Ilipoishia “Joshua naomba tuonane kwenye mgahawa muda huu” Alisema Noela  kisha alikata simu, Desmond alishusha pumzi zake baada ya  kujiridhisha kuwa Noela hajagundua lolote maana kama  angedungua asingemuita jina la Joshua bali angemuita Desmond,  kumbe Noela alishajuwa kila kitu, alikuwa katika upelelezi  wake binafsi 

Desmond alipotoka pale Hotelini moja kwa moja alienda kuonana  na Mchumba wake Noela kama alivyoambiwa, alimkuta Noela akiwa  amejawa na tabasamu na bashasha kitu ambacho kilimfanya  Desmond azidi kujiamini kuwa Noela hajafahamu lolote lile,  waliagiza chakula huku Noela akizidi kumsoma Desmond, akili  ya Desmond haikutulia kabisa sababu alihitaji kufahamu kama  Joel alikuwa amefanikiwa kupeleka Hundi ile kwa Mtu wa Tatu. Endelea

SEHEMU YA KUMI 

“Nimetoka Hospitali, unamkumbuka yule rafiki yangu uliyewahi  kuniona naye hapa?” aliuliza Noela makusudi ili kuzidi  kumsoma Desmond 

“Eeeh nakumbuka, anaumwa?” alihoji Desmond 

“Hapana amekutwa ameuawa huko porini, inasikitisha mno alafu  kaacha Mama anayeumwa sana” Alisema Noela huku akiwa makini  sana na jicho lake la uchunguzi, Desmond alishtuka mno huku  macho yake yakiwa yamemtoka pima kama Mjusi aliyebanwa na  mlango 

“Ameuawa…..Nani aliyemuuwa?” alihoji Desmond akiwa katika  hali ya kuchanganikiwa sana, Noela akagundua kuwa alichokuwa  ametumiwa na marehemu Lucia kilikuwa na ukweli mtupu 

“Haijajulikana, polisi wanafanya uchunguzi. Inasemekana pia  ameacha mgonjwa ambaye yupo mahututi na huyo mgonjwa  inawezekana kuwa chanzo cha kifo cha Lucia” Alisema Noela  huku jicho lake likiongeza umakini wa kumtambua Desmond 

“Mgonjwa!! aaah Noela, naomba tuachane na hizo stori,  tumekuja hapa kula Mpenzi” Alisema Desmond kisha alimwambia  Noela 

“Naenda chooni mara moja” Desmond alinyanyuka akaelekea  Chooni bila kujuwa kuwa Noela alikuwa tayari amegundua kuwa  yeye ni Muuuwaji 

Japo moyo ulimuuma sana Noela ila kilichompata Lucia alijiona  ana kila sababu ya kuleta haki, Desmond alipofika chooni  alijiinamia kwenye sinki la kunawia maji akiwa amechoka sana,  alianza kuhisi ugumu mkubwa sana kwenye Maisha yake,  alimpigia simu Joel akamuuliza kama amekutana na huyo Mtu wa  Tatu. 

Joel akiwa ndani ya gari hilo aliloelekezwa alipokea simu,  alionekana kuzungumza kwa kutulia sana huku pembeni yake  kukiwa na mwanaume mmoja 

“Nimeshampatia” Alisema Joel 

“Haya basi tukutane mara moja pale tunapokutanaga….naona  mambo magumu, Kifo cha Lucia kimekuja kuharibu kila kitu”  Alisema Desmond, baada ya simu ya Desmond kukatwa Joel  alimgeukia Mwanaume ambaye yupo ndani ya hiyo gani akamwambia 

“Ngoma imeanza kuchezwa, Hii Hundi hakikisha unachukua pesa  na kuziweka kwenye akaunti nyeusi, ni lazima tumtumie Desmond kuvuna pesa alafu kila kitu kitamuangukia mwenyewe” Aliagiza  Mwanasheria Joel, kumbe mwanasheria Joel ambaye ni  mwanasheria wa Mandy ndiye Mtu wa tatu ambaye alikuwa  akijifanya kuzunguka kwenye suala lililojificha ili apate  pesa kutoka kwa Desmond kwa kujifanya anajuwa siri za  Desmond, Mwanaume aliye pembeni yake ndiye yule ambaye  Desmond alikuwa akimtilia shaka na ndiye aliyekuwa akifanya  michezo mingi michafu na ndiye aliyelitoa lile gari kule  Baharini kisha akaliweka gari lingine kisha akawapigia simu  polisi 

