tatu ni nani hasa? Na kwanini hadi leo hajapiga simu  wala kutoa taarifa polisi?” Aliuliza Joel 

“Nashindwa kuelewa, kila ninapoliwaza jambo hili naishia  kukosa majibu ya kueleweka japo namtilia sana mashaka nesi  anayemuuguza Mke wangu, kuna bahasha amempa Mpenzi wangu  sijui kuna nini ndani yake napata ukichaa” Alisema Desmond 

“Desmond hii ni vita kubwa sana na mwisho wake hautokuwa  mzuri kama tunavyofikiria ni lazima tuwekeze nguvu na pesa  ili tumalize mizizi yote” Alisema Joel 

“Kesho kutwa ni siku ya kumvisha pete Noela, kama yule nesi  atakuja kwenye shughuli basi kila kitu kitaharibika, ni  lazima tumzuie asije” Alisema Desmond 

“Hiyo kazi niachie Mimi nitahakikisha hafiki kwenye shughuli  lakini wewe unatakiwa kuhakikisha unamtafuta Mtu wa tatu  aliyeona ukiwa unamuuwa Sanga Baharini, huyo ni Mtu hatari  sana na huwenda anajuwa kuhusu kifo cha Mama Mandy kuwa mimi  na wewe ndiyo wauwaji” Alisema Joel kisha alinyanyuka,  akachukua mkoba wake akapiga funda moja ya kinywaji akaiweka  glasi kwa nguvu juu ya meza kisha akaondoka zake pale.

Jioni Lucia alimpigia simu Noela wakati huo akiwa anarejea  nyumbani kwake akamuuliza kuhusu ile bahasha kama ameanza  kuifanyia kazi lakini Noela alizidi kumsistizia kuwa ni  lazima shughuli ya kuveshana pete ipite kwanza ndipo aifanyie  kazi, basi Lucia alikata simu akaelekea nyumbani kwao, akiwa  anaingia ndani aliiyona gari nyeusi ikiwa imesimama nje ya  nyumba yao, aliitazama lakini hakutia shaka kabisa, ndani ya  gari hiyo alikuwemo Mwanasheria Joel na kilichomleta pale  kilikuwa ni kuanza kazi ya kuhakikisha Lucia aendi kwenye  hiyo shughuli, baada ya kufahamu anapoishi Lucia, Mwanasheria  Joel aliondoka zake. 

Alimkuta Mama yake akiwa amelala, alikuwa mgonjwa hivyo  jukumu kubwa la Lucia lilikuwa ji kuhakikisha kuwa Mama yake  anakuwa salama, Maisha yao yalikuwa duni na yeye ndiye  tegemezi, alipitia huko chumbani na kumkuta Mama yake akiwa  amelala, alimfunika shuka kisha alitoka akaenda kuketi  sebleni. 

Alitafakari mambo mengi sana ikiwemo alichozungumza na  Daktari Mkuu kisha alikumbuka alichokiweka kwenye bahasha  aliyompa Noela, aliweka picha ya Desmond na Mwanasheria Joel  kisha aliambatanisha na maelezo ya alichotaka Noela akifanye,  alivuta pumzi zake kisha alijilaza kidogo pale pale Sebleni. 

Usiku ulipoingia, nyumbani kwa akina Noela na Mama yake  kulikuwa na shamra shamra sababu tukio la kuvishana pete  lilikuwa limekaribia, baadhi ya ndugu walikuwa wamefika pale,  sura ya Noela ilizidi kunawiri kwa tabasamu bila kujuwa kuwa  kulikuwa na vita kubwa iliyokuwa inapiganwa chini kwa chini,  Upande wa kule Hospitali matibabu yaliendelea kwa Mandy,  kukawa na tumaini kidogo lakini Desmond hakuambiwa chochote  kile sababu Tayari daktari Mkuu na Nesi Lucia walikuwa na  ajenda ya siri kuhusu uhai wa Mke wa Desmond aliyeitwa Mandy. 

Siku iliyofuata baada ya muda wa kazi kuisha, Lucia alimuomba  Noela waonane mara moja, walionana mgahawani majira ya  Mchana, ombi la Lucia likawa lile lile lakini Noela  alimsistizia kuwa hadi Shughuli ipite. 

“Lucia ni kesho kutwa tu navishwa pete, kama nilivyokwambia  sitawekeza fokasi kubwa kwenye kazi yako sababu nina shughuli  iache ipite kisha nitarudi kazidi na nitaanza na kazi yako”  Alisema Noela 

“Sawa Noela lakini ni muhimu sana ukafungua ile Bahasha”  Alisitiza sana Lucia

“Sawa nitafanya hivyo kwa ajili yako, nitahakikisha unafaulu  katika hilo jambo unalonipa kulifanya” Alisema Noela 

“Umesema ni kesho kutwa ndiyo unavishwa pete, nitajitahidi  ili nimuone shemeji yangu….kama sikosei ulisema anaitwa  Joshua” 

“Una kumbukumbu kama zamani, ndiyo anaitwa Joshua. Uje Lucia,  ni muhimu sana” Alisema Noela, waliachana baada ya kuwa  wamezungumza vya kutosha. Aliporudi nyumbani Noela aliketi  akajiuliza ni kwanini Lucia anasistiza sana afungue hiyo  Bahasha. 

