Ligi kuu ya nchini Hispania inaendelea tena leo kwa Las Palmas akimkaribisha Barcelona katika mchezo unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 5 za usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Gran Canaria.

Las Palmas anaingia katika mchezo huu akiwa nafasi ya 10 ambapo katika mechi 18 amejikusanyia alama 25 huku katika michezo yake 5 ya mwisho akishinda michezo 3 akipoteza mmoja na kusare mmoja.

Barcelona yeye anaingia katika mchezo huu akiwa amejikusanyia alama 38 katika mechi 18 alizocheza huku katika mechi zake 5 za mwisho kucheza akishinda mechi 1 pekee na kusare mechi moja na kupoteza mechi 3 huku kati ya hizo mechi 3 mechi 2 akipoteza mfululizo.

Mechi hii wakali wa Catalunya wanapewa nafasi kubwa ya kushinda na hii ni kutokana na mechi ambayo inawakutanisha na Palmas wamekua wakiibuka na ushindi huku mechi iliyokua na magoli mengi zaidi ni mwaka 2017 akimpa kipigo cha bao 5:0 na mwaka 2001 akimfunga bao 4:1.

Wakiwa nyumbani Palmas wamepoteza mchezo mmoja pekee kwa 1:0 dhidi ya Rayo Vallecano huku akisare dhidi ya Cadiz na kushinda mitatu akimpa kipigo Getafe , Atletico Madrid na Celta Vigo.

Licha ya kupewa nafasi kubwa ya ushindi Barcelona amekua hayuko vizuri viwanja vya ugenini akishinda mchezo mmoja pekee kwa bao 1:0 dhidi ya Real Sociedad lakini akisare mechi mbili na kupoteza 2.

VIDOKEZO VYA UBASHIRI

Kwa jinsi ilivyo mechi hii ni vyema kwenda na magoli zaidi kwani bado ni kama Barcelona anajitafuta zaidi hivyo ni (Goals Over 1.5)

Lakini pia unaweza kuamua kumpa Las Palmas asipate magoli zaidi ya ma 4 ( Palmas Goals Under 3.5)

Endelea kufuatilia zaidi vidokezo vya ubashiri katika mechi mbalimbali kwa kugusa hapa.

1 Comment

  1. Pingback: Sevilla vs Athletic Bilbao : Ubashiri Na Vidokezo Vya Mkeka - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version