Basi, Baada ya kumaliza kuongea na Joel akifikiria ni Mtu  mzuri anayeshirikiana naye alirudi kwa Noela ambaye  alijifanya yupo bize akipata chakula, angalau baada ya kutoka  Chooni alionekana kuwa sawa japo Noela alikuwa ameshamgundua  muda mrefu, walipata chakula ndipo Noela alipomchomekea  Desmond 

“Nasikia Mgonjwa wa Marehemu Lucia ameamka leo, ingekuwa  faraja sana kwa Lucia kumuona mgonjwa aliyemhudumia kwa muda  mrefu akiamka” Alisema kwa mtego Mkubwa sana na Desmond  akaingia mtegoni, alishtuka akauliza 

“Unamaanisha Mandy?” alihoji akiwa ameamka kutoka kitini,  ndipo sasa akawa amemdhihirishia wazi Noela kuwa ana Mke pia  ni Muuwaji 

Noela naye akaamka akijifanya kushangaa 

“Heee kumbe unamjuwa?” Alihoji Noela 

“Hapana….Hapana simjui, Noela tutaonana baadaye” Alisema  Desmond kisha aliondoka mbio kuelelekea Hospitalini bila  kujuwa kuwa alikuwa ametegwa, Haraka Noela alimfuata kwa  nyuma kisha naye aliingia kwenye gari yake akawa anamfuatilia  Desmond kwa nyuma, Safari hii ilifika hadi kwenye Hospitali  aliyolazwa Mandy 

Akiwa amepaki gari eneo lingine la Hospitali tofauti na  alipopaki Desmond, Noela alipokea ujumbe kuwa Mgonjwa Mandy  amerudisha fahamu, huu ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Daktari  Mkuu wa Hospitali sababu alimuachia maagizo kuwa akiamka  Mandy apewe taarifa na pia alipewa agizo moja kubwa sana,  Noela akakumbuka alichomwambia Daktari 

Alimwambia kuwa anafanya uchunguzi wa kifo cha Lucia na  huwenda mgonjwa huyo akawa ndiyo chanzo cha kifo cha Lucia  hivyo atakapoamka pengine kuna siri anaifahamu hivyo kitu cha  kwanza ahakikishe anamuweka sawa kiakili ili Desmond  asishtuke mapema hadi pale watakapopata ushahidi wa kutosha

Akiwa mbio mbio, Desmond alifunga breki miguuni mwa Daktari  Mkuu aliyekuwa akitoka wodini kwa Mandy 

“Dokta nimesikia Mke wangu ameamka” Alisema Desmond akiwa  katika hali ya haraka na hofu mno 

“Ndiyo Mkeo ameamka ila bado hana nguvu, unaweza ukamuona ila  usimkumbushe chochote” Alisema Dokta, Basi Desmond aliufungua  mlango wa wodi hiyo, kweli alimuona Mandy akiangaza huku na  kule kama Mtu aliyekuwa akijiuliza yupo wapi 

Hofu ilimjaa sana Desmond kisha alimsogelea Mandy taratibu  huku akiwa mwenye maswali mazito sana ya kuwa Mandy amemjuwa  Desmond kuwa ni Muuwaji wa Mama ake, Mandy alipomuona Desmond  alionekana wazi kuwa na maumivu makali moyoni, alimtazama  Desmond huku chozi likimbubujika, yule Daktari Mkuu alisimama  mlangoni akichungulia tu 

Mandy alikumbuka siku ya tukio la yeye kupigizwa ukutani na  Desmond, siku hiyo ilikuwa hivi, aliiyona cheni ya Mama yake  kwenye koti la suti la Desmond, cheni ambayo Desmond aliivua  kwenye shingo ya Mama Mandy baada ya kumuuwa kisha akaiweka  kwenye koti lake, Mandy alipoiyona ile cheni ndipo  alipogundua kuwa Desmond ni Muuwaji, wakati anapiga Simu  Desmond alitokea ndipo vurugu za kufukuzana zilipoanza 

Tuendelee, Basi Desmond alisogea na kumshika mikono Mandy  akamwambia 

“Umeamka Mama?” alihoji Desmond 

“Wewe ni Nani?” aliuliza Mandy, Desmond alishtuka sana kisha  akajiuliza ina maana Mandy amepoteza kumbukumbu zake,  alijikuta akitabasamu maana kama amepoteza kumbukumbu  hatoweza kumtaja kama Muuwaji wa Mama yake. 

