Baada mahakama ya usuluhishi barani Ulaya kuja na taarifa kuhusu European Super League ni michuano halali hivyo inaweza kuendelea kama ilivyopangwa klabu mbalimbali zimetoka hadharani kupinga kujiunga na ligi hiyo.

Unaweza ukawa unajiuliza kwanini, sababu kubwa ni moja ESL ni mshindani wa karibu wa UEFA hivyo kuanza kwa michuano hii kutapoteza mvuto wa UEFA, hivyo kuepusha hili kwa kuwa UEFA ndio wameshika kwenye mpini basi kwa kushirikiana na FIFA wameweka vikwazo kwa vilabu vya ulaya chini ya Shirikisho lao EUROPEAN CLUBS ASSOCIATION ( ECA) chini ya Mwenyekiti wake Al KHELAIFI ambaye alichukua kijiti kutoka kwa Rais wa Juventus Andrea Agnelli ambaye alijiondoa kutokana kuunga mkono European Super League.

Baadhi ya vikwazo hivyo kwa klabu yoyote itakayoshiriki michuano hiyo basi itakuwa imejiondoa kwenye uanachama wa FIFA,ULAYA na hata Shirikisho la nchi husika na hata wachezaji pia wameweka ugumu huo.

Hivyo moja kwa moja vilabu vinaogopa michuano ya ESL licha ya kuwa inatoa pesa nyingi na lengo lake ni kuongeza uchumi wa klabu kwani wanaamini michuano ya UEFA haitoi pesa nyingi.

Ndomaana Real Madrid kupitia Rais wake Florentino Perez yupo mstari wa mbele kuunga mkono michuano hii mipya akiungwa mkono na Barcelona lakini bado inaleta migogoro kwa vilabu na hata mashabiki kwani wengine wanaamini mpira unaenda kununuliwa na Matajiri na kupoteza ladha yake halisi.

Lakini ugumu unakuja zaidi hapo awali kuna baadhi ya klabu kubwa ulaya ziliingia mkataba wa kushiriki michuano hiyo ambao kwa sasa wanajitoa kitu ambacho Florentino Perez akishirikiana na wenzake wanapinga kuwa klabu hizo zimejiondoa bila kufuata sheria bali wameogopa vitisho vya Rais wa UEFA Alexander Ceferin.

Kiufupi ngoma bado mbichi, ndo kwanza imeibuliwa upya kila mtu anatetea upande wenye maslahi kwake.

Endelea kusoma zaidi kuhusu uchambuzi kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version