Liverpool wametikisa Europa League kwa kufurahia “usiku kamili” ambapo waliweka wavuni mabao matano, kuimarisha nafasi yao kama timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo, kutoa fursa kwa wachezaji wawili wapya kucheza na kusahau kosa kubwa la msimu.

Kwenye uwanja wa Anfield Alhamisi, Liverpool walioonesha ukatili waliwafunga mabao 5-1 washindi wa Kombe la Ufaransa, Toulouse. Sasa, kulingana na kiungo wa zamani Joe Cole, “wanapaswa kushinda michuano hii.”

Baada ya kuonyesha mchezo wa kushambulia na kutoa burudani nyingine, Liverpool wameshinda mara 10 kati ya mechi 13 walizocheza msimu huu na kuendeleza rekodi yao ya kushinda katika Kundi E la michuano ya pili ya Ulaya.

Kwa sehemu kubwa ya muda tulikuwa na udhibiti kamili,” alisema meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp. “Tulifunga mabao mazuri, hakuna mtu aliyepata majeraha, usiku kamili.”

“Mimi nadhani ni rahisi sana kuupenda kikosi hiki. Kuna msisimko mwingi ndani yake. Tunapaswa kufanya maendeleo makubwa, tunapaswa kukua, tunapaswa kufanya mambo mengi – lakini ishara nyingi ni nzuri sana.”

Baada ya kuanza vizuri, Liverpool itaendelea hatua ya mtoano ikiwa itashinda dhidi ya Toulouse katika mchezo wao ujao wa Europa League baada ya wiki mbili.

Liverpool wako katika michuano isiyo sahihi kwao. Kama wangekuwa Ligi ya Mabingwa, tungekuwa tunasema wanaweza kufika mbali,” aliongeza Cole, kiungo wa zamani wa England aliyeonekana kuvutiwa.

“Wanapaswa kushinda michuano hii kwa sababu kitu kingine chochote hakitoshi.

Liverpool wameshinda Europa League mara tatu na mara ya mwisho walichukua kombe hilo mwaka 2001 wakati ilikuwa Uefa Cup.

Baada ya filimbi ya mwisho, Nahodha msaidizi Trent Alexander-Arnold aliiambia TNT Sports kwamba ni “michuano tunayoitilia uzito na watu watayaona hayo.”

Liverpool ndio mabingwa wa kupewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo huko Dublin mwezi Mei, na hata baada ya kufanya mabadiliko nane kwenye kikosi kutoka kile kilichoshinda dhidi ya Everton katika Ligi Kuu mwishoni mwa wiki, waliionekana kuwa bora kuliko Toulouse.

Cole aliiambia TNT: “Hali hii inatisha kwa Europa League na Ligi Kuu. Wanacheza kwa kasi. Mara Liverpool wanapopata kasi, ni vigumu kuwazuia.

Unaweza kuona timu hii ikifika mbali sana katika kila michuano Nyakati nzuri zimerudi Wamefikaje katika michuano hii?”

Mshambuliaji wa zamani wa England, Eni Aluko, aliongeza: “Inaonekana kama Liverpool ni kubwa mno kwa michuano hii, bila kudharau wengine Hii ndiyo unayoitazamia, wanapaswa kutawala.”

“Kugusa kwanza ni ya kipekee, [vilevile] kasi yake na mpira,” Klopp aliongeza.

“Hajafikia nusu ya njia bado Jambo zuri ni kwamba ana mambo mengi ya kuboresha.” kijana Luke Chambers 

“Tuna vijana wengi wazuri na tunawaamini,” alisema Klopp.

“Katika nyakati nzuri, unaweza kuwapa vijana fursa.

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version