Basi alielekea kwenye kisanduku chake cha kuhifahdia nyaraka  mbalimbali za kazi, ndimo alimohifadhi ile Bahasha  inayotafutwa na Desmond, aliitoa kisha aliishikilia akiwa  ameketi chini kando ya sanduku hilo 

“Mmh kuna nini humu mbona Lucia anasistiza sana nifungue?”  Alijisemea Noela ndani ya moyo wake, mwisho aliona ni bora  aifungue ili kuondoa ile lawama aliyokuwa akipewa na Lucia  kuwa anapuuzia kazi yake 

Alichana kwa juu kisha karatasi zikawa zinaonekana kwa juu,  akavuta karatasi moja lakini wakati anaivuta akaidondosha  picha ya Desmond Mwanaume ambaye anamjuwa kama Joshua na  ndiye Mtu anayetakiwa amfwatilie na kujuwa ukweli wa mambo  yaliyojificha na ndiye Mwanaume anayeenda kuvishana naye  pete, bahati nzuri picha iliangukia kwa kujifunika, nyuma  hakukuwa na maandishi yoyote yale. 

Aliiokota picha hiyo ikiwa imejifunika vile vile, moyo  ulianza kumdunda hata kabla hajaona picha hiyo, alijishangaa  sana lakini kabla hajaigeuza Mama yake aliingia chumbani  akamuona Binti yake akiwa katika hali ile ya waiswasi. 

Alimpokonya ile bahasha na picha kisha akavirudisha kwenye  ile Bahasha bila hata kuiangalia picha hiyo ya Desmond,  akaweka Bahasha kwenye sanduku hilo alilokuwa ameliacha wazi  kisha alilifunga. 

“Noela huu siyo wakati wa wewe kufanya kazi, mara nyingi kazi  zako zinakuumiza kichwa na kukufanya ukose raha. Huna haja ya  kuwa katika hali hiyo cha Msingi ni kuweka akili kwenye tukio  la kesho kutwa la kuvishwa pete na Mwanaume unayempenda”  

Alisema Mama Noela kisha alimnyanyua Mtoto wake 

“Unaenda kuwa Mke wa Joshua, ni jambo ulilolipigania kwa muda  mrefu hebu lipe kipaumbele, kazi zako utaendelea nazo baada  ya shughuli kupita sawa?”

“Sawa Mama” alijibu Noela kisha alitoa tabasamu, laiti kama  angelikuwa ameiyona ile picha basi mambo yote yangelikuwa  yameharibika maana angesoma kilichoandikwa na Lucia, angekuta  siri ya jina la Desmond kisha tuhuma nzito. 

“Haya twende” Alisema Mama Noela kisha alitoka na Binti yake  lakini akili ya Noela ilijikuta ikianza kuwaza ile Bahasha ya  Lucia. 

Naaam!! Desmond hakupotea Hospitalini sababu alijuwa fika  kuwa kwa huduma anazopewa Mke wake anaweza akaamka muda  wowote hivyo alihitaji kummaliza japo alizuiliwa kumuona,  alimtafuta Nesi Lucia akamwambia anahitaji kumuona Mke wake. 

“Lucia mnanitendea vibaya sana kwa kutoniruhusu nimuone Mke  wangu, wewe unajuwa ni jinsi gani nampenda Mke wangu na  nimekuwa hapa kila siku kuhakikisha afya ya Mke wangu inakaa  sawa” Alisema Desmond wakiwa wamesimama, hakujuwa kama Lucia  tayari alimuhisi vibaya 

“Sasa kipi bora Desmond, umuone Mke wako kila siku akiwa  katika hali ileile au usimuone ili afya yake ikae sawa ndani  ya muda mfupi? kumbuka Mkeo amekuwa hapa kwa zaidi ya miezi  mitano, hadhi ya maisha yenu hakupaswa kuwa kwenye ile wodi  wewe hukulioma hilo?” Alisema Lucia huku kila mmoja wao  akipigana vita ndani kwa ndani, Desmond alipokuwa akimtazama  Lucia alikuwa akijiambia kuwa lucia ndiye Mtu wa tatu  anayejuwa kila kitu huku Lucia akijisemea ndani ya moyo wake  kuwa ukweli utajulikana Desmond 

“Hilo ni sawa lakini kwanini maamuzi haya yamekuja ghafla tu  tena bila kunishirikisha Mimi? Hamjui ni kiasi gani nimeumia  mimi Lucia, nampenda Mke wangu Mandy” alisema Desmond akiwa  anatokwa na mchozi 

“Huna sababu ya kulia Desmond, ungekuwa unampenda Mke wako  usingemsainisha hati ya Makabidhiano ya Mali ukiwa na  Mwanasheria” Alisema Lucia, Desmond akashtuka sasa kuwa Lucia  ndiye aliyetoa hilo wazo la kuhamishwa kwa Mke wake baada ya  ile siku kumsainisha Mandy mbele yake 

“Anhaaa kwahiyo wewe ndiye uliyetoa wazo la Mke wangu  kuhamishwa?” aliuliza Desmond akiwa anafuta chozi kisha  aliweka tabasamu la kikatili, ile hali ya majonzi aliiondoa  baada ya kugundua kuwa anaongea na Mtu ambaye alikuwa  ameushtukia mchezo mzima. 

