Wachezaji wa Simba SC wamefanya mazoezi kabla ya mechi yao ya ugenini katika Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumamosi dhidi ya Wydad Club Athletic ya Morocco.

Mechi kati ya Yanga na Medeama FC itafanyika katika Uwanja wa Baba Yara huko Kumasi, Ghana, kuanzia saa 1 usiku saa za Tanzania.

Timu hizo mbili zitacheza mara ya tatu katika historia yao na Medeama SC wamefanikiwa kung’ara dhidi ya Yanga.

Kocha wa Young Africans (Yanga) Miguel Gamondi amesema kuwa timu yake itacheza kwa azma kubwa dhidi ya Medeama SC katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika siku ya Ijumaa.

Mechi ya Yanga-Medeama FC itafanyika katika Uwanja wa Baba Yara huko Kumasi, Ghana, kuanzia saa 1 usiku saa za Tanzania.

Timu hizo zilikutana Julai 26, 2016, katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF na matokeo yalikuwa 1-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, huku katika mechi ya marudiano nchini Ghana, Medeama SC walishinda 3-1.

Kusudio letu ni kupata matokeo chanya katika mchezo huu. Najua tunakabiliana na changamoto kubwa ugenini dhidi ya timu inayolenga ushindi pia,” alisema.

Kulingana na Gamondi, mchezo huu ni muhimu sana kwa upande wake kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

Mpaka sasa, Yanga wamekusanya alama moja tu katika kundi D baada ya sare ya 1-1 Jumamosi iliyopita dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha wa Yanga alifafanua kuwa timu yake itacheza kwa nidhamu kubwa, wakilenga kuibuka washindi.

Tunahitaji kupambana licha ya kucheza ugenini Na pia tunahitaji kuheshimu wapinzani wetu,” alisema.

Wakati huo huo, Simba waliondoka jana kuelekea Marrakech, Morocco, kwa ajili ya mchezo wao muhimu dhidi ya Wydad Club Athletic.

Mchezo wa Simba-Wydad unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Stade de Marrakech nchini Morocco na utaanza saa 4 usiku saa za Tanzania.

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version