Klabu ya Petro Atletico de Luanda kutoka nchini Angola ni miongoni mwa zile timu ambazo zimefuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kama ulikua hujui tu ni kuwa hawatajwi sana lakini ni wana balaa sana katika michuano.

Hii inakua timu ya kwanza kumaliza hatua ya makundi bila kuruhusu bao lolote katika nyavu zao. ambapo wamecheza mechi 6 ambapo wameshinda mechi 3 na kupata sare 3 na zaidi sana nikuwa wamefunga mabao matano hawajaruhusu bao lolote kwenye nyavu zao.

Golikipa wao H.Margues ndiye mlinda lango mwenye clean sheet nyingi kwenye michuano hii ya mabingwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu ambapo mpaka sasa akiwa na clean sheet 6 kwenye michezo 6 aliyocheza.

Hawa Petro ni moja ya timu ya kuchungwa sana, katika harakati za kumkwepa Mamelodi basi na huyu Petro sio mtu wa kukutana naye. Petro ndiyo wanabeba ramani ya Angola katika michuano ya CAF barani Afrika na kwa misingi mingi wameiwakilisha vyema Angola Na msimu huu.

Malengo yao yanaonekana wanalitaka kombe lenyewe na hawajawahi kuwa wanyonge kwenye michuano hii. Nikiri wazi kwa kusema kuwa hii ni moja ya timu yangu pendwa kwenye hatua ya makundi japokua mpaka sasa naweza kusema kuwa kwa jinsi ambavyo michuano hii ilivyo ni ngumu sana kumtambua bingwa wa msimu huu labda mpaka itakapoonekana wae walioingia fainali.

SOMA ZAIDI:Hizi Ndio Pesa Za CAF Kwa Kila Hatua Ligi Ya Mabingwa

Leave A Reply


Exit mobile version