“Pole kwa maumivu sawa Eeh!! Mimi ni Mume wako Desmond”  Desmond alijitambulisha pale, Daktari alielekea moja kwa moja  kwenye maegesho ya Magari akamwambia Noela kuwa Mandy  amefanya kama alivyoagizwa yaani kujifanya amepoteza  kumbukumbu. 

“Safi sana, Desmond ni mchumba wangu na hii pete amenivisha  jana tu” Alisema Noela kisha aliivua pete hiyo 

“Sistahili kuwa na pete yake sababu ni Mume wa Mtu pia  Muuwaji, kwakuwa ameshajulikana ndiye Muuwaji basi kazi  iliyobakia niachie Mimi” 

“Sawa!!” Noela aliondoka Hospitalini hapo.

Desmond alibakia Hospitali kwa ajili ya kuangalia kama kuna  chochote Mandy anaweza akakumbuka, hii ilimfanya yule Daktari  ashindwe kumpa taarifa muhimu Noela. 

Jioni ilipoingia ilimkuta Noela akiwa nyumbani kwao akiwa  kwenye tafakari nzito kuhusu Desmond ambaye alimdanganya jina  kama Joshua, alikumbuka vingi ikiwemo walipotoka, alijikuta  akiangusha chozi lenye maumivu makali sana, mapenzi aliyompa  Desmond yalikuwa ya dhati sana kwa kipindi chote, kugundua  kuwa Desmond alikuwa Muuwaji na Muongo kulimliza sana Noela. 

Alijikuta kwenye wakati mgumu sana, ndiyo alimpenda sana  Desmond hadi kufikia hatua ya kuvishwa pete lakini angefanya  nini wakati Mwanaume huyo alikuwa Muongo na Muuwaji. 

Jioni hiyo alitoka akarudi kule Hospitali, Desmond alikuwa  wodini kwa kipindi chote akiwa na mawazo kuwa huwenda Mke  wake atarudisha kumbukumbu muda wowote ule, ili kumtoa pale  Noela alimtumia meseji Desmond akimwambia 

“Mpenzi naelekea kwenye pori ambalo Lucia aliuawa, kuna  taarifa kuwa alipotoka nyumbani kwao alitoka na kitabu chenye  siri pengine nacho kilikuwa ni sababu ya kifo chake,  inasemekana kilipotea porini” Alipotuma meseji hiyo alijuwa  wazi kuwa Desmond ataenda huko porini ili kuhakikisha  alichoambiwa, kweli muda huo huo Desmond alikurupuka kutoka  pale wodini akaingia kwenye gari kisha akatoka. 

Lakini wakati anatoka Desmond, yule Mwanaume anayetumwa kazi  na Mwanasheria Joel alikuwa pale ndani akamuona Desmond  akitoka kisha Noela aliingia wodini, yule Mwanaume alimpigia  simu Joel haraka sana akamwambia alichokiona, basi haraka  Joel alimpigia simu Desmond na kumueleza kuwa kulikuwa na  mchezo uliokuwa ukichezwa hapo na kwamba mpenzi wake Noela  alikuwa hapo Hospitalini na baada ya yeye kutoka Mpenzi wake  huyo aliingia wodini kwa Mke wake Mandy. 

Desmond alisitisha safari ya kwenda eneo ambalo Lucia aliuawa  baada ya kuambiwa kuwa kuna mchezo mchafu Hospitalini, haraka  aligeuza gari akarudi kule Hospitalini, akiwa hoi hai  aliingia wodini na kumkuta Mandy akiwa amelala huku chumba  hicho kikiwa kimya sana, Desmond alishangaa sana wakati  aliambiwa na Joel kuwa mpenzi wake alikuwa hapo, akaamuwa  kumpigia simu ili ajihakikishie alichoambiwa, simu  ilipopokelewa ilionesha wazi kuwa Noela alikuwa barabarani  hivyo alishindwa kuthibitisha alichoambiwa, alimpigia simu  Joel na kumwambia alichokiona lakini Joel alimtaka Desmond  kuwa makini sana maana Mpenzi wake alikuwa hapo Hospitalini  na huwenda anafahamu kuhusu Mandy.

Alienda kukutana na Mwanasheria Joel ambaye alikuwa  akimchezea Mchezo mchafu, Joel alimuonesha video Desmond  iliyomuonesha Noela akiingia na kutoka pale wodini, ndipo  alipopata picha kamili kuwa Noela alikuwa amefanikiwa  kumfahamu, Joel alimuuliza 

“Huyo ameshajuwa siri kuwa wewe ni Muuwaji, kibaya zaidi huyo  ni mpenzi wako alafu mpelelezi utafanya nini?” Desmond alikaa  kimya baada ya sekunde kadhaa akamwambia 

“Nitajuwa cha kufanya” Desmond alitoka kuonana na Joel,  alionekana kuwa mwenye mawazo sana ya nini afanye, alimpigia  simu Noela akamuuliza kama alifanikiwa kukipata hicho kitabu,  alifanya hivyo makusudi ili kumfanya Noela afahamu kuwa bado  Desmond hajajuwa chochote. 

