Ni mashariki mwa Afrika sehemu ambayo Bahari ya Hindi imepita, nchi ambayo imefunikwa na maeneo makubwa yenye mito na maziwa, ardhi yenye udongo wenye rutuba na vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na safu za milima na mabonde.

Tanzania nchi yangu, hii ndiyo fahari yetu sote, tunajivunia nawe kwenye pande zote za duniani, na ndiyo maana halisi ya Soka la nyumbani limenoga, tumeungana watu wa rika tofauti kuitazama burudani hii ya Kabumbu popote pale nchini, wazawa na wageni kwenye Ligi yetu wanatupa Ladha ya Ligi kuu pamoja na Championship.
Wacha leo niwaambie nikiwa kwenye ardhi ya Chief Mkwavinyika Mwinyigumba, naamini hata watoto na wajukuu wa Kinjekitile Bokero Ngwale wataisikia, msimu ujao unatarajiwa kuwa mgumu sana kila timu inahitaji kufanya vizuri usajili umefanyika na timu zote kambini maandalizi ya msimu mpya.

Zaidi ya miaka minne sasa wageni wamekuwa Lulu nchini, sifa mbwembwe wamekuwa wakipewa wao, ni wakati sasa na sisi wazawa kuonyesha ubora wetu, uwezo Ufundi na vipaji tunavyo vya kutosha, kwa sasa hatuhutaji kupendelewa Bali wazawa wanahitajika kupambana zama zinakwenda sana muda unasonga mbele, uwekezaji umeongezeka watu wanaweka hela.

Vituo mbalimbali vinafunguliwa vijana wanafundishwa na vipaji mitaani vinaonekana, hakuna haja ya kupunguza idadi ya wageni 12 wanatosha sana na Wala siyo wengi, kilichobora ni kupambana na kujituma ukionyesha uwezo jitihada hakuna Kocha atakunyima nafasi kosa kuna wageni.

Mara ngapi tumeshuhudia wageni wakiwekwa benchi na wazawa, mara ngapi vijana wamepambana mbele ya wageni na wakatoboa na kuwa na nafasi ya uhakika ya kucheza mbele ya wageni? Vijana wangapi wamekwenda kucheza Soka la kulipwa kupitia Ligi ya nyumbani. Ni wakati sasa wa kuendelea kupambana Feisal Salum, Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathiri Yahya Pascal Msindo ni baadhi ya wazawa wanaopata nafasi kwa kuwaweka wageni kwenye mbao ndefu.

Nikukumbushe kuwa Saimon Msuva, Himid Mao walipata nafasi ya kucheza nje ya nchi kupitia Ligi ya nyumbani, hakuhitaji kutafutiwa nafasi ya lazima ili wazawa wacheze. Mnaocheza Ligi kuu sasa Academy ni nyingi sana nchini vijana wanawaangalia nyie kama kioo chao, wanawatazama kama watu wenye ushawishi mkubwa sana kwao na kuwafanya kuwa na matamanio makubwa kupitia nyie.

Ni wakati sasa kuwaonyesha kuwa wazawa wanaweza hakuna haja ya kuonekana wanatafutiwa nafasi maana wana ubora wa kushindana na wageni.

Wageni wamefanya Ligi yetu kama daraja kwao kufika mbali Kimataifa tena kwenda kwenye vilabu vikubwa barani Afrika na Mfano halisi Upo Kipre Junior, Luis Miquisone, Fiston Mayele wamekwenda vilabu hivyo baada ya kuonyesha uwezo wakiwa nchini sasa kwanini isiwezekane kwetu?
Mimi sina mengi sana Wacha niwaache na hayo machache tu ila Imani yangu ni kuwa wazawa wana uwezo tu mkubwa na ilo kadri miaka inakwenda taratibu wanadhihirisha ilo.

SOMA ZAIDI: Baada Ya Usajili Tuitegemee Yanga Ya Namna Gani Msimu Huu?

4 Comments

  1. Pingback: Misingi Sahihi Ya Wachezaji Vijana Ni Elimu Ya Makocha

  2. Wafate nyayo za Fei toto. Zanzibar finest huyu ni balaaa kwa washambuliani wote wamuige Fei. Ila kwa beki pia Kuna kijana kutoka kwenye vikosi SI mengine ni Ibra Bacca huy ni beki Bora sana kwa Sasa kakita viunga vya NBCPL. Wasimsahau dogo mmoja matata kutoka azam anakichafua sana katika ENEO la kiungo. Ni kiungo halisi kabisa jina nimemsahau kidog ila hachafuki Wala hana fujo uwanjani ila kazi yake usipme ni noma (bitegeko)

  3. Pingback: Hatukatai Umefanya Vingi Ila Hili Ni Deni Kubwa Sana Kwako

  4. Kaka hapo si wazawa tatizo viongozi, pili wazawa washajiona watawa especially hao wanaojiita wakongwe kongole kwa simba kwa kuvua ndaga na kuwaachaa kambale wenye ndevu

Leave A Reply


Exit mobile version