Kuna upepo hivi sasaa unasambaa kama moto wa mafuta ya petroli kuwa inakuwaje kwenye ligi moja mdhamini aweze kudhamini timu 6 kwenye ligi moja? Kwa maana hiyo kumeendelea kuibuka tena kwamba hizi timu ndogo zinazodhaminiwa na GSM kupitia kampuni ya Haier kuwa  zinaipa Yanga matokeo ya bure kwa sababu tu zinatokana na mdhamini kuwa mmoja.

Swali la kujiuliza je Simba na Azam na zenyewe zimedhaminiwa na GSM? mbona wanakula kichapo kama kawaida? Au tujiulize swali jepesi dogo kabisa ambalo kila mmoja anaweza kujiuliza Azam anadhamini timu 16 kwenye ligi kuu Tanzania bara je naye anashiriki kuifanya ligi kuwa ya mchekechea? Mbona mpo kimya??

Wanasema siku zote ukiwa na timu mbovu unatafuta kila aina ya sababu na kuandaa propaganda mbalimbali ili kuwafanya tu watu waache kuzungumzia jinsi ambavyo timu yako haifanyi vizuri au kuwa na matokeo ambayo hayaridhishi.

Hata ukiangalia kwenye mashindano makubwa ya CAF champions league na kwenyewe YANGA inahonga? Nadhani ni wakati wa kubadilika na kuamini kuwa kuna kipindi timu inaweza kufanya vizuri na kuna wakati pia tunapaswa kuamini kuwa kuna wakati timu itakua katika kipindi kigumu na kushindwa kufanya vizuri hata kama mtakua mmesajili wachezaji ambao mnakua mmeaminishwa au walikotoka walikua wanafanya mengi makubwa.

Ni lazima ifikie wakati Watanzania tubadilike na tuache upumbavu. Walianza Yanga wachawi, ikaenda wanatembeza bahasha, sasa upepo upo kwa GSM kudhamini timu 6 hawataki na imekuwa mada kuu kwa sasa na hii inaonesha ni jinsi gani mafanikio na mabadiliko ya utendaji ndani ya klabu ya Yanga yanavyowaumiza kichwa.

SOMA ZAIDI: Alichofanya Mwigulu Kwa Ihefu Ni Kawaida Tu Katika Mpira

2 Comments

  1. Pingback: Simba vs Singida Tutegemee Mchezo Wa Aina Gani? - Kijiweni

  2. Pingback: Tuendelee Kuuamini Ukuta Wa Yerikho Simba SC? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version