Noela alimwambia kuwa hawakufanikiwa kukipata kitabu ila  uchunguzi bado unaendelea, Desmond alipata wazo la haraka  nalo ni kuondoa uhai wa Noela maana Mke wake hakumbuki  chochote hivyo kwa vyovyote Mtu anayeweza kusema ukweli ni  Noela. 

Alimtunia ujumbe wakutane nyumbani kwake usiku wa siku hiyo,  baada ya kuupata ujumbe Noela aliwataarifu polisi aliokuwa  akifanya nao kazi maana alihisi huwenda Desmond alishafahamu  kuwa anaijuwa ile siri ya Mauwaji. Usiku ulipofika Noela  alienda nyumbani kwa Desmond, alimkuta akiwa ameketi mahali  anapata bia 

Noela aliketi naye akapata chupa ya Bia bila hata kumsemesha  Desmond, waligida kidogo kisha Desmond alimuuliza Noela 

“Umemuaga Mama?” 

“Ndiyo!!” Alijibu Noela 

“Siku moja ya uchumba wetu umeshavua pete ya uchumba” Alisema  Desmond ndipo Noela aliposhtuka sasa kuwa Desmond alikuwa  ameshafahamu. 

“Nafikiri ni kitu cha kawaida, inakuwaje kwa Mtu akawa na  majina mawili, la uhalisia analificha na kutumia jina feki?”  Alisema Noela, hakukuwa na siri tena sababu kila jambo  lilikuwa wazi 

“Noela umekuwa kikwazo kwangu, ili niwe salama ni lazima  nikutangulize” Alisema Desmond kisha alitoa bastola akawa  anaifutafuta

“Kwa mpelelezi ambaye amefanya kazi nyingi hawezi kuogopa  kufanya kazi hata kama ni hatari kiasi gani au inamgusa  ampendaye, Desmond….kumbe una Mke tena ni Mke ambaye  ulitaka kuutoa uhai wake kisa pesa, unakumbuka kuhusu Mama  Mandy?” aliuliza Noela, Desmond alijawa na hasira  akamnyooshea Noela 

“Kabla hujaniuwa Desmond, nataka nikwambie kitu kimoja. Pesa  haiwezi kukupa kila kitu katika Maisha yako, ila Maisha  yanaweza kukupa kila kitu ikiwemo na pesa, waliochagua kuishi  walifanikiwa lakini wewe ulichagua pesa ili uishi” 

“Ishia hapo hapo Noela” Alisema Desmond kisha alifyatua  risasi iliyowashtua polisi aliokuja nao Noela 

Haraka waliingia na kumkuta Noela akiwa chini anaugulia  maumivu ya bega, bastola ikawa udhibiti kwa Desmond,  alikamatwa na wale polisi. Taarifa ya kukamatwa kwa Desmond  ilimfikia Joel, akapata wazo la kuikimbia Nchi maana  alishajuwa kuwa atatajwa na kukamatwa, Naam!! alitajwa na  Desmond, Joel alienda kukamatwa Uwanja wa ndege…. 

Taarifa ya kukamatwa kwa Joel na Desmond ilimfanya Mandy alie  kwa uchungu mkubwa, baada ya kupona kwa Noela, Desmond na  Joel walifikishwa Mahakamani kwa makosa ya Mauwaji, Mandy  alisimama kama Shahidi namba moja, Hatimaye Desmond na Joel  walifungwa kifungo cha Maisha jela, Mandy alimshukuru sana  Noela kwa msaada huo hadi kukamatwa kwa Wauwaji 

Noela aliishia maisha ya majuto sana sababu aliamini kama  angelifanyia kazi mapema bahasha aliyopewa na Lucia basi  rafiki yake huyo asingeliuaawa 

MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

  

5 Comments

  1. Mapenzi na Maumivu ❌❎
    Mapenzi ni Maumivu ✅
    Na Pesa sio kitu
    Utu ndio kila kitu.
    Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na mazingatio katik maisha yetu ya kila siku hususan maisha yetu ya saiv.
    Asanteni.
    Mtunzi na Admin❤️

Leave A Reply


Exit mobile version