“Lucia hukupaswa kujiingiza huku kabisa kwasababu hujui  ilianzaje wala inaenda kuishaje, umefanya kosa kubwa litakalo 

kugharimu. Mama yako ni Mgonjwa, ni bora uweke Mawazo yote  kwa Mama yako kuliko kuweka kwa Mtu ambaye atakuja  kukugharimu” Alisema Desmond kwa sauti iliyokaza yenye  kumaanisha, Lucia alicheka chini chini kisha akamwambia  Desmond 

“Mwanzo nilikuwa nikikupenda sababu niliamini una mapenzi  mazito sana kwa Mke wako lakini baadaye nilikuchukia baada ya  kugundua kuwa wewe ni miongoni mwa waliosababisha yeye akawa  pale, nakuhakikishia Desmond, igizo unalofanya ukweli  utajulikana Mkeo akiamka” Alisema Lucia kisha alianza  kuondoka lakini Desmond alimshika mkono akamwambia 

“Una masaa 24 ya kutoka katika hili Lucia, Uwe na siku njema”  Alisema Desmond kisha kila mmoja alielekea alipopakusudia,  lakini Maneno aliyoyazungumza Lucia yalimtia ukichaa sana  Desmond akiwa kwenye gari aliwasiliana na Joel akamwambia  Wamuuwe Lucia kabla ya tukio la kuvishwa pete kwa Noela. 

Siku hiyo Lucia alizidi kuchanganikiwa sana, aliporudi  nyumbani kwao alichukua simu yake ambayo wakati anaongea na  Desmond alimrekodi ili aweze kuongeza ushahidi wa kumpa  Noela, alimtumia sauti hiyo ya mazungumzo Noela kisha  akampigia simu ili amuelekeze lakini Noela hakupokea simu,  maandalizi ya Tukio la kuvishwa pete yalikuwa yamepamba moto  sana hivyo hakuwa na muda wa kukaa na simu. 

Siku hiyo iliisha, siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku ya  kuvishwa pete kwa Noela, maandalizi yote yalifanyika pale  pale nyumbani kwao sababu hawakutaka Watu wengi, gharama zote  alizifanya Desmond. Usiku wa tukio Lucia alijiandaa, akamuaga  Mama yake akamwambia 

“Mama naenda kwenye sherehe ya rafiki yangu, sitochelewa  kurudi. Nakupenda sana Mama yangu” Alisema 

“Nakupenda pia Binti yangu, usijali nenda Mama nitakuwa  salama. ” alisema Mama yake Lucia, waliagana hapo kisha Lucia  alitoka. Alisimama Nje akimsubiria Mtu wa Pikipiki  aliyewasiliana naye kuwa aende kumchukua hapo na kumpeleka  nyumbani kwa akina Noela, alisimama kwa muda mrefu nje,  alipoona muda unazidi kwenda alianza kutembea taratibu ili  kama atakutana na Pikipiki aitumie, Ulikuwa ni usiku wa saa  mbili, baadaye likaja gari moja na kusimama mbele yake, Lucia  alijiuliza ni nani aliyesimama mbele yake. 

Kioo kilishushwa akaonekana Mwanaume mmoja 

“Samahani Dada unaenda wapi?” Aliuliza huyo Mwanaume

“Naenda mahali kwani vipi?” aliuliza Lucia maana alikuwa  amechukia kwasababu bodaboda wake alikuwa amendanganya kuwa  hayupo mbali kumbe yupo mbali 

“Sio vema Mtoto wa kike akatembea kwa mguu usiku huu,  naelekea barabara ya sita sijui wewe” Alisema Mwanaume huyo,  Lucia alifikiria akaona ajishushe tu kwa huyo Mwanaume maana  yeye alikuwa akielekea Barabara ya nne. 

“Naelekea Barabara ya Nne” Alijibu Lucia 

“Basi twende nikusindikize” Alisema Mwanaume huyo, Lucia  aliingia kwenye gari, safari ilianza kuelekea nyumbani kwao  Noela, wakiwa Barabarani mwanaume huyo alionekana kumtongoza  Lucia lakini Lucia hakuonekana kumkubali kisha alimwambia 

“Kama umenipa msaada ili unitongoze naomba unishushe Mimi  siyo Mwanamke wa hivyo” Alisema Lucia akionekana kuchukizwa.. 

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NANE

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

  

2 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version