Ligi kuu ya NBC imefikia mzunguko wa 22  ikiwa ni raundi ya pili ya msimu huu 2023/2024 msimu ambao umekuwa na mabadiliko makubwa sana kuanzia viwanja, udhamini kwa vilabu, jezi na namna ya uchezaji kiwanjani.

Lakini pia ndiyo msimu ambao umeshuhudia ukiwa na wageni wengi waliyoonyesha ubora wa kiwango kile ambacho muda mrefu tulitamani kukiona, siyo kwa wageni wa Simba na Yanga tu bali hata Tabora Utd, Azam FC, Coastal Union, Ihefu FC, Singida FG na Kagera Sugar. Huu ndiyo msimu ambao wachezaji wageni wameonyesha maana halisi ya wao kuvuka mipaka hadi ardhi yenye mlima mrefu Kilimanjaro mbuga bora na yenye hadhi Afrika ya Serengeti.

Wachezaji wengi kwa nafasi mbalimbali wameonyesha viwango bora na kuileta maana halisi ya Ligi namba 6 za ubora barani Afrika, siyo golikipa, mabeki, washambuliaji na viungo wote wameipa hadhi ya namba sita. Mpaka sasa magolikipa wengi wageni wamekuwa bora Djigui Diara wa Yanga SC akiwa na “Clean sheet” tano, John Noble wa Tabora Utd, Jonathani Nahimana wa Namungo au kinara wa “Clean sheet” Matampi kutokea Coastal Union na wala siyo Ayoub Lakred wa Simba SC wote wameidhaminisha Visa ya kuingia Tanzania kuwa ni halali kwao.

Uwepo wa wageni wengi kwenye ligi kuu umewapa nafasi makocha wao kufanya vizuri kwani wachezaji waliyonao wamekuwa bora wakisaidiana na wazawa baadhi, hakuna kocha ambaye haitji huduma ya Henock Inonga na Che Malone wa Simba SC, Benjamini Tamimu wa Ihefu FC, Duke Abuya au Yao Attouhala, Clatous Chama, Max Nzengeli na Joyce Lomalisa wa Yanga SC ni wakati wa kujivunia uwepo wao kwenye Ligi yetu imeongeza ubora wa baadhi ya vilabu vyetu na hiyo ahitaji kuficha.

Moja ya nafasi ambayo wageni wameitendea haki kwa msimu huu ni Kiungo, inaweza ikawa huu ndiyo msimu ambao Ligi yetu imepata kuwa na viungo wengi wazuri kuliko misimu yote tokea kuruhusiwa kusajili wageni kwenye vilabu vyetu, haina haja ya kubisha sana wala kuweka mjadala kwani takwimu zao zinajieleza kuanzia kufunga hadi kutengeneza magoli wakati pekee wa kufurahia uwepo wao kwani wengi wao ndiyo sehemu ya wachezaji muhimu kwenye vilabu vyao.

Orodha ya wanaongoza kwa kufunga magoli ligi kuu imeshikiliwa na viungo wengi kuliko washambuliaji  kwenye 10 bora kuna wachezaji saba wa kigeni huku watano kati yao wakiwa ni viungo wakiongozwa na Stephane Aziz Ki wa Yanga SC mwenye magoli 5 akifatiwa na Max Nzengeli wa Yanga SC na Marouf Tchakei wa Ihefu FC wenye magoli 8, Kipre Junior wa Azam FC naye akiwa na nane na Jean Baleke wa Simba (ambaye hivi sasa hayupo kikosini.

Nje ya kufunga orodha wa kutengeneza magoli inaongozwa na wageni watatu Kipre Junior wa Azam FC akiwa na “Assist” 8  akifatiwa na Yao Attohoula wa Yanga SC na “Assist” 7 , takwimu zao ni nzuri lakini nje ya takwimu hizo wamekuwa na kiwango bora kuanzia namna ya uchezaji wao imekuwa bora sana hakuna mpenda soka ndani ya nchi hii asiyefurahia sana yao ya uchezaji kiwanjani ni fahari kwetu wazawa kumiliki wachezaji wa kigeni wenye uwezo nzuri kama msimu huu, imetupa nafasi ya kujivunia nafasi 12 ya ruhusa ya kuwa na wageni kwenye timu.

Namna wanavyocheza na viwango wanavyoonyesha ni dhahiri kuwa kuna nafasi kubwa Tuzo ya Mchezaji bora, Kipa Bora pamoja mshambuliaji bora (mfungaji bora) basi zikachukuliwa na wachezaji hao na hata watakaowania kwa kiasi kikubwa idadi Ya wachezaji wengi watakuwa wageni.

Hata hivyo uwepo wao imesaidia kuongeza jitihada kwa wazawa wetu kupambana na kuamini wanaweza imekuwa chachu kwao kupambania namba na baadhi yao imewapa nafasi ya kwenda nje ndani ya msimu huu, jicho langu laona huu msimu wageni watachukua Tuzo nyingi sana mwisho wa msimu ila uzuri ni kuwa wamekuwa bora sana na ilo halijifichi kwa nafasi tatu ambazo ni kipa, beki na viungo.

SOMA ZAIDI: Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba Sc 

4 Comments

  1. Kozi Bora
    1. Diara djigue 🔥
    2. Yao attohoura🤕
    3. Lomalisa mtambala🤑
    4. Bacca Ibrahim 👐
    5. Inonga 🐖
    6. Aucho Khalid
    7. Nzengeli max mpira 😎
    8. Feisal Salim🤛
    9. Wazili junior🤝
    10. Ki 😆🔑🗝️
    11. Pacome 😷

    Sub.
    1. Ayoub
    2. Lusajo m.
    3. Msindo
    4. Job
    5. Lawi
    6. Jakaminko
    7. Kibu
    8. Mudathiri
    9. Adam adam
    10. Mzize
    11. Silla

    ✍️ ttraveller347@gmail.com

    • SIMBA
      Lakreed
      Mwenda
      Mohammed hussein
      Che malone
      Innonga
      Mzamiru
      Kanoute
      Ngoma
      Kibu denis
      Chama
      Onana
      Substitution:::::
      1:Ngoma
      2:Kennedy juma
      3:Ally salim
      4:Jobe
      5:Hussein kazi

Leave A Reply


Exit mobile version